Mbowe apewe heshima yake anayostahili!!

Mbowe apewe heshima yake anayostahili!!

Yaani unataka watu wauawe, wateswe, uchaguzi uchafuliwe mara ngapi ili uone umuhimu wa mabadiliko ya Sheria za uchaguzi na Katiba?

Kama mtu una akili timamu kipi kinakuzuia kutambua kuwa kuanzia mwaka 2019, 2020,2024 uchaguzi uliharibiwa na huo ndiyo utakuwa muendelezo Kwa uchaguzi wa mwaka 2025?

Ni akili za aina gani zinazomfanya mtu kusubiri afanyiwe kosa Kwa zaidi ya mara ya tatu ndipo apambanie haki au utu wake!?
Na mtu mwenye akili timamu atasusia mara ngapi kabla ya kutambua kuwa mwenzake hana nia ya kubadilisha Katiba? Hamtagombea mwaka 2029 kama hapatakuwa na reforms? Na mwaka 2030 kama bado hamna mabadiliko? Hivi mnaamini kuwa CCM wataona aibu kutangaza uchaguzi kwa sababu tu CDM wamesusa?

Kwani miaka yote hii ambayo CDM wamekuwa wakigombea walikuwa hawapiganii haki na utu wao? Hamna kitu kinachomtisha bully kama kujua kuwa victim wake ataendelea kupambana nae hata amfanyie nini. Hakainde Hichilema aligombea mara 5 kabla ya kushinda mara ya sita. Alifanyiwa kila aina ya uonevu lakini hakukata tamaa. Nyinyi mara tatu ndio mnataka kufyata mkia. Congress party ya India ilitawala kwa miaka 30 baada ya uhuru wao lakini mwishowe wakatolewa kwenye utawala.

Kushindana na chama kilichotawala toka nchi ipate uhuru sio kazi rahisi. Inahitaji uvumilivu na kuto kata tamaa.
Inaonekana CDM imekata tamaa.

Amandla...

Amandla...
 
Hoja ya ajabu kabisa! Yaani watu wamezoezwa na watawala kuwa haki zao watapewa kwa hisani!
Hebu niambie mtapataje haki zenu nje ya sanduku la kura? Mnategemea EU watawapamania? Au Mahakama ndio itawapa ushindi? Clubhouse ndio zitawapa ushindi? Mpaka sasa hivi mmeshindwa kusema mtahakikishaje uchaguzi haufanyiki. Basi tuambieni mbinu mtakayotumia nje ya sanduku la kura?

Amandla...
 
Na mtu mwenye akili timamu atasusia mara ngapi kabla ya kutambua kuwa mwenzake hana nia ya kubadilisha Katiba? .
Mandela alikataa kwa miaka zaidi ya 27 kuachiliwa huru kwa masharti yasiyo na maslahi Kwa wananchi.
Kushindana na chama kilichotawala toka nchi ipate uhuru sio kazi rahisi. Inahitaji uvumilivu na kuto kata tamaa.
Inaonekana CDM imekata tamaa.
Badala ya kusema CHADEMA wamekata tamaa wewe ndiyo umekata tamaa. Kama CHADEMA wangekuwa wamekata tamaa hiyo mikutano wanayofanya ni ya kazi gani Sasa?
 
Mandela alikataa kwa miaka zaidi ya 27 kuachiliwa huru kwa masharti yasiyo na maslahi Kwa wananchi.

Badala ya kusema CHADEMA wamekata tamaa wewe ndiyo umekata tamaa. Kama CHADEMA wangekuwa wamekata tamaa hiyo mikutano wanayofanya ni ya kazi gani Sasa?
Unamfananisha Lissu na Mandela? Wakati wote ambapo Mandela alikuwa ndani chama kilikuwa vitani na utawala wa makaburu. Hawakusema kwa sababu watoto wao waliuliwa Sharpeville basi mapambano basi!

Hivi seriously unaamini kuwa CCM watakubali mabadiliko kwa sababu tu ya mikutano ya hadhara? Mikutano ambayo wanaweza kuizuia siku yeyote wakitaka. Na wakiizuia, hizo kampeni zenu mtazifanyia wapi?

Amandla...
 
Wanachodai CHADEMA ni uchaguzi huru na wa haki. Inawezekanaje kuamini kuwa mfumo wa uchaguzi unaoupinga unaweza kukupa haki?

Mantiki ya kushiriki kwenye uchaguzi usioamini mifumo yake ya uendeshaji, ni uwendawazimu!
Swali ni kuwa watafanya nini kama hayo madai yao yatapuuzwa? Wataendelea kukaa pembeni mpaka lini?
CUF walisusa baada ya kufanyiwa dhulma ya wazi wazi. Leo warithi wao hawataki kusikia neno kususa. Mnatakiwa mjifunze kwao.

Amandla...
 
Freeman Aikaeli Mbowe ni mwanasiasa ambaye huwezi kuzungumzia siasa za Tanzania bila ya kutaja jina lake. CHADEMA hii ya sasa ina mchango mkubwa sana wa juhudi za Mbowe kuifanya iwe imara.

