Mbowe na tafakuri zake...

Mbowe na tafakuri zake...

MNYIKA

HUJANIJIBU naona unaendelea kulumbana na KULIKONI wakati mie ndiye niliyeuliza maswali

hebu nijibu kwa ufupi mswali NILIYULIZA HAPO AWALI nayo ni yafuatayo:


1. JE, NI KWELI FREEMAN MBOWE ANASOMA VYUO 3 TOFAUTI NCHI 3 TOFAUUTI? KAMA NI KWELI NI VYUO VIPI?



2. JE, KATIKA VYUO HIVYO ANASOMEA KOZI ZIPI? MASOMO HAYO YANACHUKUA MUDA GANI?



3. YUKO KWENYE KIWANGO (Level) GANI?



4. JE, ANAUHUSIANO GANI NA NDESAMBURO?




5. JE, ANAUHUSIANO GANI NA LUCY OWENYA?



6. JE, ANAUHUSIANO GANI NA GRACE KIHWELU?




8. JE, MAJOR DONORS (WAFADHAILI) WAKE NI AKINA NANI?
 
Dr.WHO,

Really?

But sijatoa maana na dhamira ya thread husika. Au ulifungua thread ili iwe kama ilivyokuwa inaelekea? I did not notice that it's your intention to where we were redirecting ourselves. Kama dhamira yako ilikuwa hiyo basi mzee kumradhi nisingeruhusu watu waparane na kuhama hoja. I had to do my best to bring people back to the topic. Meanwhile; nisingependa kuchangia kwenye thread zaidi.

Am out

NB: Thanks JJ kwa hoja na naomba wengine tuendeleze HOJA



Whatever happened to the decency of communicating through PM?

NADHANI YOU SHOULD WHAT YOU DO BEST: kaa pembeni waache waheshimiwa na waungwana waendelee na hili baraza ukihitajika tutakuarifu
 
Malick,

Mimi ni mpinzani, na CCM ni wapinzani kwa mtazamo wangu.(CCM ni wapinzani wangu kama mimi nilivyompinzani kwao).

Lakini sijakataa Mbowe kuhojiwa. Ninachokataa ni Kulikoni kusema UWONGO kwamba Mbowe anasoma Shahada tatu kwa miezi 18. Huu ni uwongo wenye kupotosha. Ukiachwa ukisimama ni character assassination.

Unajua mtu akiweka hapa orodha ya maswali yanakaa katika sura ya allegations-sasa nilichosema ni kuwa ziwekwe bayana hizo hoja ambazo zinatakiwa zitolewe ufafanuzi.

Sasa kusema tu Mbowe anapata wapi pesa zake?Ilihali ameshahojiwa mara kadhaa na kusema kwamba yeye ni mfanyabiashara ikiwemo katika hii source ambayo kulikoni mwenyewe ameitumia http://www.habaritanzania.com/articles/1609/1/Mbowe-amua-kunoa-ubongo-Ulaya

Kunaacha maswali mengi kuhusu motive!

JJ

Halafu, je tumemaliza kuwahoji viongozi wetu wa serikali ambao wanawajibika kwa mujibu wa sheria na maadili kutaja mali zao? Sasa why rushing on Mbowe au Mnyika 4 that matter kabla ya kuanzia na Lowasa, Kikwete et al? Unless niridhike na motive nitabaki na hisia kuwa ni strategy and spin! Viongozi wa vyama vya siasa nao ni public figures wanatakiwa kuhojiwa, I agree!

Mwanakijiji: Kabla ya kumhoji Mbowe anzia na Lowasa!(Joke)
 
Dakta Huu una matatizo na bado hujagundua kuwa una matatizo . Anyway watu wana macho wanaona na sasa MKJJ mpe Mbowe nafasi tumsikie kwa sauti yake naamini he can do it better .haogopwi mtu hapa .
 
