Mbowe apewe heshima yake anayostahili!!

Mbowe apewe heshima yake anayostahili!!

Freeman Aikaeli Mbowe ni mwanasiasa ambaye huwezi kuzungumzia siasa za Tanzania bila ya kutaja jina lake.

Lakini naona Baada ya uchaguzi wa Januari 21 mwaka 2025, Kuna baadhi ya watu wanapambana kwa kila Hali kuonesha kuwa Mbowe alikuwa mamluki ndani ya CHADEMA na alikitumia chama kwa faida yake.

Mimi nakubaliana na wale wanaosema kuwa baada ya Mbowe kukaa madarakani CHADEMA kwa zaidi ya miaka 20, Kuna mambo alianza kutoyapa umuhimu na umakini wake kwenye kusimamia mambo ya msingi ulipungua.

Lakini ukweli lazima usemwe, CHADEMA hii ya sasa ina mchango mkubwa sana wa juhudi za Mbowe kuifanya iwe imara.

Wengine tunaomfahamu Mbowe tangu mwaka 2004 tunajua ni kwa kiasi gani amepambana kuifanya CHADEMA iwe hivi ilivyo.

Pamoja na mitizamo yetu dhidi yake, lakini tumheshimu yeye kama binadamu na mtu aliyechangia sana uimara wa CHADEMA hii ambayo sote ni wafuasi wake!

Kama tunaona Mbowe hakuna jema alilolifanya ndani ya CHADEMA, Iko siku na Lissu naye tutamdharau hivi hivi tunavyomdharau Mbowe.

Tukubaliane tu kwamba ni watu wachache sana waliopambana kama Mbowe ndani ya CHADEMA wakati akiwa kiongozi. Mbowe apewe heshima yake!
Kwenye mapambano yoyote unahitaji mwanzo mzuri na mwisho mzuri hayo ndio tunayoyajua,katika siasa ukiwa na mwanzo mzuri,usipokuwa mwangalifu lzm utakuwa na mwisho wa kijinga kama ule wa Mbowe na unaweza ukatoa picha yako halisi iliyokuwa imejificha siku nyingi, CHADEMA ilifanya Demokrasia halisi,wajinga wanalaumu matunda ya Demokrasia ya kweli ikiwa ni pamoja na Mbowe mwenyewe inasikitisha sana,badala ya chama kuwa kimoja wanajitojeza washenzi wachache tuliowaamini kwamba Wana Akili kumbe tulikosea kwa kuwa amini punguani kuwa na Akili.Kundi la G55 lililojiondoa CHADEMA Lina hoja zilizojificha za kimapenzi tu,wengi pale wake zao ndio wale COVID 19 watu kama John Mrema na Salum mwalimu hawana hoja wake zao ndio wale COVID 19 na kukubali kuwa chawa wa Mbowe.
 
Heshima yake iliishia siku ile aliyotangaza kugombea dhidi ya Lisu.

Wenye akili timamu walilisema hili kabla hata hajatangaza.

Huyo Mzee kuna sensor ni mbovu upstairs,hawezi hata kusoma alama za nyakati???

Imagine leo amekuwa wa kuombewa heshima!! Yaani watu ni wa kukumbusha wema wake leo??
 
Mbowe alikamatwa kwa ugaidi, Lissu akiwa hoi hospitali hakukaa kimya. Mdude labda ameshauawa, ila Mbowe hajali kabisa

Leo Lissu anataka kunyongwa makengeza utafikiri kafa, hasemi chochote. Kwahiyo kutetea haki siku hizi mpaka uwe na cheo???

Genge lake limepora mpaka akaunti za mitandao ya kijamii ya chama, yuko kimya na makengeneza yake.

Mbowe ni tapeli na alikuwa anaendesha CDM kama kampuni yake binafsi, na huko aliko anatamani kabisa Chama kife ionekane bila yeye mambo hayaendi.