Pamoja na mitizamo yetu dhidi yake, lakini tumheshimu yeye kama binadamu na mtu aliyechangia sana uimara wa CHADEMA
Mbowe apewe heshima yake!
Naunga mkono hoja. Nimemwelewa sana Mbowe, usipoteze imani na Rais Samia. Alivyo kwa Kauli na Matendo hawezi kuwa ni yeye!
P
 
Swali ni kuwa watafanya nini kama hayo madai yao yatapuuzwa? Wataendelea kukaa pembeni mpaka lini?
CUF walisusa baada ya kufanyiwa dhulma ya wazi wazi. Leo warithi wao hawataki kusikia neno kususa. Mnatakiwa mjifunze kwao.
CUF ipi?

Bado mawazo ya wengi ni ya kibinafsi kuwa ni lazima wao ndiyo wafaidike na mifumo bora ila wao hawapo tayari kupigania uwepo wa mifumo bora kwa ajili ya kizazi kijacho! CHADEMA ya sasa inapigana kwa ajili ya CHADEMA ya kizazi kijacho.

Leo hii vyama vya siasa vya upinzani vinafaidika na marekebisho ya Sheria ya mikutano ya hadhara yaliyotokana na Christopher mtikila kupeleka kesi mahakamani. Jee Mtikila bado yupo?
 
Yaani unataka watu wauawe, wateswe, uchaguzi uchafuliwe mara ngapi ili uone umuhimu wa mabadiliko ya Sheria za uchaguzi na Katiba?

Kama mtu una akili timamu kipi kinakuzuia kutambua kuwa kuanzia mwaka 2019, 2020,2024 uchaguzi uliharibiwa na huo ndiyo utakuwa muendelezo Kwa uchaguzi wa mwaka 2025?

Ni akili za aina gani zinazomfanya mtu kusubiri afanyiwe kosa Kwa zaidi ya mara ya tatu ndipo apambanie haki au utu wake!?
Yaani kuna aina ya binadamu kwa reasoning yao nabaki nashangaa kama ni binadamu kamili na timamu.

Kitu kile kile kimetokea mara nne, leo eti unaamini tu kuwa kinawezekana kisiendelee kutokea tena!!??

Watu wameuwawa mwaka jana tu, tena kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, kipi kitakuhakikishia kuwa kesho hawatakufa wengine kwenye uchaguzi mkuu!!??
 
Ushahidi wa 2020 umesaidia nini?

Ushahidi wa local govt, 2024 umesaidia nimi?

Huo ushahidi unapelekwa wapi?
Yaani kuna aina ya binadamu kwa reasoning yao nabaki nashangaa kama ni binadamu kamili na timamu.

Kitu kile kile kimetokea mara nne, leo eti unaamini tu kuwa kinawezekana kisiendelee kutokea tena!!??

Watu wameuwawa mwaka jana tu, tena kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, kipi kitakuhakikishia kuwa kesho hawatakufa wengine kwenye uchaguzi mkuu!!??
 
CUF ipi?

Bado mawazo ya wengi ni ya kibinafsi kuwa ni lazima wao ndiyo wafaidike na mifumo bora ila wao hawapo tayari kupigania uwepo wa mifumo bora kwa ajili ya kizazi kijacho! CHADEMA ya sasa inapigana kwa ajili ya CHADEMA ya kizazi kijacho.

Leo hii vyama vya siasa vya upinzani vinafaidika na marekebisho ya Sheria ya mikutano ya hadhara yaliyotokana na Christopher mtikila kupeleka kesi mahakamani. Jee Mtikila bado yupo?
Kumbe CDM inapigania kizazi kijao cha CDM na sio watanzania wote?

Mimi maswali yangu yanabaki pale pale. 1. Chadema itahakikisha vipi kuwa uchaguzi haufanyiki kama hamna reforms zote za maana.
2. Na je wataendelea na mkakati huo huo mwaka 2029, 2030, 2034, 2035 na kuendelea kama CCM itaendelea kukataa mabadiliko ya maana?
3. Mtahakikisha vipi kuwa wafuasi wenu hawaumizwi, hawatekwi, hawafunguliwi mashtaka ya ajabu na hata kuuawa wakati wa hizo jitihada za kuhakikisha uchaguzi haufanyiki? Tumeona Slaa ameswekwa ndani bila reaction yeyote kutoka CDM. Leo Mwenyekiti yuko ndani na hali ni hiyo hiyo. Au mnangojea kibali cha serikali ili mumpigania kiongozi wenu aachiwe?

Amandla...
 
Yaani kuna aina ya binadamu kwa reasoning yao nabaki nashangaa kama ni binadamu kamili na timamu.

Kitu kile kile kimetokea mara nne, leo eti unaamini tu kuwa kinawezekana kisiendelee kutokea tena!!??