DrWHO:

Swali namba 1 mpaka 3 nimekujibu. Soma maelezo yangu hapa http://www.jamboforums.co.tz/showthread.php?p=26035#post26035

Kama kuna swali mahususi uliza. Ila soma kwanza!

4 mpaka 7 sijajibu. Na nimesema kwamba nitajibu siku nyingine kama nilivyomuahidi kulikoni- nitajibu na masuala yote ya family bussiness na viti maalumu etc yaliyoubuliwa na Chinga, Mtalii, Mswahili, Kulikoni na wewe. Wewe umeianza hii sasa. Wenzako walishaianza ila sipendi kudandia basi kwamba mbele. Nataka nijibu hoja kwa hoja.

Nimemjibu Kulikoni kwa sababu yeye ndiye aliyeanzisha hii hoja. Wewe ulichofanya ni kuiweka thread tofauti kwa hiyo nisinge mjibu maneno yake yangebaki kwenye records kuwa ni ya kweli. Nimekujibu maswali yako kupitia yeye. Soma.

Adios. Naelekea kwenye public rally!
 
Anm sure this Forum inahitaji watu kama CCM . Hakuna viongozi wa CCM hapa wala serikali kuna wachache wenye maslahi ndiyo wanao kuja hapa kusema. Nadhani sasa baada ya malumbano ya aina Hii Chadema mnapashwa kuacha kuja hapa kujibu maswali maana badala ya maswali kuna matusi na dhihaka .Chadema endeleeni na kazi zenu badala ya kuja hapa kusema mambo ya Taifa na watu wanabaki kwenye personal life za watu nna uzushi na kupindisha mijadala. CCM hawako hapa and they have nothing to loose .kwanza watu wengi wa hii forum si wapiga kura .Akiwemo dakta hu na wengineo ila hapa wanachonga kupooteza muda . Issues nzito na majibu ya Vyama vya Siasa hayafiki Tunduru .

nashauri Chadema kaeni pembeni acheni watu wapige bla bla hapa wanajua watakalo na nyie wekeni nguvu kwa wasio kuwa na access na Dunia .
 
Lunyungu:

Nashukuru kwa ushauri wako. Nitauzingatia. Nitakuja hapa tu nikiwa na wasaa. Otherwise, kwenye niende uraiani kwa wananchi wasio hata na umeme sembuse internet!

JJ
 
MNYIKA

Unajua nilikutegemea ungeweka RECORDS STRAIGNT ILI BAADE TU MOVE ON KWENYE MAMBO MENGINE LAKINI NAONA BADO TUKO PALE PALE

kwani nimeenda katika thread uliosema UMESHAJIBU hilo swali lakini naona hujahibu kitu bali umeendelea kubishana na kulikoni:

maelezo yako ni kama yafuatayo:



Umeligusia tena suala la "digrii za Mbowe", na umeendelea kudanganya. Kwa yoyote anayejua digrii ya siasa, uchumi na falsafa ya chuo kinachotambulika duniani kama Hull haisomwi kwa miezi 18. Thats why I said, acha spinning. Tuonyeshe wapi kwenye profile ya Chuo cha Hull kunaonyesha kwamba Mbowe atasoma kwa miezi kumi na nane. Ama wapi Mbowe amesema atasoma kwa miezi kumi na nane! Acha spinning. Kadiri unavyozidi kupotosha ndio kadiri taarifa zako zitaanza kutoaminika humu. We need you kama mtetezi wa serikali unayetoa ufafanuzi toka upande wa pili. Huo ndio wajibu unaoweza kuutimiza vizuri zaidi. Huo wa character assissination waachie wenyewe humu ambao baada ya kupata majibu ya uzushi wao walitoweka kwa muda sasa wameanza kurejea kimya kimya.

Naamini unajua pia kwamba Mbowe anasoma shahada nyingine kwa distance learning.

