Jinsi ‘mikono’ ya Serikali ilivyotishia uhuru Bunge sintofahamu ya kujiuzulu Ndugai

saidoo25

JF-Expert Member
Jul 4, 2022
602
1,407
Spika wa Bunge, Job Ndugai anadaiwa huenda kujiuzulu kwake nafasi ya Spika alilazimishwa na hakujizulu kwa matakwa yake kama ilivyoripotiwa.

"Mbali na mawazo hayo, kuliibuka kauli mitandaoni kwamba kiongozi huyo alijiuzulu kwa kulazishwa, jambo ambalo halikuthibitishwa wala kukanushwa"

Source: Gazeti la Mwananchi
Jinsi ‘mikono’ ya Serikali ilivyotishia uhuru Bunge
Alhamisi, Desemba 15, 2022
 
Ndugai alikuwa mkuu wa muhimili, analazimishwa vipi kujiuzulu bila ya kura ya bunge kutokuwa na imani na Spika?

Angekataa kujiuzulu tuone kama wangemvua uanachama.

Na hata wangemvua uanachama, hilo lingemuondolea ubunge tu, kuwa Spika wa bunge sio lazima uwe mbunge.

Marehemu Dr. Aleck Che Mponda aligombea Uspika bila ya kuwa mbunge.

Ndugai kwa njia moja au nyingine alikubali kujiuzulu yeye mwenyewe.

Kuna mtu anaitwa Preet Bharara, huyu alikuwa US State Attorney for the Southern District of New York, a presidential appointment. Rais Trump alikuwa hampendi, akawa anamfanyia figisu ajiuzulu. Jamaa likasema sijiuzulu ng'o, nataka nione unanifukuza kazi, dunia nzima ijue nimefukuzwa kazi na Trump, sijajiuzulu.

Trump akamfukuza kazi, dunia nzima ikajua Preet Bharara amefukuzwa kazi na Donald Trump.

Kwa nini Ndugai hakusimamia anachoamini na kukataa kujiuzulu mpaka afukuzwe tuone kafukuzwa clearly bila chengachenga?
 
Yaezekana alitengenezewa mazingira threat ya kwake au wanafamilia serikali hawashindwi kufanya umafia akaona isiwe taabu
Tatizo Watanzania tunapenda sana speculations za "inawezekana". Na siwalaumu sana, serikali yetu yenyewe haina uwazi na ina historia mbaya sana.

Lakini.

Kama aliwekewa threat hivyo kwa nini hakusema?

Mbona Mrisho Gambo, pamoja na historia yake yote, kasema?

Without discrediting his main point regarding debt, which is debatable, Ndugai ni mtu weak tu, na mtu mjinga aliyekuwa anaropoka bila mpango. Hakutakiwa hata kuwa Spika, ndiyo maana kashindwa kutetea alichosema.

Mimi nampa lawama Ndugai, kwa sababu, tukienda na "the facts of the case", vitu vinavyojulikana wazi bila utata, Ndugai kajiuzulu mwenyewe, hakulazimika kujiuzulu.

Haya mambo mengine ya kusema labda alilazimishwa, labda alitishwa kwa kweli ni speculations tu, hakuna fact hapo.

Inawezekana pia mnaionea serikali kuivika lawama za kumtisha Ndugai, wakati Ndugai kajiuzulu mwenyewe kwa uoga wake.

Ndugai alitakiwa asimamie anachokiamini mpaka mwisho, ndiyo maana ya uongozi.

Kama kashindwa kusimamia alichokiamini mpaka mwisho, basi hafai kuwa Spika na ilifaa ajiuzulu hata bila ya kushinikizwa na serikali.
 
Tatizo ni katiba.
Ndugai alikuwa mkuu wa muhimili, analazimishwa vipi kujiuzulu bila ya kura ya bunge kutokuwa na imani na Spika?

Angekataa kujiuzulu tuone kama wangemvua uanachama.

Na hata wangemvua uanachama, hilo lingemuondolea ubunge tu, kuwa Spika wa bunge sio lazima uwe mbunge.

