Mazungumzo kati ya Rais na Vyama vya siasa , Vyama vyaambiwa vipeleke ajenda zao kwa John Shibuda au kwa Msajili wa Vyama vya siasa Francis Mutungi

Status
Not open for further replies.
Baada ya kufika huko zitakusanywa na baadaye zitafikishwa kwa Mh Rais kwa hatua zaidi .

Francis Mutungi ni Msajili wa vyama vya siasa mwenye tuhuma nyingi za kuhujumu vyama vya siasa akishirikiana na kada mwingine wa ccm aitwaye Sisty Nyahyoza , sasa kuvitaka vyama vya siasa vipeleke ajenda zao kwa watu wa aina hii ni sawa na kuvitukana matusi ya nguoni , bila shaka jambo hili halitawezekana

Bali bado haijafahamika John Shibuda anapewa kazi ya kupokea Ajenda za vyama vya siasa kama nani .

Endelea kubaki hapa hapa JF kwa Taaifa zaidi .
Shibuda ana cheo fulanj kwenye jukwaa la vyama vya siasa....ila Mama anakosea sasa ana wasaidizi kibao ikiwemo wa siasa...na huyo waziri asiye wizara hiyo ndio kazi yake link jamii na rais kama Wasira awamu 4 alikuwa hivyo
 
Baada ya kufika huko zitakusanywa na baadaye zitafikishwa kwa Mh Rais kwa hatua zaidi .

Francis Mutungi ni Msajili wa vyama vya siasa mwenye tuhuma nyingi za kuhujumu vyama vya siasa akishirikiana na kada mwingine wa ccm aitwaye Sisty Nyahyoza , sasa kuvitaka vyama vya siasa vipeleke ajenda zao kwa watu wa aina hii ni sawa na kuvitukana matusi ya nguoni , bila shaka jambo hili halitawezekana

Bali bado haijafahamika John Shibuda anapewa kazi ya kupokea Ajenda za vyama vya siasa kama nani .

Endelea kubaki hapa hapa JF kwa Taaifa zaidi .
Acha uongo.
 
Mama anataka kudesa kabla ajakutana nao. Miki nadhani bora angeagiza aletewe moja kwa moja, hawa wapambe wanaweza wasifikishe ajenda zote.
 
Shibuda na Mutungi wanaweza kuchakachua.

Mimi nadhani yapelekwe kwa mshauri wa Rais wa mambo ya siasa!
Alipaswa kukutana na kila chama peke yake maana kila mmoja ana priorities zake ambazo zitahitaji muda kujadili. Kuwaita wote kwa pamoja ni kuwapa wapambe kama Shibuda uzito wasiostahili. Unaweza kukuta kuwa Shibuda na Msajili wa Vyama ndio watapewa nafasi ya kuzungumza kwa niaba.
Sidhani kama Chadema watahudhuria kwa utaratibu huu. Na hamna wa kuwalaumu. Zitto na Shibuda na yule dada aliyegombea urais watawakilisha upinzani unaotakiwa.

Amandla....
 
Agenda ya Chadema inajulikana maana kila siku wanaizungumzia.
1. Katiba Mpya.
2. Tume Huru ya Katiba.
3. Kufuatwa kwa Katiba iliyopo.
4. Vyombo vya dola kutowatendea haki.
5. Wanachama wao walio na kesi za ajabu ajabu.
6. Kuwajibika kwa wale ambao hawakuwatendea haki.

Kiutendaji wangetaka uwazi zaidi katika mikataba ambayo serikali inaingia.

Haya yote wameyaweka wazi wala hamna haja kusubiri wapeleke kwa Shibuda au Msajili.

Amandla....
 
Yaani wameshapewa na masharti, maana yake Rais anataka kuchambua yale atayoona yanawezekana ndio ayafanyie kazi, yasiyowezekana anayaacha.

Kwa hali hii nini maana ya kukutana na Rais kama anaogopa maswali ya papo kwa hapo? anaonekana ana nia ya kuleta maridhiano tatizo lake anasikiliza washauri wanaomchanganya.

Hiki kikao cha ikulu ni maigizo matupu.
 
Inaonekana atakuna na CDM peke yao kwa kuitikia ombi lao. Akifanya hivyo itakuwa heri.

Wakina Shibuda waende kivyao na CDM kivyao. ACT kwa vile wamo serikalini wao wanaweza kukutana nae wakati wowote watakaotaka.

Amandla...
 
Ni protocol, kwa uzoefu wa kiutawala huwa kuna agenda ya mengineyo. Muhimu Chadema ipeleke negiotiators wenye uwezo na sio kupeleka wakina John Mrema ambao mdomo mzito hata kusema neno peoples power ni shida.

My fav list.
Freeman mbowe
Jj Mnyika
Mwalimu
Somebody Ahmed yule mzenji
Catherine Ruge
Devotha Minja
Dr Marco's Albanie
 
Umeshataja wadhifa wake halafu unatuuliza anapokea agenda kama nani??
 
nakubali huyu mama ni Rais kwa mujibu wa Katiba tu. ila akili zake kama ndo hizi bado naamini hafai isipokuwa tu kama atani-prove wrong with time.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom