Mbowe na tafakuri zake...

Mbowe na tafakuri zake...

Mzee Ngurumo,

With all respect, maneno yanayokuhusu yakiwekwa hapa, kama yana kasoro ni wajibu wako kuja na kuyarekebisha, kama una ubavu, ukitukanwa hapa basi wewe ni kuja hapa kujibu hayo matusi kiroho mbaya, but kama huwezi, basi ni kulala mbele na kuwaachia wananchi waendelee kukata ishus, lakini kutuambia maneno ya majina na the rest of your story hapana happa wrong place!

Kama umeamua kutumia jina lako la kweli, heshima mbele, nia na madhumuni hapa ni kunadika yale ambayo nyinyi media mmeshindwa kuyaandika, kutokana na kuwa either upande wa ccm au upinzani, na sisi wananchi sio wajinga maana tulishalijua hilo mapema ndio maana tukajiunga na kijiwe, kwa hiyo mzee endele kutupa mavitus lakini umetukuta hatuna macho na wewe toa yako bro, infact, hiki kijiwe hatujawahi kulaumiwa na wakubwa wa nchi kwa kutumia majina ya bandia, ila tumelaumiwa kwa kutoa maneno mengi mazito ambayo yanawaudhi wakubwa, ndio maana tukatemwa na jamaa majuzi juzi, kijiwe kidumu na wembe ni ule ule tu kumkoma nyani!

Heshima hapa forum huletwa na hoja, na sio majina ya ukweli au bandia, it is all about hojas bro!
 
Dua: nahisi itabidi usome tena maandishi ya Ngurumo; nimesoma hoja zako zilizoelekezwa kwake sioni kabisa ni hoja ipi hasa unamjibu (sorry for my ignorance)!
 
Tatizo hapa watu wanajua kusema chochote tu wanachojisikia.Kwa vile tu ule uzushi eti mbowe anaandikiwa course work na Ngurumo haujasimama kama walivyotegemea sasa wakielezwa na waliemsingizia wanajifanya hawajamuelewa.Chukua Tano Ngurumo kwa kuja hapa kuwafanya waongo waumbuke.
Naamini mawe yamewafikia walengwa!
 
I see! Na kama kuna mtu nakubali uvumilivu wake basi ni kijana Mnyika. Sijui how come nowadays haonekani JF. Huenda yuko kusiko mtandao. Jitihada za kujibu hoja zote zinazoilenga CHADEMA kwa ushirikiano na Eric Ongara (naye haonekani nowadays) zimewafanya watu kadha wa kadha kuijua CHADEMA kwa undani.


WORM:

Nashukuru ndugu. Ni kweli nilikuwa nje ya mtandao. Lakini kila nipatapo fursa nasoma na kuchukua hatua zinazostahili. Lakini nilishatoa udhuru hapa kuwa sitakuwa tena mchangiaji wa mara kwa mara http://www.jamboforums.co.tz/showthread.php?p=26733#post26733 ila jua kwamba nafuatilia kwa karibu na kila itakapolazimu kuchangia nitachangia.

Ngurumo asante kwa kujitokeza

JJ
 
Ngurumo

Hivi hata kabla ya kuanza kujibu hoja humu ulianza kuwasaka wachangiaji wa hii JF ili uwafahamu maana yake ni nini hasa? Unaogopa kitu gani kusema bila kuwachunguza wachangiaji? Hii inaonyesha jinsi ulivyo filisika kimawazo i.e. unaangalia nani kasema nini badala ya hoja iliyotolewa. Inaonyesha jinsi ambavyo bado una safari ndefu katika masomo yako kama ni kweli na uelewa wako.


Unaongelea elimu, tulikuwa na Mkwawa, Kinjekitile, Mirambo, Chaburuma etc. waliweza kuongoza makabila tofauti na kutufikisha katika fani tofauti tofauti. Mfano Mkwawa aliweza kuwapiga Wajerumani na kuweza kuwakomesha katika vita yao ya kwanza, na walilifahamu hili, bila shaka uliona jinsi walivyojizatiti mara ya pili. Kuna kitu kinaitwa elimu dunia, sio lazima ukae darasani tu kuwa na elimu.