Marehemu Dr. Aleck Che Mponda aligombea Uspika bila ya kuwa mbunge.

Ndugai kwa njia moja au nyingine alikubali kujiuzulu yeye mwenyewe.

Kuna mtu anaitwa Preet Bharara, huyu alijuwa US State Attorney for the Southern District of New York, a presidential appointment. Rais Trump alikuwa hampendi, akawa anamfanyia figisu ajiuzulu. Jamaa likasema sijiuzulu ng'o, nataka nione unanifukuza kazi, dunia nzima ijue nimefukuzwa kazi na Trump, sijajiuzulu.

Trump akamfukuza kazi, dunia nzima iksjua Preet Bharara amefukuzwa kazi na Donald Trump.

Kwa nini Ndugai hakusimamia anachoamini na kukataa kujiuzulu mpaka afukuzwe tuone kafukuzwa clearly bila chengachenga?
 
Spika wa Bunge, Job Ndugai anadaiwa huenda kujiuzulu kwake nafasi ya Spika alilazimishwa na hakujizulu kwa matakwa yake kama ilivyoripotiwa.

"Mbali na mawazo hayo, kuliibuka kauli mitandaoni kwamba kiongozi huyo alijiuzulu kwa kulazishwa, jambo ambalo halikuthibitishwa wala kukanushwa"

Source: Gazeti la Mwananchi
Jinsi ‘mikono’ ya Serikali ilivyotishia uhuru Bunge
Alhamisi, Desemba 15, 2022
Chezea wana mtandao wewe hio habari ingine tukiamua jambo letu tunafanya na tunafanya
 
Katiba ya nchi haina "checks and balances" imara kati ya mihimili kama inavyokuwa katika demokrasia zilizo imara. Ni kweli katika nchi zote huwa kuna mhimili uliojichimbia chini zaidi lakini angalau katika demokrasia imara huwa kuna vizingiti ambavyo mhimili huo hauwezi kuvivuka kutokana na jinsi mifumo na taasisi ya nchi hizo ilivyosukwa ku contain "executive overreach".

Katika nchi na katiba hii kiongozi mkuu akitofautiana na mtumishi au kiongozi mwingine yoyote huyo mtu anaweza kuondolewa kwa wepesi sana katika nafasi yake katika wakati wowote kwa njia nyingi sana.
Tatizo gani?

Katiba ndiyo iliyomlazimisha Ndugai kujiuzulu?
 
Ndugai alikuwa mkuu wa muhimili, analazimishwa vipi kujiuzulu bila ya kura ya bunge kutokuwa na imani na Spika?

Angekataa kujiuzulu tuone kama wangemvua uanachama.

Na hata wangemvua uanachama, hilo lingemuondolea ubunge tu, kuwa Spika wa bunge sio lazima uwe mbunge.

Marehemu Dr. Aleck Che Mponda aligombea Uspika bila ya kuwa mbunge.

Ndugai kwa njia moja au nyingine alikubali kujiuzulu yeye mwenyewe.

Kuna mtu anaitwa Preet Bharara, huyu alijuwa US State Attorney for the Southern District of New York, a presidential appointment. Rais Trump alikuwa hampendi, akawa anamfanyia figisu ajiuzulu. Jamaa likasema sijiuzulu ng'o, nataka nione unanifukuza kazi, dunia nzima ijue nimefukuzwa kazi na Trump, sijajiuzulu.

Trump akamfukuza kazi, dunia nzima iksjua Preet Bharara amefukuzwa kazi na Donald Trump.

Kwa nini Ndugai hakusimamia anachoamini na kukataa kujiuzulu mpaka afukuzwe tuone kafukuzwa clearly bila chengachenga?
Kuwa spika ni lazima uwe sponsored na Chama cha siasa ata kama wewe si Mbunge
 
Halafu nani alee familia yake...!!???
 
Ndugai alikuwa mkuu wa muhimili, analazimishwa vipi kujiuzulu bila ya kura ya bunge kutokuwa na imani na Spika?