Tapeli la kimachame
Makengeza tena mlevi wa kutupa
 
Mi siasa nimezichukia mazima. Tabia mbaya za kiafrika ni kuchagua madhaifu ya watu na kuwahukumu na kusahau mema mengine yote. Upuuz mtupu
Inategemea mizani unayopimia hayo "mema"na "mabaya" ina calibration gani.

Kwa mfano, jengea nyumba watu 100 kisha kata kichwa cha mtu mmoja aliyekuita mpumbavu. Halafu tarajia watu waseme: japo alikata kichwa cha mtu lakini alikuwa na "mema" mengi. Hakuna binadamu asiye na mapungufu.
 
Lakini cha ajabu ni kuwa, sasa yuko kwenye harakati za chini kwa chini kuidhoofisha CHADEMA chini ya uongozi mpya wa Tundu Lissu na wenzake...

Ukimya wake ktk wakati huu ambapo chama unachodai kuwa alikijenga kwa jasho na damu, kinapitia ktk wakati mgumu wa mashambulizi kutoka pande zote; i.e CCM na serikalI yao pamoja na taasisi zake kama polisi, TISS, Msajili wa vyama vya siasa, mahakama na kutoka ndani ya chama chenyewe kwa waliokuwa chawa wake wakati wa uchaguzi wakisaidiwa na CCM kumtaka aendelee ni uthibitisho wa wazi sana kuwa, yuko kwenye harakati za kumdhoofisha mwenzake (Tundu Lissu) ionekane hawezi kuongoza chama kama alivyokaa yeye miaka 22 asijue kuwa isingekuwa kina Lissu hawahawa, asingekaa muda mrefu hivyo...

Mimi badala ya kumheshimu, nimemdharau kabisa na namuona kama mtu mwenye ego na ubinafsi. Na hii ni udhihirisho kuwa, alijenga chama ambacho yeye na baadhi wenzake walikigeuza kama mradi wa kisiasa kufanyia deal zao za kifedha kutoka kwa CCM na serikali yao...

Kuona kuwa kitega uchumi chao sasa kiko chini ya viongozi wengine tena waadilifu wasiojihusisha na bishara za kisiasa kwa CCM na wanausafisha uchafu waliouficha miaka mingi ndani ya chama, inawauma na kuibua vita mpya dhidi ya uongozi mpya kwa msaada wa waliokuwa wanafanya nao biashara ya kisiasa yaani CCM na serikali yao ovu...
Ndiyo maana Chadema ilikuwa inaitwa Saccos ila tukawa tunapinga kumbe kweli mwamba alikuwa anapiga pesa kutoka Ccm
 
1. Alipopigwa risasi Lissu Mbowe alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa hapelekwi Muhimbili.
2. Mbowe alikaa rumande na wakina Esther Matiko. Alipofungwa jela, alikataa kutoka mpaka wale wote waliofungwa nae walipotolewa jela kwa dhamana.
3. Alienda Mwanza kuungana na wenzake wakati anajua wazi kuwa atatiwa ndani na uwezekano wa kupigwa ulikuwepo.
4. Alikaa ndani kwa takriban miezi minane. Alipoachiwa alikubali mualiko wa Samia kwenda Ikulu, ambako chimbuko likawa mada ya maridhiano.
5. Kutokana na hayo maridhiano wanachama wa CDM waliokuwa nje waliweza kurudi, mikutano ya hadhara na zaidi ya yote mamia ya wanachama na wafuasi wa CDM waliweza kuachiwa kutoka rumande na jela.
6. Alipopigwa Lissu Mbeya, Mbowe alienda kuungana nae. Matokeo yakawa ya yeye kukamatwa na kurudishwa Dar.
7. Aliitisha maandamano ya kupinga mauaji na kupotea kwa watanzania ikiwa pamoja na wanachama wa Chadema. Lissu alizuiwa nyumbani kwake. Lema akakamatwa airport. Mnyika akajifungia kwa maista. Sijui Heche alikuwa wapi. Mbowe hakulala nyumbani siku ya maandamano kwa sababu alijua watamzuia kutoka. Akaibuka sehemu ya kuanzia maandamano akiwa yeye na binti yake. Mashujaa wafia Chadema hawakuonekana hata mtu mmoja.
8. Alitoa shilingi zaidi ya milioni 250 kufanikisha mkutano mkuu wa chama. Alihakikisha kuwa uchaguzi mkuu unakuwa wa haki na uwazi. Haku endorse mtu katika uchaguzi huo tofauti na mshindani wake ambae aliendorse watu kama aliyekuwa mgombea wa uenyekiti wa Bawacha.
9. Mara baada ya uchaguzi alimpongeza aliyeshinda akajiondokea.