Hiyo ya tatu kwa kadiri nijuavyo mimi hamna kitu kama hicho. Hiyo ni sehemu ya fulfillment ya programme yake ya Hull. Aliomba iwe hivyo. Sasa hii huwezi kuiita digrii, naamini kulikuwa na overlook katika habari ilipoandikwa mara ya kwanza kabisa. Na hili limewahi kutolewa ufafanuzi. Lakini unaendelea kulirejesha tena na tena na tena. Hii ndio spinning yenyewe.

But I tell you my brother-strategy is better than spinning, substance is above scandal!

Tuonyeshe source yako ya kwamba Mbowe anasoma Hull kwa miezi kumi na nane kama ulivyosema....na usihamishe mjadala...miezi kumi na nane....miezi kumi na nane..kwanza

JJ


MNYIKA

Mimi kama mwananchi ambaye kura yangu moja inaweza kumuingiza FREEMAN huko IKULU nisingependa uni bully kama ambayo unajaribu

KWA NINI USINIJIBU MASWALI STRAIGHT?

Mindhali wewe unuwezo mkubwa wa kuandika nadhani nahitaji SHORT answers kama YES au NO its that simple..

hebu nipe short and clear answers



1. JE, NI KWELI FREEMAN MBOWE ANASOMA VYUO 3 TOFAUTI NCHI 3 TOFAUUTI? KAMA NI KWELI NI VYUO VIPI?



2. JE, KATIKA VYUO HIVYO ANASOMEA KOZI ZIPI? MASOMO HAYO YANACHUKUA MUDA GANI?



3. YUKO KWENYE KIWANGO (Level) GANI?



4. JE, ANAUHUSIANO GANI NA NDESAMBURO?




5. JE, ANAUHUSIANO GANI NA LUCY OWENYA?



6. JE, ANAUHUSIANO GANI NA GRACE KIHWELU?




8. JE, MAJOR DONORS (WAFADHAILI) WAKE NI AKINA NANI?
 
Hivi Mnyika kuna sehemu gani katika katiba ilikoandikwa kuwa Mtu kuwa CCM ni DHAMBI?


Je hizo ni politics za CHADEMA au zako binafsi? hivi kwa msimamo huo kama kuna mwana CCM anataka kukipigia kura CHADEMA ataweza? maana tayari ushamwonyesha kuwa ni mtu mbaya badla ya kumjibu na kum convince kuwa your side is better than CCM lakini unakubaliana na bullying tactics unazoshauriwa uzichukue.

Sasa hiyo ni kwa msalahi ya nani? mimi kama mpiga kura inabidi uninyenyekee kura yangu na kunijibu na sio kuiburuza tuu

Mnyika YOU CAN DO BETTER THAN THIS
 
Mzee Es:

Nimeamka!

Naona mnanichokoa kusema. Nimenyamaza kwa miezi mingi kuzungumzia watu!

Iliwahi kusemwa-watu wenye akili/hekima kidogo huzungumzia watu, watu wenye akili/hekima za kawaida huzungumzia matukio, lakini watu wenye akili/hekima nyingi huzungumzia masuala. Na ndio maana wakati wote naepa kuzungumzia watu.

Lakini wewe umekwenda mbali-umeibua hoja za kumhusu Mbowe(mtu) lakini umezihusisha na Masuala(Ukweli vz Uwongo, Uongozi Vs Kuwa safi/coming clean, Kuweka kumbukumbu sahihi vs Kuchafulia jina).

Mimi nawaombeni hapa niyajadili haya masuala. Nawaomba kabisa nisijadili watu wala mtu. Na najua naweza kupata lawama toka kwa chama changu kutokana na michango ninayoitoa humu. Lakini naamini hatma ya siku ukweli utatufanya huru.

