1. Alipopigwa risasi Lissu Mbowe alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa hapelekwi Muhimbili.
2. Mbowe alikaa rumande na wakina Esther Matiko. Alipofungwa jela, alikataa kutoka mpaka wale wote waliofungwa nae walipotolewa jela kwa dhamana.
3. Alienda Mwanza kuungana na wenzake wakati anajua wazi kuwa atatiwa ndani na uwezekano wa kupigwa ulikuwepo.
4. Alikaa ndani kwa takriban miezi minane. Alipoachiwa alikubali mualiko wa Samia kwenda Ikulu, ambako chimbuko likawa mada ya maridhiano.
5. Kutokana na hayo maridhiano wanachama wa CDM waliokuwa nje waliweza kurudi, mikutano ya hadhara na zaidi ya yote mamia ya wanachama na wafuasi wa CDM waliweza kuachiwa kutoka rumande na jela.
6. Alipopigwa Lissu Mbeya, Mbowe alienda kuungana nae. Matokeo yakawa ya yeye kukamatwa na kurudishwa Dar.
7. Aliitisha maandamano ya kupinga mauaji na kupotea kwa watanzania ikiwa pamoja na wanachama wa Chadema. Lissu alizuiwa nyumbani kwake. Lema akakamatwa airport. Mnyika akajifungia kwa maista. Sijui Heche alikuwa wapi. Mbowe hakulala nyumbani siku ya maandamano kwa sababu alijua watamzuia kutoka. Akaibuka sehemu ya kuanzia maandamano akiwa yeye na binti yake. Mashujaa wafia Chadema hawakuonekana hata mtu mmoja.
8. Alitoa shilingi zaidi ya milioni 250 kufanikisha mkutano mkuu wa chama. Alihakikisha kuwa uchaguzi mkuu unakuwa wa haki na uwazi. Haku endorse mtu katika uchaguzi huo tofauti na mshindani wake ambae aliendorse watu kama aliyekuwa mgombea wa uenyekiti wa Bawacha.
9. Mara baada ya uchaguzi alimpongeza aliyeshinda akajiondokea.
Baada ya uchaguzi tumeshuhudia wale waliokuwa Team Lissu wakiendeleza mapambano dhidi ya Mbowe. Wanawake wa Bawacha walioenda kumsalimia baada ya uchaguzi walionyeshwa wazi wazi kuwa uongozi wa sasa hawakufurahia kitendo chao. Sigrada alimsifia Mbowe mbele ya Lissu, matokeo yakawa ni kichapo. Lissu akamsimanga Aida hadharani.
Yote hayo bado mnataka Mbowe akajipendekeze kwa wakina Heche?
Wanacho sahau keyboard warriors ni kuwa Mbowe alijijengea heshima kubwa na kuna watu wengi hawafurahi wanapoona anavyodhalilishwa na kuvunjiwa heshima. Watu kama G55 ni lazima wanaumia wanapo shuhudia yote hayo. Lakini kila kitu kina mwisho wake.
Amandla...