Kawaida atuma Salamu kwa Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941
KOMREDI KAWAIDA, ATUMA SALAMU KWA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI, ASISITIZA KUMLINDA RAIS SAMIA NI JUKUMU LA VIJANA

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Ndg. Mohammed Ali KAWAIDA (MCC) ametuma salamu kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini na kumtaka kuwachukulia hatua wale wote wanaombagaza na kumtusi Kiongozi Mkuu wa Nchi.

Ndg. Kawaida, ametuma salamu hizo katika Mkutano wa Hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Daniel Chongolo uliofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha tarehe 22 Julai, 2023.

"Vijana wa Chama cha Mapinduzi, kama kuvumilia tumeshavumilia sana kama kuchoka tayari tumeshachoka" amesema Ndg. Kawaida.

Katika muendelezo wa hutuba yake Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Ndg. Kawaida, ameonesha masikitiko yake makubwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kwa kushindwa kuwachukulia hatua wale wote wanaovunja kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa.

"Tunamtaka Msajili wa Vyama vya Siasa, tumechoka na Matusi anayotukanwa Kiongozi wetu, awachukulie hatua wale wote wanaombagaza na kumtusi Kiongozi wetu" amesema Ndg. Kawaida.

Aidha Ndg. Kawaida, amesisitiza ya kwamba Vijana wa Chama cha Mapinduzi kwa namna yoyote ile tutamlinda Mwenyekiti wetu wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwani hili ni jukumu letu Vijana.

Mwisho Ndg. Kawaida, ametuma salamu kwa Vijana wengine nakusema huu moto hata kwa fire hauzimiki, huu moto wa Arusha ni wa mfano tunawapa salamu tukutane mikoa mengine.

Imetolewa Na:
Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa.

#MtumishiWenu
#ChongoloKazini
#KulindaNaKujengaUjamaa
#CCMImetimiaKaziIendelee
#SisiNaMamaMleziWaWana

F1pNPv_WYAU7m_A.jpg
F1pNPv6XgAQF98w.jpg
 
Back
Top Bottom