Nitachangia kiasi kuhusu Swali Na. 1 mpaka 3. Swali namba 4 mpaka 7(imeandikwa 8), nitayaacha kwa sababu mbili-mosi mjadala wa family business nimesema nitachangia siku za baadae lakini pili- mtoa hoja na hata wachangiaji wengine bado hawajasema bayana nini ni nini kinachotakiwa kutolewa ufafanuzi. Kwa hiyo kama mnataka ufafanuzi sema ni masuala yapi hayo. Na kama nilivyosema nitazungumzia masuala! Sio mtu. Na kama mnataka nizungumzie mtu au watu,basi niambieni kabisa niache kuendelea kuchangia.

Suala la Elimu ya Mbowe lilisemwa humu sana kwenye thread nyingine. Sikuchangia wakati huo nikijua hoja zilizotolewa na watu mbalimbali zilijitokeza. Lakini naona linaendelea kuibuliwa tena na tena , kwenye mijadala tofauti tofauti. Sijui ni kwa nia gani. Kila tukijadili masuala nyeti ya kitaifa Mbowe anaingizwa katikati. Inaleta hisia kwamba ni mkakati wa kuhamisha mjadala.

Suala hili limeshika chati wiki hii kutokana na hoja za Kulikoni. Nadhani hata Mzee Es ameamua kulichukua kuanzia hapo.

Sasa kwa nia ya kuchagiza mjadala na kuweka kumbukumbu sahihi nirudie hoja za Kulikoni:

1. Kwamba Mbowe anasoma Shahada tatu
2. Kwamba Mbowe anasoma Shahada hizo zote kwa miezi 18
(kulikoni aliyasema maneno hayo katika thread hii http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=2032&page=10)


Nikamwambia Kulikoni kuwa Mbowe anasoma shahada mbili: moja Hull na nyingine kwa distance Learning. http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=25927#post25927

Na nikamuomba Kulikoni alete ushahidi wa maneno yake kwamba Mbowe anasoma Shahada tatu kwa miezi 18 ama walau atuambie ni wapi Mbowe amesema meneno hayo:

Kulikoni akaleta ushahidi wa chanzo chake cha habari kuwa ni http://www.habaritanzania.com/articles/1609/1/Mbowe-amua-kunoa-ubongo-Ulaya

Ukisoma chanzo cha Kulikoni chenyewe utaona amemua kudanganya(natumia neno hili badala ya neno kukosea kwasababu amerudia maneno haya mara kadhaa pamoja na kuona wazi kabisa kuwa chanzo kinasema tofauti na pamoja na kuelezwa ukweli):

Mosi: Chanzo kinasema Mbowe anasoma programu mbili. (kwa maana ya shahada mbili) ila kwa nchi tatu tofauti.) . Kwa hiyo kulikoni kusema Mbowe anasoma Shahada tatu amemua kwa dhati kabisa kupotosha. Hii inaleta hisia ya kwamba alilenga katika suala la kumchafulia Mbowe jina lake kwa kumfanya uonekane ni mdanganyifu. Sasa Kati ya Kulikoni na Mbowe nani ni mdanganyifu? Kwa bahati mbaya kwako Mbowe anasoma Hull, anasoma distance learning na kama sehemu ya digrii yake ya Hull atakwenda Japan-hii ni special arrangement ambayo amepanga kuifanya kwa ajili ya kupata exposure ya masuala ya middle East)

Pili: Chanzo kimesema Mbowe atasoma kwa miaka mitatu. Kulikoni amesema Mbowe atasoma kwa miezi 18. Kwa hiyo Kulikoni ameamua kudanganya. Kwa motive gani? Ama unataka ijengeke picha kuwa Mbowe anasoma digrii ya uzushi ama ya kununua kama zile za Udaktari wa Mawaziri kadhaa wa Serikali ya CCM ya awamu ya nne ya Kikwete? Kwa bahati mbaya kwako ukweli unajulikana wazi kuwa Mbowe yuko Hull ambacho ni moja ya vyuo vinavyoheshimika.