Vile vile hakuna sheria ya whistle blowers Tanzania unataka wale wanaoleta nyeti za viongozi (mfano wakubwa wao wa kazi) wawafahamu, you must be joking! Where is the freedom of speech? Una maanisha kama mtu hakusoma kutokana na definition yako asichangie? Mbona hao waliosoma ndio wametufikisha hapa! (PANAPONUKA) Sasa hiyo elimu ina maana gani kama kila siku mnaimba kwa kutegemea kura kwa wasiosoma lakini kwenye mawazo hamuwataki.

Tunafahamu waandishi wengi wanatumiwa na wale wanaowawekea kitoweo mezani, huwezi kukata mkono unaokulisha hivyo huandika yale ambayo hayako mioyoni mwao bali ya vikaragosi wao kwa hiyo hubadilika na kuwa vibaraka.

Ngurumo kukata mzizi wa fitna wapo ambao watafungua forum kwa wale wanaopenda kutumia majina halisi n.k. ni uchaguzi. Usije hapa na kutuletea longolongo ambalo halina maslahi kwa Taifa. Kama umekwazwa jibu hoja na weka ukweli, waswahili husema kwenye uongo ukweli hujitenga.

Ngugu yangu DUA,

Mbona hoja yangu ilikuwa wazi?

Nimesoma maandishi yako na nimegundua kwamba:

Unaogopa kufahamika na unadhani wanaojitahidi kukufahamu wamefilisika. Binafsi nimejieleza kwamba I am curious. kama unadhani curiosity hiyo haipaswi kunifikisha katika kutaka kujua watu ninaowasiliana nao, basi fikiri upya. Lakini una haki ya kuwa na maoni yako. Sitayaingilia.

Nionavyo mimi, na ninavyoelewa, ukiwafahamu watu unaojadiliana nao mjadala unanoga. Kule kuwajua kuna-shape hata lugha unayotumia. Unachagua maneno yanayolingana na ujumbe unaokusudia kufikisha, unaoshahabiana na upeo wa calibre ya wanaokusikiliza au kukusoma. Hii ni sehemu ya etiquette za mawasiliano. Kama nimekosea kukufahamu, ndugu yangu niwie radhi. Maana naona nimegusa nyongo yako! Pole! Ila sasa napata shida. Nitafanyaje ili nisikufahamu baada ya kuwa nimekufahamu? Changamoto hiyo!

Hata hivyo, nimegundua kwamba wewe nami tunakubaliana katika mambo mengi ya msingi uliyojadili kuhusu identity, elimu, na waandishi kutumiwa. Tunachotofautiana ni approach.

Kwa mfano, mimi sikuubeza usomi wa mtu yeyote. Nilichosisitiza ni kwamba kuna watu katika forum hii wanadhani wamesoma sana, wana upeo kuliko wenzao, kiasi cha kubeza wengine. Nikahoji kwamba hata mimi nikiwachunguza hao wanaobeza wenzao, sioni usomi katika maandishi yao. Usiwe na shaka. Naelewa vema tofauti kati ya elimu na usomi; ujuzi na vyeti. Huu pia ni mjadala mwingine unaoweza kujitegemea. Lakini kwa sababu nimeshakufahamu, usihofu; kama kuna hoja tutajadiliana tu. Hatuna sababu ya kurushiana maneno. Tujadiliane.

Nimefarijika na kauli mbiu yako ya Dua la Kuku Halimpati Mwewe, ambayo ni sehemu ya jina lako la kalamu kwenye forum hapa. Wakati ningependa ukumbuke hoja ya msingi iliyonifanya niingie kwenye forum hii, si vibaya nikukuhakikishia kwamba sitakasirika kwa sababu ya ukali wa kauli zako. Hayo nakutana nayo sana sehemu nyingi. Binadamu hatufanani na hatulingani. Na kama wewe ni kuku, basi mimi ni mwewe! Nina hakika dua lako halitanipata!

