Hongera Msajili wa Vyama vya Siasa kwa kufuta Vikundi vya Ulinzi (mgambo) kwenye vyama!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,977
141,988
Palikuwepo na Vikundi kama Green guards, Red brigade, Blue brigade nk nk kwenye vyama vya Siasa hususan CCM, Chadema, CUF na Nccr Mageuzi lakini Msajili wa Vyama akavipiga Marufuku

Baada ya kufuatilia kwa makini kinachoendelea Gaza niseme wazi Msajili wa Vyama vya Siasa alitumia busara na Hekima ya hali ya juu kupiga Marufuku mgambo kwenye vyama vya Siasa

Mungu ni mwema Wakati wote

===
Mwaka 2015 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu alipiga marufuku vikundi hivyo vya vyama vya siasa ambavyo vina muonekano na muundo wa vyombo vya usalama, kwani ni kinyume cha katiba na sheria ya nchi. Alivitaka vyama hivyo kuhakikisha vinafuata muongozo uliotolewa na Ofisi ya Msajili wa vyama hivyo na kama vikienda kinyume jeshi litapambana navyo.

Alivitaja vikundi hivyo na vyama vyao kwenye mabano kuwa ni Green Guard (CCM), Red Brigade (Chadema) na Blue Guard (CUF), ambavyo hutumiwa na vyama vya siasa hususan katika mikutano yao.

IGP Mangu aliyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Polisi uliokuwa ukijadili namna ya kuondoa vikundi hivyo pamoja na namna ya kuboresha shughuli za uendeshwaji wa vikundi hivyo. Alisema vikundi hivyo vipo kinyume cha sheria na kwamba kuendelea kuvimiliki kwa kisingizio chochote ni uvunjifu wa Katiba ya nchi na sheria ya vyama siasa, jambo ambalo polisi haliwezi kulivumilia.
 
Awakataze wote Sasa waache kushona magwanda mfano wa nguo za majeshi ili kutofautisha siasa , na mambo ya kijeshi na kuyapa heshima majeshi yetu kuanzia mgambo hadi JWTZ. Natambua Jeshi walishatoka tamko kuhusu wanaovaa Mavazi yanayofanana na ya kwao Sasa naamini Mkuu wa Jeshi la mgambo Tanzania( kama yupo) ni muda wake kuanza msako mkali kwa vyama vya siasa vinavyovaa Mavazi ama ya rangi zake au mishono inayofanana na mishono yajeshi la akiba la mgambo na kushindwa kutofautisha ni yupo askari wa mgambo au ni yupo mwanasiasa ambaye hajawahi hata kurukaruka kichura ,miguu yote ya kushoto naye anavaa Mavazi ya mgambo na kujiita eti KAMANDA.
 
Palikuwepo na Vikundi kama Green guards, Red brigade, Blue brigade nk nk kwenye vyama vya Siasa hususan CCM, Chadema, CUF na Nccr Mageuzi lakini Msajili wa Vyama akavipiga Marufuku

Baada ya kufuatilia kwa makini kinachoendelea Gaza niseme wazi Msajili wa Vyama vya Siasa alitumia busara na Hekima ya hali ya juu kupiga Marufuku mgambo kwenye vyama vya Siasa

Mungu ni mwema Wakati wote
CCM watavibadilisha jina Sasa hivi, take it from me
 
Awakataze wote Sasa waache kushona magwanda mfano wa nguo za majeshi ili kutofautisha siasa , na mambo ya kijeshi na kuyapa heshima majeshi yetu kuanzia mgambo hadi JWTZ. Natambua Jeshi walishatoka tamko kuhusu wanaovaa Mavazi yanayofanana na ya kwao Sasa naamini Mkuu wa Jeshi la mgambo Tanzania( kama yupo) ni muda wake kuanza msako mkali kwa vyama vya siasa vinavyovaa Mavazi ama ya rangi zake au mishono inayofanana na mishono yajeshi la akiba la mgambo na kushindwa kutofautisha ni yupo askari wa mgambo au ni yupo mwanasiasa ambaye hajawahi hata kurukaruka kichura ,miguu yote ya kushoto naye anavaa Mavazi ya mgambo na kujiita eti KAMANDA.
Umeandika matope
 
Green Guards si mgambo wala jeshi...

Kazi zetu:-

-Kukaribisha wageni na kuwaonesha sehemu za kukaa.

-Kuonesha wageni "parking" za magari.

-Kusambaza maji na vinywaji laini

-Hamasa mikutanoni

Msajili AMETUONEA
 
Pia kuwa machawa na wengi wenu ni chakula Cha wakubwa
 
Back
Top Bottom