Nimeandika kwa kifupi. Nimeepuka kuandika kwa kina- na siwezi kuandika kwa kina kwa kuwa sipendi kujiingiza katika mjadala wa kujadili watu, sitaki kila sentensi niandike Mbowe, Mbowe, Mbowe, Mbowe. Nataka nipate wasaa wa kujadili masuala ya nchi.

Mimi nami ni kiongozi wa kisiasa. Na watu wanaamini maisha ya kiongozi wa kisiasa ni maisha ya umma. Kila kitu lazima kifahamike kwa umma. Lakini kumbuka hata mwanasiasa ni binadamu na anayo maisha yake binafsi. Yanakuwa tu yakujadiliwa kama yana uhusiano na masuala ya umma. Binafsi huwa naweka mambo wazi lakini si kila kitu. Uanike kila njia unayotaka kupita ili wapinzani wako wakuwekee vikwazo? Kama CCM waliweza kutuma mtu kwenda Kenya kufanya Booking ya Helikopta katika kampuni ambayo CHADEMA ilipanga kukodi Helikopta inashindwaje leo nikisema naenda kusoma chuo fulani mkaanza kuweka kauzibe? Ndio maana hata Mbowe alitangaza kuwa anakwenda Hull baada ya kufanikisha kila kitu ikiwemo visa ya kwenda masomoni. Kama Besigye anaminywa kutoka Uganda, kama Tvangirai ananyimwa kutoka Zimbabwe, wanasiasa wa upinzani waamini vipi hii Comrades Club ya CCM, ZANU PF, Movement nk? Kwa hiyo msitegee kuchokonoa tutoe kila taarifa hapa. Mambo mengine tutawaambie-UKWELI ni huu, kwa taarifa zaidi subirini miaka mitatu ijayo wakati mambo yote yamekamilika.

Kwa herini kwa leo…tutaonana panapo majaliwa………ngoja nielekee kwenye mkutano wa hadhara katika kata mojawapo Hapa Ubungo…..Hakuna Kulala, Mpaka Kieleweke.

JJ


(Mzaha)Ps: Mkimaliza kuuliza maswali haya kwa Mbowe muulize maswali kama hayo kwa Kikwete, Lowasa, Mwinyi etc…duh kwa kwa heli orodha ni ndefu na muulize maswali hayo-nani ana elimu gani, ana uhusiano gani na nani, anapata wapi pesa zake na anazitumiaje!. Lakini msiwajadili maisha yao binafsi mjadili masuala UKWELI VS UWONGO, UONGOZI Vs MASLAHI YA TAIFA etc teh teh teh, its like hide and seek(Joke)


“Mabadiliko ya Kweli, hayawezi Kuletwa na Mafisadi wale wale, wa chama kile kile, chenye uoza ule ule, wakiendeleza yale yale, eti kwa Ari, Nguvu na Kasi mpya…kwa falsafa ya Chukua Chako Mapema……Tanzania yenye neema haiwezekani”.

DrWHo,

Another spin!

Maelezo yangu ni hayo hapo juu. Na kuhusu namba 4 mpaka 7(imeandikwa 8). Nimesema; mosi, nitaandikia siku zingine, pili, ibua issues specific ambazo unataka zizijadili. Maswali yako yako too short and too general. Pitia kwanza michango yangu. Otherwise, utathibitisha maneno ya Lunyungu kwamba tunapotezeana MUDA!
 
DrWHo:

Hoja nyingine ya kupotezeana muda na kuhamisha mjadala; wapi nimesema kuwa CCM ni DHAMBI?

Wapi nimeKUBURUZA?

Naamini wasomaji watakuwa MAJAJI

JJ
 
John
Nimetoa ushauri wa bure hapa kwamba it is time Chadema kuwa kama CCM na kuendelea na kazi zingine badala ya kuja kutoa ufafanuzi wa mambo then it turn to be war . Hapa kuna makundi na fitina na hizi tumeziona kuanzia muda . Ama Chadema acheni kujibu hoja maana wengi hapa wapiga kura .Wakoi nje wanaongea mambo kupoteza muda wao . Ukweli wanaujua lakini pia wana bidii ya kupindisha ukweli wa hoja na kuwachafua watu hapa .