Siku nyingine, Dua, punguza hasira, jenga hoja kama unavyosisitiza.

Nimemsoma pia Mzee ES.

Amenishauri kwamba nikitukanwa nami nijibu kiroho mbaya! Namhakikishia kwamba sitajibu matusi bali hoja kama zitakuwapo, na kama zitakuwa zinahitaji kujadiliwa nami pia.

Kwamba kuna mambo mengi sisi watu wa media tumeshindwa kuyafanya, nakubali. Yapo. Tunayajua. Na tunajitahidi kujikosoa. Usisahau kuwa nasi ni binadamu kama wewe na mwingine. Tunakosea, tena sana. Jambo muhimu ni kutambua kwamba tunakosea, tukayarekebisha na kusonga mbele tukiwa watu wapya, kuliko kuyang'ang'ania au kuyakana.

Kwamba ni jambo la kipuuzi mtu kuuma mkono unaomlisha (kama alivyodokeza Dua), kila mmoja wetu anajua. Na ndiyo maana tumekuwa tukielezana kuwa walioajiriwa na serikali kufanya kazi ya serikali waifanye kweli kweli, watumikie mikataba yao, maana tunawalipa mishahara na posho; na wasitulaumu tunapokata kuwaunga mkono au kuwasaidia. Wao wamo katika chombo chenye nguvu na mabavu; sisi wengine tutabaki kuwa midomo na masikio ya raia wanyonge wasio na kauli. Ila tunakumbusha kuwa katika kufanya hiyo, watofautishe maslahi ya umma na ya watawala. Na wakizingatia ethics za kazi yao, hakuna litakaloharibika.

Hata sasa kama unasoma habari za nyumbani nadhani umeona malumbano yanajitokeza katika media hizo hiyo. Ni harakati ambazo labda zinatusaidia kuliweka taifa letu katika ramani mpya ya utawala.

Pamoja na hayo yote, nadhani ujumbe uliokusudiwa umefika. Waliochukia approach yangu, poleni na samahani. Nadhani sasa mmeshaanza kutabasamu ili muweze kuenmdelea kujenga hoja ( au kukata issue kama anavyosema Mzee ES.) Kwa kuwa nanyi ni watu wazima kama mimi, nadhani mnaelewa. Ndio ukubwa wenyewe huo!
 
Mzee Ngurumo,

Heshima mbele mkuu, naomba kurekebisha hoja kidogo, tunapowalaumu media ya bongo, tunawalaumu kwa sababu wanawa-mislead wananchi kwa makususdi kutokana na hela chache wanazopewa na viongozi kuanzia wa ccm mpaka upinzani,

kwa hiyo sisi hapa sio wendawazimu kwamba hatuelewi maana ya mapungufu au kuteleza kwa binadamu katika shughuli zake za kila siku, hapana tatizo ni pale tu wanapopindisha ukweli kwa makusudi, na tunawajua wote wanaoandika kwa kuridhisha wanaowapa pesa, na wanaoandika kwa misingi na utaalamu wa media ambayo ni kazi yao!

Otherwise tuendeleee kukata ishus, tena kiroho mbaya!
 
Hahahahahahaha.....misamiati ya Mzee Es inaniacha hoi kishenzi.......'kukata issue' 'mwendo mdundo' 'heshima mbele' 'mawe' etc. etc.........

Super big ups Es
 
Ngurumo

Hata kama unanifahamu sasa unafaidika nini na hilo? Wewe pamoja na Serikali ambayo inajifanya inatumia UWT mna tofauti gani? Hususan you as CHADEMA hata hamjatawala mnakuwa na mawazo potofu kama haya. Mimi sitishiki na vibaka na vibaraka huwa nasimamia msimamo thabiti; Lakini utaona kutokana na tabia ambayo inajionyesha utakuwa ni mjadala ambao ni pungufu i.e. malengo yake ni haba. Kama umeamua kujiita msomi wakati wewe ueleo wako ni haba unajidanganya mwenyewe humdanganyi JF member yoyote yule.