Watu wameuwawa mwaka jana tu, tena kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, kipi kitakuhakikishia kuwa kesho hawatakufa wengine kwenye uchaguzi mkuu!!??
Nani amesema kuwa watu hawataumizwa n.k.? Mnatuhakikishiaje vipi kuwa wafuasi wenu hawataumizwa wakati wanafuata njia mliochagua? Mimi sielewi mnategemea kupata mabadiliko vipi kwa kususia uchaguzi huku mkiepuka kuumizwa?

Wazanzibari wanaheshimiwa kwa sababu inajulikana kuwa hawatakata tamaa hata waumizwe vipi. Na wataendelea kusimamisha wagombea wao katika uchaguzi.

Amandla...
 
Freeman Aikaeli Mbowe ni mwanasiasa ambaye huwezi kuzungumzia siasa za Tanzania bila ya kutaja jina lake.

Lakini naona Baada ya uchaguzi wa Januari 21 mwaka 2025, Kuna baadhi ya watu wanapambana kwa kila Hali kuonesha kuwa Mbowe alikuwa mamluki ndani ya CHADEMA na alikitumia chama kwa faida yake.

Mimi nakubaliana na wale wanaosema kuwa baada ya Mbowe kukaa madarakani CHADEMA kwa zaidi ya miaka 20, Kuna mambo alianza kutoyapa umuhimu na umakini wake kwenye kusimamia mambo ya msingi ulipungua.

Lakini ukweli lazima usemwe, CHADEMA hii ya sasa ina mchango mkubwa sana wa juhudi za Mbowe kuifanya iwe imara.

Wengine tunaomfahamu Mbowe tangu mwaka 2004 tunajua ni kwa kiasi gani amepambana kuifanya CHADEMA iwe hivi ilivyo.

Pamoja na mitizamo yetu dhidi yake, lakini tumheshimu yeye kama binadamu na mtu aliyechangia sana uimara wa CHADEMA hii ambayo sote ni wafuasi wake!

Kama tunaona Mbowe hakuna jema alilolifanya ndani ya CHADEMA, Iko siku na Lissu naye tutamdharau hivi hivi tunavyomdharau Mbowe.

Tukubaliane tu kwamba ni watu wachache sana waliopambana kama Mbowe ndani ya CHADEMA wakati akiwa kiongozi. Mbowe apewe heshima yake!
Vijana wengi kama Ben Saanane tumpempoteza kwenye mikono ya Mbowe na mpaka mzee Kibao inasemekana Mbowe kuna mkono wake.
 
Kumbe CDM inapigania kizazi kijao cha CDM na sio watanzania wote?
Hapa si tunazungumzia CHADEMA? Kwani watanzania wote ni wanasiasa. Au hata hujui mjadala unahusu nini?
Au mnangojea kibali cha serikali ili mumpigania kiongozi wenu aachiwe
Kwa hili la Lissu wewe ulitaka CHADEMA wafanyeje?
 
Siasa za visasi havitaisaidia Chadema.Jana Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Kilimanjaro Bazil Lema amesimamishwa eti kwa kuandaa mkutano wa wanachadema wanaotaka kuhama chama.
Kwa mujibu wa Lema kikao cha kumsimamisha kingefanywa na kamati ya maadili ya Kanda kwa mujibu wa katiba..Anadai hakuna kikao kilichofanyika na amearifiwa kwa barua tu bila kuitwa.Tuhuma ni kwamba kuna mtu aliripoti kwamba ameambiwa Bazil Lema anaandaa mkutano.
Akihojiwa na Moshi FM Bazil Lema amedai chama kimekuwa kinaendeshwa kwa matamko na sio Katiba.
Tulisema sana kabla ya uchaguzi hawa sio viongozi bali ni kundi la walalamikaji,hawana kesho hawa,wamejaa ubabe bila uwezo wa ubabe
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Mbowe alikamatwa kwa ugaidi, Lissu akiwa hoi hospitali hakukaa kimya. Mdude labda ameshauawa, ila Mbowe hajali kabisa

Leo Lissu anataka kunyongwa makengeza utafikiri kafa, hasemi chochote. Kwahiyo kutetea haki siku hizi mpaka uwe na cheo???

Genge lake limepora mpaka akaunti za mitandao ya kijamii ya chama, yuko kimya na makengeneza yake.

Mbowe ni tapeli na alikuwa anaendesha CDM kama kampuni yake binafsi, na huko aliko anatamani kabisa Chama kife ionekane bila yeye mambo hayaendi.

Tapeli la kimachame
Kama Lisu na nyie mlisema yeye ndio mharibifu,huyo mharibifu na tapeli mnamtaka wa nini sasa hivi.Mbowe kanyamaza ila kila siku mnamtaja kuliko mnavyomtaja Mungu.Hapo yuko Kimya siku akiongea si ndio mtazimia na hao viongozi wenu watatu Heche,Lema na Lisu.Kwanza Lema kashafunga mdomo baada ya kujua upumbavu aliiofanya.
 
G 55?
 
Back
Top Bottom