Kwa kuwa Chadema mnawahitaji wapiga kura , basi endeleni vijijini na kuachana na hawa wa huku ambao kazi yao ni ku spin na hata kutafuta ajira kwa namna ama nyingine ana kutuondoa kwenye hoja za msingi nakutuweka hapa tulipo yaani kubishana kama tusiojua lolote nakutokuwa na mwelekeo.


CCM they have nothing to loose for not being here . Kuna wasemaji wao ambao si official ila watengeneza mkate wao yote tunayajua lakini wengi wenu najua mko sincere na issues ila zinaharibiwa na watu wenye personal motives.

Chadema time to learn , Mtanzania na majiungu tu na si issues .Kweli kwa njia hi CCM watatawala hadi mwisho.
 
Wandugu, acheni mchezo. Mimi ni moja ya watu wanaopinga sana kujadili pua za watu badala ya issues. Lakini lazima tuweke mambo in proper perspective. Ukishakuwa kiongozi wa umma, ubinafsi wa mambo yako unapungua mno. So a leader is both a person and an issue. Maswali yaliyoulizwa kuhusu Mbowe ni valid as a public leader; more importantly, a leader of a serious political party such as CHADEMA. Kwa hiyo sisi tulio wanachama wa hiki chama na wapenzi wa kiongozi wetu huyu mpendwa tunawajibika kujibu hoja za wana forum hapa ambao kwa kweli wanauliza kwa niaba ya wananchi wengine ambao hawana nafasi na uwanja wa kuuliza lakini pengine wanajiuliza maswali hayahaya vichwani mwao.

Mimi nitatoa majibu kwa baadhi ya maswali yaliyoulizwa na daktari wa falsafa wa forum hii kwa kadri ninavyoelewa. Naomba ieleweke mapema kuwa haya ni maoni yangu kwa kadri ninavyoelewa tu na wala sijatumwa na chama na wala Mbowe mwenyewe.

1) Swali: JE, NI KWELI FREEMAN MBOWE ANASOMA VYUO 3 TOFAUTI NCHI 3 TOFAUUTI? KAMA NI KWELI NI VYUO VIPI?
Jibu: Mheshimiwa Mbowe kwa sasa ni mwanafunzi wa shahada ya kwanza akisomea Bachelor of Philosophy, Economics and Political Science (PEP) katika chuo kikuu cha Hull, nchini Uingereza. Anasoma shahada hii akiwa ni mwanafunzi kamili, yaani fulltime student. Hii ni programme ya miaka mitatu, kuanzia 2006/2007 hadi 2008/2009. Kabla hajajiunga na Hull University, Mheshimiwa Mbowe pia alikuwa anasoma MBA by distance mode akiwa amejiandikisha katika chuo kikuu cha Witwatersrand, nchini Afrika Kusini. Walimu waliokuwa wanamsimamia moja alikuwa based USA na mwingine South Africa. Alishamaliza course work na hadi anaenda Hull alikuwa katika hatua ya kuandika dissertation. Hii MBA atatunukiwa na University of Witwatersrand. Kwa hivyo ni kweli kwamba huyu mheshimiwa atamaliza hizo programmes zake around the same period of time. Haishangazi basi kwamba waandishi waliliripoti kuwa Mbowe anasomea degree tatu, lakini sidhani kama ni sawa kusema anasoma katika vyuo vitatu tofauti at the same time. That sounds enigmatic. Hata hivyo inabidi tuelewe kuwa waandishi wetu wengi bado wanapenda sansational news. Ila watu wanaojua mambo ya elimu wanaelea nilichokieleza hapo juu.

Nafikiri jibu hili limejibu pia swali la 2 na 3.