Baada ya uchaguzi tumeshuhudia wale waliokuwa Team Lissu wakiendeleza mapambano dhidi ya Mbowe. Wanawake wa Bawacha walioenda kumsalimia baada ya uchaguzi walionyeshwa wazi wazi kuwa uongozi wa sasa hawakufurahia kitendo chao. Sigrada alimsifia Mbowe mbele ya Lissu, matokeo yakawa ni kichapo. Lissu akamsimanga Aida hadharani.
Yote hayo bado mnataka Mbowe akajipendekeze kwa wakina Heche?

Wanacho sahau keyboard warriors ni kuwa Mbowe alijijengea heshima kubwa na kuna watu wengi hawafurahi wanapoona anavyodhalilishwa na kuvunjiwa heshima. Watu kama G55 ni lazima wanaumia wanapo shuhudia yote hayo. Lakini kila kitu kina mwisho wake.

Amandla...
 
Freeman Aikaeli Mbowe ni mwanasiasa ambaye huwezi kuzungumzia siasa za Tanzania bila ya kutaja jina lake.

Lakini naona Baada ya uchaguzi wa Januari 21 mwaka 2025, Kuna baadhi ya watu wanapambana kwa kila Hali kuonesha kuwa Mbowe alikuwa mamluki ndani ya CHADEMA na alikitumia chama kwa faida yake.

Mimi nakubaliana na wale wanaosema kuwa baada ya Mbowe kukaa madarakani CHADEMA kwa zaidi ya miaka 20, Kuna mambo alianza kutoyapa umuhimu na umakini wake kwenye kusimamia mambo ya msingi ulipungua.

Lakini ukweli lazima usemwe, CHADEMA hii ya sasa ina mchango mkubwa sana wa juhudi za Mbowe kuifanya iwe imara.

Wengine tunaomfahamu Mbowe tangu mwaka 2004 tunajua ni kwa kiasi gani amepambana kuifanya CHADEMA iwe hivi ilivyo.

Pamoja na mitizamo yetu dhidi yake, lakini tumheshimu yeye kama binadamu na mtu aliyechangia sana uimara wa CHADEMA hii ambayo sote ni wafuasi wake!

Kama tunaona Mbowe hakuna jema alilolifanya ndani ya CHADEMA, Iko siku na Lissu naye tutamdharau hivi hivi tunavyomdharau Mbowe.

Tukubaliane tu kwamba ni watu wachache sana waliopambana kama Mbowe ndani ya CHADEMA wakati akiwa kiongozi. Mbowe apewe heshima yake!
Either you are not serious au unaleta utapeli JF. Wakati Mbowe akiwa Mwenyekiti for over 20 yrs mafanikio yake yalitokana na support ya haohao akina Tundu Lissu. Kwanini yeye Leo baada ya. Kushindwa uenyekiti hataki kuwapa support akina hao hao akina Lissu ili chama kiendelee kuimarika?! Kwamba waliokuwa wakimpa support yeye akiwa Mwenyekiti walikuwa wajinga?! Halafu apewe heshima, kwa kipi?! Mambo hayawezi kwenda namna hiyo.
 