Angekataa kujiuzulu tuone kama wangemvua uanachama

Kwa nini Ndugai hakusimamia anachoamini na kukataa kujiuzulu mpaka afukuzwe tuone kafukuzwa clearly bila chengachenga?
Mkuu, Watanzania ni WANAFIKI sana! Kwa wakati ule, kelele zilikuwa kila kona za kumtuhumu! Wabunge wengi wakageuka kuwa ni CHAWA wa MWENYE NGUVU kuliko SPIKA.
Ni afadhari alivyojiuzulu "mwenywe",kwani alikuwa anaelekea KUAIBISHWA!
 
Katiba ya nchi haina "checks and balances" imara kati ya mihimili kama inavyokuwa katika demokrasia zilizo imara. Ni kweli katika nchi zote huwa kuna mhimili uliojichimbia chini zaidi lakini angalau katika demokrasia imara huwa kuna vizingiti ambavyo mhimili huo hauwezi kuvivuka kutokana na jinsi mifumo na taasisi ya nchi hizo ilivyosukwa ku contain "executive overreach".

Katika nchi na katiba hii kiongozi mkuu akitofautiana na mtumishi au kiongozi mwingine yoyote huyo mtu anaweza kuondolewa kwa wepesi sana katika nafasi yake katika wakati wowote kwa njia nyingi sana.
Katiba ya Tanzania haimruhusu rais kumuondoa Spika. Unless avunje bunge na kuitisha uchaguzi mpya kwa namna ambayo hata yeye rais anaenda kuchaguliwa tena.

Sasa katika hili katiba yetu imempa nguvu vipi rais kumlazimisha Spika ajiuzulu?
 
Rais wa Tanzania ni mwenyekiti wa CCM pia.
Na ni vigumu kuitofautisha CCM na dola.
Katiba ya Tanzania haimruhusu rais kumuondoa Spika. Unless avunje bunge na kuitisha uchaguzi mpya kwa namna ambayo hata yeye rais anaenda kuchaguliwa tena.

Sasa katika hili katiba yetu imempa nguvu vipi rais kumlazimisha Spika ajiuzulu?
 
Unaamka asubuhi unakuta barua yako ya kujiuzulu inasambaa mitandao, unashangaa "mbona mimi sijaandika hiyo!!". Alafu watu wanakiri wameshaipokea na michakato ya chama imeanza.

Unataka kutoka nje labda uongee na vyombo vya habari unakuta umewakwa chini ya ulinzi nyumbani kwako, ni umafia yaani.

Wanasema ukiua kwa upanga utakufa kwa upanga, maza asije kushangaa nayeye yakimkuta ya 'kujiuzulu' akiwa amewekwa mtu kati na 'wazalendo'.
 
Ndugai alikuwa mkuu wa muhimili, analazimishwa vipi kujiuzulu bila ya kura ya bunge kutokuwa na imani na Spika?

Angekataa kujiuzulu tuone kama wangemvua uanachama.

Na hata wangemvua uanachama, hilo lingemuondolea ubunge tu, kuwa Spika wa bunge sio lazima uwe mbunge.

Marehemu Dr. Aleck Che Mponda aligombea Uspika bila ya kuwa mbunge.

Ndugai kwa njia moja au nyingine alikubali kujiuzulu yeye mwenyewe.

Kuna mtu anaitwa Preet Bharara, huyu alijuwa US State Attorney for the Southern District of New York, a presidential appointment. Rais Trump alikuwa hampendi, akawa anamfanyia figisu ajiuzulu. Jamaa likasema sijiuzulu ng'o, nataka nione unanifukuza kazi, dunia nzima ijue nimefukuzwa kazi na Trump, sijajiuzulu.

Trump akamfukuza kazi, dunia nzima iksjua Preet Bharara amefukuzwa kazi na Donald Trump.

Kwa nini Ndugai hakusimamia anachoamini na kukataa kujiuzulu mpaka afukuzwe tuone kafukuzwa clearly bila chengachenga?
Kwa ufujaji wa pesa za umma aliofanya hui ujasiri unaotaka aoneshe angeutoa wapi? Ulitaka Mwenzio akanyee debe?
 
Back
Top Bottom