Kuhusu malalamiko yako ingekuwa busara ukayaweka wazi hapa yale yaliyosemwa kuhusu wewe na Mbowe na tufahamu yalitolewa katika mazingira gani? Huwezi ukaingia hapa na kuanza kuleta mambo ya bulicheka.
 
Mzee Dua,

Heshima mbele mkuu, poa mkuu ujumbe umefika inatosha, tukate ishus! turudi kwenye ishus mkuu inatosha tumewasikia!
 
Kuna mambo mawili ya msingi:

1. Ngurumo ni mwajiriwa wa Mama Mbowe na mtoto wa Mbowe (Gazeti la Tanzania Daima, linamilikuwa na kampuni ya Free Media, ambayo wakurugenzi wake ni mke na mtoto wa Freeman Mbowe)

2. Ngurumo anasomeshwa na "mwajiri" wake huko Uingereza;

3. Ngurumo alishiriki kikamilifu kwenye kampeni ya Urais wa Mbowe;

Conclusion: Huwezi kumtaja Ngurumo bila kumtaja Mbowe and vice versa. Kwahiyo, Bwana Ngurumo you are going to have to deal with it. Acha wadau tuendeleze makamuzi.
 
Naona bado kabisa watu tuna tongo za Ujamaa!..

Nashindwa kabisa kuelewa tunakoelekea ktk mada hii na lipi lengo letu!..
Ngurumo kaja kutueleza hali halisi ya huko mnakotaka kufahamu, leo yeye kawa ndio somo. Sijui mwandishi wa White house huko US huwa anachambuliwa yeye kutokana na ajira yake ama watu mnakuwa makini zaidi kwa yale anayoandika na kuyachambua.

Bila Ngurumo kuwa ktk nafasi hiyo tusingeweza kupata habari alizoandika hata kidogo!
Binafsi nitazidi kuamini kwamba hatupo hapa kumjadili mtu na nafasi yake ila tujadiliane matumizi mabaya ya nafasi aliyokuwa nayo, ikiwa Yapo!
 
Kuna mambo mawili ya msingi:

1. Ngurumo ni mwajiriwa wa Mama Mbowe na mtoto wa Mbowe (Gazeti la Tanzania Daima, linamilikuwa na kampuni ya Free Media, ambayo wakurugenzi wake ni mke na mtoto wa Freeman Mbowe)

2. Ngurumo anasomeshwa na "mwajiri" wake huko Uingereza;

3. Ngurumo alishiriki kikamilifu kwenye kampeni ya Urais wa Mbowe;

Conclusion: Huwezi kumtaja Ngurumo bila kumtaja Mbowe and vice versa. Kwahiyo, Bwana Ngurumo you are going to have to deal with it. Acha wadau tuendeleze makamuzi.

Hivi mtu anayedai huu ndio ushahidi wa fikira zake bado kuna mtu humu ndani anatokea kumsifia kama afanyavyo Mzee ES? No wonder hata Masai akawa anavishwa kila msalaba wa rushwa na unyang'au kama ilivyo kwa bosi wake kuhusu warembo..

Tanzanianjema
 
Mimi sio mfuasi wa Mbowe na ukweli ni kwamba bado sijaweza kumuamini kama kweli ana nia ya kuwasaidia watanzania lakini likija suala la uwezo kichwani huyu jamaa ni mzuri. Zamani nilikuwa namwona Ziro lakini siku ya kwanza tu nilipopata wasaa wa kuwa nae karibu na kubadilisha mawazo niligundua kuwa huyu jamaa ana upeo mkubwa kichwani (intelligence+smart)

Uzuri mwengine ni kuwa tofauti na wanasiasa wetu wengi niwajuao huyu jamaa haoni aibu kuonyesha kuwa hajui na hiyo ndio imeweza sana kumjenga kifikira na kisiasa (kiasi fulani) katika miaka ya karibuni.

Wale wanaodhania kuwa Mbowe anawategemea kina Ngurumo ama hawamjui Mbowe vizuri, wana wivu naye ama wanamjua na wanamuogopa.

Kama anafaa kuongoza Taifa letu hilo swali lingine....