Mbowe huko uliko endelea na mishe zako, achana na hizi people za Tanzania - zenye ushujaa online physically chenga. Tena shukuru Mungu umeachana nao ukiwa mzima wa afya, ungekuwa umetobolewa jicho au ungekuwa kilema, familia yako ingekuwa ndo inahasara.
Watz ni wanafiki na wajinga sana - Mdude katekwa, kapigwa badala ya kulianzisha kutaka warudishwe - mko busy na NO REFORM NO ELECTION..halafu mnakaa mnamlaumu Mbowe.
Yaani nyinyi watu wa CDM mko kama vifaranga vya kuku - mwewe anakuja anajinyakulia amtakaye - hakuna mnachofanya seriously. Yaani nyinyi watu wenu wa muhimu wanatekwa, wanapotezwa, wanauliwa - mko busy na mikutano, kula nyama na bia za bure wengine..halafu mnamsema Mbowe...

Mbowe huko uliko kunywa bia, enjoy na familia yako..
 
Freeman Aikaeli Mbowe ni mwanasiasa ambaye huwezi kuzungumzia siasa za Tanzania bila ya kutaja jina lake.

Lakini naona Baada ya uchaguzi wa Januari 21 mwaka 2025, Kuna baadhi ya watu wanapambana kwa kila Hali kuonesha kuwa Mbowe alikuwa mamluki ndani ya CHADEMA na alikitumia chama kwa faida yake.

Mimi nakubaliana na wale wanaosema kuwa baada ya Mbowe kukaa madarakani CHADEMA kwa zaidi ya miaka 20, Kuna mambo alianza kutoyapa umuhimu na umakini wake kwenye kusimamia mambo ya msingi ulipungua.

Lakini ukweli lazima usemwe, CHADEMA hii ya sasa ina mchango mkubwa sana wa juhudi za Mbowe kuifanya iwe imara.

Wengine tunaomfahamu Mbowe tangu mwaka 2004 tunajua ni kwa kiasi gani amepambana kuifanya CHADEMA iwe hivi ilivyo.

Pamoja na mitizamo yetu dhidi yake, lakini tumheshimu yeye kama binadamu na mtu aliyechangia sana uimara wa CHADEMA hii ambayo sote ni wafuasi wake!

Kama tunaona Mbowe hakuna jema alilolifanya ndani ya CHADEMA, Iko siku na Lissu naye tutamdharau hivi hivi tunavyomdharau Mbowe.

Tukubaliane tu kwamba ni watu wachache sana waliopambana kama Mbowe ndani ya CHADEMA wakati akiwa kiongozi. Mbowe apewe heshima yake!
Hakuna mwana Chadema ambaye anamdharau ila wanachama wanasikitika kwa Mbowe kuwa nyuma ya Genge 55 ambao wanaihujumu Chadema
 
Mtoto akililia wembe mpe. Heche alimwambia Mbowe kuwa tutakushinda katika uchaguzi ili tukuonyeshe kuwa tumekomaa. Na kweli wakafanya hivyo. Sasa wafuasi wao mnamlilia nini Mbowe?

Amandla...
Hakuna mtu anamlilia Mbowe.

Wanaomlilia Mbowe ninwafuasi wake.

Sis siyo hata wanaCHADEMA, ila ni wapemda haki tu.

Wala huhitaji kuwa mfuasi wa CHADEMA kuona uovu aliofanyiwa Lissu au Mdude. Hizp siyo siasa.

Ila Mbowe haoni shida, ni haki ipi alikiwa anapogania??
 
Mbowe kajishushia heshima mwenyewe kwa kukataa ushauri wa kung'atuka kwa heshima kabla ya uchaguzi.Baada ya kushindwa uchaguzi na makamu wake,ni wazi heshima aliyojijengea imetikisika hakuna la ajabu.Kitendo chake cha kususia uongozi mpya ndicho kitakachomaliza heshima yake kabisa kwani kila mtu aliona uchaguzi kufanyika kwa haki
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom