Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,980
Ni kweli Katiba inatamka kwamba Spika atajiuzulu mbele ya Bunge, na nikweli kabisa kwamba Spika alipaswa kujiuzulu mbele ya Bunge. Lakini ukweli uliowazi kwamba yeye kiu ya kuongoza Bunge imeisha kipindi ambacho hakuna Bunge linaendelea. Ilikuwa haiwezekani kujiuzulu mbele ya Bunge maana ilo Bunge halijakaa litakaa February
Endapo angeitisha bunge maaalumu kwa ajili ya kutangaza kujiuzulu mambo mawili yangetokea yasiyo na tija
1. Angevunja katiba kwa sababu kujiuzulu kwake hakujatajwa kwamba ataitisha Bunge la dharura.
2. Wabunge wangelazimika kulipwa stahiki za vikao vya dhararu pesa ambayo Ingetokana na kodi za wananchi na may muhimili wa serekali unaotunza fedha ungeweza kuzalisha audit query au Kugoma kulipa Kama ambavyo umewahi kuingilia bunge Hadi wakarejesha fedha kwa JPM
Kwa msingi huo Mhe Ndugai yupo sahihi kumjulisha Katibu wa Chama na kuwapa nakala Bunge Kwa ajili yakuanza maandalizi ya kujaza nafasi itakayokuwa wazi kikatiba hapo February. Hivyo takwa la kikatiba litatimizwa kwenye kikao kijacho Cha Bunge ambacho kitapokea taarifa rasmi ya kujiuzulu uspika na baadaye taratibu za kumpata spika mpya kufanyika.
Nimwombe Mhe. Mbatia asiangaike kwenda Mahakamani maana anachotaka kifanyike leo kisingeweza kufanyika hadi February. Kwa tafsiri nyingine Bunge halina taarifa rasmi yakujiuzulu kwa Spika hadi litakapokaa na kupewa taarifa ndipo mchakato wa kosheria wa kujiuzulu utakapokamilika.
Mwisho, nishukuru kwamba wale wote walioshindwa kutumia akili na maarifa waliyopewa na Mwenyenzi MUNGU wanavuliwa nguo. Ndugai alishindwa kujua Spika ana kazi gani yeye akawa anaambatana na RAIS Kila anapokwenda, akawa anapokea maelekezo Nini akafanye Bungeni, Leo wale waliomtuma wamemtumbua kwa fedhea