Mbowe apewe heshima yake anayostahili!!

Mbowe apewe heshima yake anayostahili!!

Freeman Aikaeli Mbowe ni mwanasiasa ambaye huwezi kuzungumzia siasa za Tanzania bila ya kutaja jina lake.

Lakini naona Baada ya uchaguzi wa Januari 21 mwaka 2025, Kuna baadhi ya watu wanapambana kwa kila Hali kuonesha kuwa Mbowe alikuwa mamluki ndani ya CHADEMA na alikitumia chama kwa faida yake.

Mimi nakubaliana na wale wanaosema kuwa baada ya Mbowe kukaa madarakani CHADEMA kwa zaidi ya miaka 20, Kuna mambo alianza kutoyapa umuhimu na umakini wake kwenye kusimamia mambo ya msingi ulipungua.

Lakini ukweli lazima usemwe, CHADEMA hii ya sasa ina mchango mkubwa sana wa juhudi za Mbowe kuifanya iwe imara.

Wengine tunaomfahamu Mbowe tangu mwaka 2004 tunajua ni kwa kiasi gani amepambana kuifanya CHADEMA iwe hivi ilivyo.

Pamoja na mitizamo yetu dhidi yake, lakini tumheshimu yeye kama binadamu na mtu aliyechangia sana uimara wa CHADEMA hii ambayo sote ni wafuasi wake!

Kama tunaona Mbowe hakuna jema alilolifanya ndani ya CHADEMA, Iko siku na Lissu naye tutamdharau hivi hivi tunavyomdharau Mbowe.

Tukubaliane tu kwamba ni watu wachache sana waliopambana kama Mbowe ndani ya CHADEMA wakati akiwa kiongozi. Mbowe apewe heshima yake!

Asiyeamini kwenye no reforms no elections si mwenzetu, ninakazia:

"Anayejiita CHADEMA asiyeamini kwenye "no reforms no elections" huyo si mwenzetu!" Miluzi mingi ya nini?

imhotep, Drifter, Erythrocyte, binti kiziwi na wale ndugu wengine au nasema uongo?
 
Ooh sawa,hebu tuambie mkishindwa kuzuia uchaguzi nini kitaendelea!!?maana hapo mahakamani penyewe walinzi wa malkia wanavunja watu miguu.Naomba ufafanuzi tafadhali

Kwani wewe unataka uchaguzi bila reforms? Kumbe ili iweje? Kwani wewe ni mnufaika kwenye kile chama nufaika kusipokuwa na reforms? Ufafanuzi wako kwanza tafadhali.
 
Siyo lazima kwasababu ni TAPELI.

Limeshakula ruzuku, ambazo ni kodi za walalahoi, sasa hivi linacheua tu makengeza juu.

KIna mdude wameuawa hata

Siyo lazima kwasababu ni TAPELI.

Limeshakula ruzuku, ambazo ni kodi za walalahoi, sasa hivi linacheua tu makengeza juu.

KIna mdude wameuawa hata udiwani hawajapata
Sasa huyo mnaemuita TAPELI ndio mnalialia kwanini hajitokezi kuwatetea??

Kazi kweli kweli!
 
Walimunsiku zote ni viazi sikulaumu.

Leta ushahidi hapa mimi nataka.Mbowe anitetee.

Makengeza Mbowe anafanya siasa za Pesa, hajawahi kutetea mtu.
 
Freeman Aikaeli Mbowe ni mwanasiasa ambaye huwezi kuzungumzia siasa za Tanzania bila ya kutaja jina lake.

Lakini naona Baada ya uchaguzi wa Januari 21 mwaka 2025, Kuna baadhi ya watu wanapambana kwa kila Hali kuonesha kuwa Mbowe alikuwa mamluki ndani ya CHADEMA na alikitumia chama kwa faida yake.

Mimi nakubaliana na wale wanaosema kuwa baada ya Mbowe kukaa madarakani CHADEMA kwa zaidi ya miaka 20, Kuna mambo alianza kutoyapa umuhimu na umakini wake kwenye kusimamia mambo ya msingi ulipungua.

Lakini ukweli lazima usemwe, CHADEMA hii ya sasa ina mchango mkubwa sana wa juhudi za Mbowe kuifanya iwe imara.

Wengine tunaomfahamu Mbowe tangu mwaka 2004 tunajua ni kwa kiasi gani amepambana kuifanya CHADEMA iwe hivi ilivyo.

Pamoja na mitizamo yetu dhidi yake, lakini tumheshimu yeye kama binadamu na mtu aliyechangia sana uimara wa CHADEMA hii ambayo sote ni wafuasi wake!

Kama tunaona Mbowe hakuna jema alilolifanya ndani ya CHADEMA, Iko siku na Lissu naye tutamdharau hivi hivi tunavyomdharau Mbowe.

Tukubaliane tu kwamba ni watu wachache sana waliopambana kama Mbowe ndani ya CHADEMA wakati akiwa kiongozi. Mbowe apewe heshima yake!
Mbowe kajivunjia heshima mwenyewe. Alipokubali kutumika na sasa kutumia vijana njaa wake kwa sababu alishindwa uchaguzi. Amejidhalilisha mwenyewe.
 
Walimunsiku zote ni viazi sikulaumu.

Leta ushahidi hapa mimi nataka.Mbowe anitetee.

Makengeza Mbowe anafanya siasa za Pesa, hajawahi kutetea mtu.
Mimi siyo CDM, wala siyo mfuasi wa mwanasiasa.

Hoja yangu ni kuwa, kutetea haki za watu ni lazima Mbowe awe na cheo??
Hapa ulikuwa unamaanisha nini?
 
Huyu huyu ambaye mmemwita tapeli na majina mengine mabaya leo mnashangaa kwa nini yuko kimya??
Mimi siyo CHADEMA.

Ila naliita tapeli. Kwasababu limedanganya watu kwa muda mrefu sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom