Peter Madukwa
JF-Expert Member
- Sep 20, 2012
- 3,135
- 2,471
Kumekuwa na mjadala kutoka baadhi ya watu mbalimbali mtandaoni juu ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Spika Mh Job Ndugai.
Ulianza mjadala kwamba kwanini ktk barua yake ameandika herufi kubwa pekee? KIMSINGI kilichosambaa mtandaoni siyo barua bali ni TAARIFA KATIKA VYOMBO VYA HABARI ambayo ni sawasawa tu na TANGAZO. Katika uandishi TANGAZO/TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NI KAWAIDA SANA KUANDIKWA KWA HERUFI KUBWA PEKEE. Barua za kujiuzulu zimewasilishwa katika bunge na katika Chama cha Mapinduzi.
Jambo la Pili nimeona Ndg James Mbatia amesema anakusudia kupeleka kesi mahakamani kupinga utaratibu uliotumika ktk kujiuzulu kwa spika. Kwamba kwa maelezo ya Mbatia ni kiwa Spika alitakiwa aende bungeni kujiuzulu kupitia ktk kamati ya bunge na bunge lenyewe.
Kimsingi hoja yake siyo sahihi. Kwa maoni yangu Mh Spika amefuata utaratibu wa kikatiba na ametimiza matakwa ya kisheria katika mchakato wa kujiuzulu.
Ukisoma katiba ya JMT sura ya 11 ibara ya 149(1)(c) imeeleza wazi kuwa endapo Spika au Naibu spika anataka kujiuzulu anatakiwa kuwasilisha taarifa hiyo katika bunge. Katiba haijatoa masharti kuwa taarifa hiyo iwe ktk mkutano, kamati au kwa barua original au nakala ya barua? Katiba imetaka tu kuwa Spika atoe taarifa katika Bunge.
Mh Spika Job Ndugai katika kujiuzulu ametoa taarifa katika bunge na chama cha mapinduzi na kwamba KWA KUWA BUNGE LIMEKIRI KUPOKEA TAARIFA YA KUJIUZULU KWA SPIKA (KAMA TAARIFA YA KATIBU WA BUNGE INAVYOJIELEZA) Basi tuhitimishe kwa kusema Spika amewasilisha taarifa yake ktk bunge na amefuata taratibu za kisheria za kujiuzulu kwa spika.
Kwa lugha rahisi Spika amejiuzulu kisheria na uchaguzi wa Spika mwingine utafanyika mwezi Februari kama ilivyotangazwa na BUNGE katika taarifa yake ya vyombo vya Habari.
BARUA RASMI YA KUJIUZULU KUTOKA KWA SPIKA KWENDA KWA KATIBU WA BUNGE AMBAPO NAKALA IMEELEKEZWA KWA KATIBU MKUU WA CCM.
UPDATES: Tarehe 28.1.2022
Mahakama imetupilia mbali kesi ya kikatiba ya kupinga kujiuzulu kwa SPIKA.