4) Swali: JE, ANAUHUSIANO GANI NA NDESAMBURO?
Jibu:
i) Kindugu: Hawana
ii) Kisiasa na kikazi: Wote ni wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA. Wote ni wafadhili wakubwa wa CHADEMA.

5) Swali: JE, ANAUHUSIANO GANI NA LUCY OWENYA?
Jibu:
i) Kindugu: Hawana
ii) Kisiasa: Wote ni wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.

6) Swali: JE, ANAUHUSIANO GANI NA GRACE KIHWELU?
i) Kindugu: Hawana.
ii) Kisiasa/kikazi: As for Ndesamburo except that I am not sure if Grace is also one of the party funders.

Swali: JE, MAJOR DONORS (WAFADHAILI) WAKE NI AKINA NANI?
Jibu: Hakuna wafadhili binafsi wa Mh. Freeman Mbowe. Bali kuna wafadhili wa CHADEMA. Siwajui wafadhili wote, ninaowajua mimi ni pamoja na yeye mwenyewe Freeman Mbowe, Mzee Ndesamburo na Mzee Edwin Mtei. Sisi wanachama pia huchangia kwa kadri ya uwezo na mapenzi yetu. Kwa mfano mimi katika uchaguzi uliopita nilichangia Tsh. 250,000. Kama huo ndio unamaanisha ufadhili, basi mimi pia ni mojawapo!

Tuendelee. Kama kuna follow up questions, please!
 
THANK YOU MWANASIASA


sasa nasshangaa MNYIKA ALISHINDWA nini kujibu kama ulivyojibu

Once again thank you very much

nadhani mimi na wewe tunaweza kujadiliana sasa
 
Mwanasiasa:

Great. As I said. Swali namba 4 mpaka 7 nitatoa mtizamo wangu siku nyingine. Nashukuru umeanza. Mimi sina wasaa kwa sasa.

Ila naona umeingia kwenye mtego wa KULIKONI wa tuhuma kwa Mbowe anasoma degree tatu kwa miezi 18 na umewalaumu waandishi kwa kuandika vibaya. Kwa kifupi ni kuwa si kweli kama waandishi wameandika hivi. Tusiwasingizie katika hili. Huu ni uzushi wa KULIKONI mwenyewe ambao DrWHO naye ameubeba bila kuhoji. Mimi nilihoji na kumwambia amepata wapi hizo habari akaleta chanzo hiki http://www.habaritanzania.com/articles/1609/1/Mbowe-amua-kunoa-ubongo-Ulaya ambacho kimetokana na gazeti la Mwananchi ambalo ndio gazeti pekee wakati Mbowe anaondoka lilifanya mahojiano naye.

Gazeti halisemi digrii tatu wala miezi 18. Linasema programu mbili kwa miaka mitatu. Kwa hiyo the bottom line is KULIKONI et al waliamua kupotosha! Spinning that in tantamount to character assassination. Wajitokeze wakiri makosa ndio tuendelee kujadili mengine!

Thanx.

JJ
 
MWANASIASA

By the way nitarudi baadae kukuliza maswali toka kwenye majibu yako
 
Mwanasiasa:

Great. As I said. Swali namba 4 mpaka 7 nitatoa mtizamo wangu siku nyingine. Nashukuru umeanza. Mimi sina wasaa kwa sasa.

Ila naona umeingia kwenye mtego wa KULIKONI wa tuhuma kwa Mbowe anasoma degree tatu kwa miezi 18 na umewalaumu waandishi kwa kuandika vibaya. Kwa kifupi ni kuwa si kweli kama waandishi wameandika hivi. Tusiwasingizie katika hili. Huu ni uzushi wa KULIKONI mwenyewe ambao DrWHO naye ameubeba bila kuhoji. Mimi nilihoji na kumwambia amepata wapi hizo habari akaleta chanzo hiki http://www.habaritanzania.com/articles/1609/1/Mbowe-amua-kunoa-ubongo-Ulaya ambacho kimetokana na gazeti la Mwananchi ambalo ndio gazeti pekee wakati Mbowe anaondoka lilifanya mahojiano naye.