Tanzanianjema
 
Tz Njema,

Msingi wa kero yangu, and therefore bandiko langu hapo juu, ni the idea kwamba Bwana Ngurumo ni objective kwenye masuala ya siasa, hasa yanayomhusu Mbowe. Cha msingi hapa ni kwamba Bwana Ngurumo asituamulie ya kujadili na namna ya kujadili. Kama anayajua majina ya kweli ya wengi wetu humu, Mwenyezi Mungu amjalie. Lakini msingi mzima wa JF ni kwa watu kuandika anonymously. Na watu tulishakubaliana hapa kwamba pre-occupation isiwe kutafutana identity...ndio maana kijiwe kinapendeza.

Karibu Jambo Forum Bwana Ngurumo.

I am willing to concede kwamba there will arrive a day when it will dawn on me kwamba perhaps Mbowe is smarter than I thought.
 
Mzee TZnjema,

Heshima mkuu wangu, this Mugongox2's thing ni the best gold ya hii forum as independent voice kutoka kwa kawaida, I mean what else can I sya about jamaa, maana naona kila kukicha akipachikwa majina mapya ambayo hayana uhusiano wowote na the man, isipokuwa chuki tu za hoja zake, hoja hujibiwa kwa hoja, sio mmoja atoe hoja ajibiwe kuwa ni agent au anatumwa, NONESENSE, let the man atumwagie vitu vyake na wewe pia endelea kutumwagia vyako, ndipo mjadala unanoga bros!

na Mzee Ngurumo, heshima mbele nimeiona article yako ya kujibu serikali kwa viongozi kuitwa wasaniii, bravo ni maneno makali na very clear, kuwa walipokuwa wanaitwa Boys11 Men walifurahia sana, bila ya kuelewa kuwa hao jamaa huko Us ni wasaniii, I kind of love it jinsi ulivyosimama kidete bila uoga, kama maoni ya gazeti hilo ambayo yalikuwa ni a big joke!
 
Mzee ES - nimekupata, nimekusikia na nakukubali. Kuna jamaa hapa wanahubiri demokrasia, lakini wanapata kinyaa kusikia maoni tofauti na ya kwao kiasi l cha kutumia matusi. For me, hitting hard is the best way to expose hipocrisy.

Like you, I liked Ngurumo's mea culpa on the usage of "Msanii" in reference to JK. Anasema neno hilo lilitumika kwa context ya kwamba hawa mabwana (Lowassa na JK) toka zamani walikuwa wanatumia neno "Boys II Men" - wanamuziki wasanii, ndio na yeye (Mbowe) akalitumia kwa maana hiyo. Kwanini asingesema tu kwamba "msanii" siku hizi Bongo manake "muongo". Period! Talk about lacking balls! Halafu leo wanataka tuwaone mashujaa who can face the establisment head on!
 
Kwa wanaharakati wote na wapenda mageuzi nikimaanisha kizazi kipya cyo kijacho kama tulivyozoea kauli za chama tawala nikimaanisha wazalendo wa kweli na wapenda nchi yao Tanzania.tatizo tulilonalo sisi watanzania wengi bado hatujaweza kujivunia na kujitambua kama sisi ni watanzania halisi na hili tu ndiyo dawa pekee ya wananchi kujua haki yao na inapobidi kuidai either kwa nguvu au tu kwa idadi ya kura na kumpatia kura yule mwenye uzalendo wa kweli.mweshimiwa mbowe harakati zako zina matunda hata kama siyo sasa hivi basi baadaye ila tu mimi ninachoona ni kwamba tunawaendea wananchi wakati wa kuomba kura tu ingekuwaje sasa hivi ukaanza mchakato wa kupita nchi nzima tuko wazalendo ambao tayari elimu yako tulishaipata tutachanga upate mafuta, kwa mfano nilifurahishwa sana baada ya kukuta wazee wa kijiji cha Nronga kama mwalimu Sawe,Mzee Eben lema wamepata changamoto ya kujua utaifa wao ,watu ambao hatukuwategemea kabisa,huo ni mwanzo mzuri.tukaze buti
 
Back
Top Bottom