Gazeti halisemi digrii tatu wala miezi 18. Linasema programu mbili kwa miaka mitatu. Kwa hiyo the bottom line is KULIKONI et al waliamua kupotosha! Spinning that in tantamount to character assassination. Wajitokeze wakiri makosa ndio tuendelee kujadili mengine!

Thanx.

JJ



JJ

nilikupa nafasi ya kuweka sawa mambo kuhusu hayo maswali lakini ukana na kuandika NAKALA NDEFU ambazo hazikujibu maswali


lakini baada ya MWANASIASA kujibu naona umeamua ku BANDWAGON ...nashangaa mwanzo uliaga unaenda kuongea na wananchi lakini bado upo tuu vipi?


Binafsi nadhani MWANASIASA amefanya kazi ambayo tangu ulipolog in leo leo ulishindwa kuifanya na hii inanifanya ni question hata uwezo wako wa kujibu hoja

MWANSIASA assuming wewe ni member wa CHADEMA nadhani its time mkamtafuta mtu ambaye ataweza kujibu haya mambo ya INTERNET na kama ni mnyika then kuna umuhimu wa kumpiga BRUSH aachane na NAKALA ndefu ambazo wasomaji ni wa chache na ambazo hazijibu wala kuweka msimamo wa chama chake open
 
) Swali: JE, NI KWELI FREEMAN MBOWE ANASOMA VYUO 3 TOFAUTI NCHI 3 TOFAUUTI? KAMA NI KWELI NI VYUO VIPI?
Jibu: Mheshimiwa Mbowe kwa sasa ni mwanafunzi wa shahada ya kwanza akisomea Bachelor of Philosophy, Economics and Political Science (PEP) katika chuo kikuu cha Hull, nchini Uingereza. Anasoma shahada hii akiwa ni mwanafunzi kamili, yaani fulltime student. Hii ni programme ya miaka mitatu, kuanzia 2006/2007 hadi 2008/2009. Kabla hajajiunga na Hull University, Mheshimiwa Mbowe pia alikuwa anasoma MBA by distance mode akiwa amejiandikisha katika chuo kikuu cha Witwatersrand, nchini Afrika Kusini. Walimu waliokuwa wanamsimamia moja alikuwa based USA na mwingine South Africa. Alishamaliza course work na hadi anaenda Hull alikuwa katika hatua ya kuandika dissertation. Hii MBA atatunukiwa na University of Witwatersrand. Kwa hivyo ni kweli kwamba huyu mheshimiwa atamaliza hizo programmes zake around the same period of time.

Sikuwa najua kwamba you can do a Masters degree (MBA) before an undergraduate degree (or even cheti cha form six!). And I didn't know that you can actually graduate the same day for both graduate and undergraduate degrees! Kumbe inawezekana!

By the way, I appreciate majibu ya Mwanasiasa na JJ lakini I thought maswali yaliulizwa kwa Bwana Mbowe kama mwanachama mwenzetu wa JF. Unless, Mwanasiasa na JJ waseme wanajibu kwa niaba ya Bwana Mbowe, the record will never be straightened-up unless aje Bwana Mbowe mwenyewe.
 
Mbowe ana form 6 we should not spin this one again . Majibu haya kama huyapendi unangoja aje mwenyewe basi kazi maana tumeshindwa kumpata, Makamba , JK , EL , na wengineo wengu kuja humu kutuelezea tunayo yauliza .

MKJJ mhoji Mbowe tumalizane na uozo huu wa hoja za kila siku ambazo hazilisaidii Taifa kuendelea ilei tuishie kweney hoja za kuendeleza Tanzania .
 
Back
Top Bottom