DOKEZO Matangazo na barua za vitisho zashamiri kwa wataokaidi kuhudhuria Sherehe za Mei Mosi kitaifa Morogoro. Sheria ikoje?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

TRAT

Member
Nov 29, 2022
41
117
Wapo watumishi wasioona mafanikio ya kutatuliwa kero zao za kiutumishi siku ya Mei Mosi, wapo watumishi wasio wanachama licha ya kukatwa mishahara yao ili kulipia michango ya vyama vya wafanyakazi, wapo watumishi wanao amini michango yao inaliwa tu na viongozi wa vyama hivi kwa kujilipa mishahara mikubwa na posho nyingi.

Wanaamini wanaostahili kuandamana ni viongozi wa vyama na viongozi wakubwa wa serikali. Kumekuwa na tabia ya waajiri kuwalazimisha watumishi kuhudhuria sherehe hizi hasa watumishi waliopo katika eneo ambalo sherehe hizi zinafanyika kitaifa.

Humu ndani kuna wabobezi wa sheria za kazi, watusaidie je, usipohudhuria ni kosa kisheria na mwajiri anaweza kukuchukulia hatua?
 
Hamna ulazima wowote.....acheni kutumia kama tawi la chama Cha kisiasa!
Watumishi wengi wa uma... Anyway ngoja nkae kimya
 
Kuwaambia walimu na t shirt zao lazima wahudhurie ni kama kumsukuma mlevi haihitaji nguvu nyingi.
Labda walimu wakuu na maafisa elimu kata maana wanaweza kunyang'anywa madaraka ila kwa sisi wengine hatuna cha kupoteza hivo kulazimisha hakutatufanya tuende,,,Ila namna bora ya kushawishi watumishi wengi kihudhuria ni kutengeneza tu mazingira yawe rafiki kwa wao kwenda.
 
Wewe kama umeajiriwa ni kosa la jinai kumtunishia msuli mwajiri wako , follow order , amri ya kijeshi haijadiliwi ni kutekeleza kwendeni MEI mosi
 
Wapo watumishi wasioona mafanikio ya kutatuliwa kero zao za kiutumishi siku ya Mei Mosi, wapo watumishi wasio wanachama licha ya kukatwa mishahara yao ili kulipia michango ya vyama vya wafanyakazi, wapo watumishi wanao amini michango yao inaliwa tu na viongozi wa vyama hivi kwa kujilipa mishahara mikubwa na posho nyingi. Wanaamini wanaostahili kuandamana ni viongozi wa vyama na viongozi wakubwa wa serikali. Kumekuwa na tabia ya waajiri kuwalazimisha watumishi kuhudhuria sherehe hizi hasa watumishi waliopo katika eneo ambalo sherehe hizi zinafanyika kitaifa. Humu ndani Kuna wabobezi wa sheria za kazi, watusaidie je, usipohudhuria ni kosa kisheria na mwajiri anaweza kukuchukulia hatua?
huu uzushi mwandikie mamako. shenzy type
 
Labda walimu wakuu na maafisa elimu kata maana wanaweza kunyang'anywa madaraka ila kwa sisi wengine hatuna cha kupoteza hivo kulazimisha hakutatufanya tuende,,,Ila namna bora ya kushawishi watumishi wengi kihudhuria ni kutengeneza tu mazingira yawe rafiki kwa wao kwenda.
Uko sahihi, mtumishi hawezi kufikuzwa kazi kwa kutohudhuria sherehe hizi. Labda waamue kumkomoa tu kwa kumhamisha mazingira magumu hasa Walimu.
 
Vyama vingi havina muelekeo kazi kukandamiza ebu assume vyama kuna watu wanachangia 50k kila mwezi ila siku ya Mei mosi wanapewa tu T-shirt then wakapigwe na jua pale hamna posho wala nn ni ufala wa kiaina.

Kuna vyama eti vinatetea kesi zinazowakabili wafanyakzi ila ukijichanganya ukadodge bila kwenda kazini siku kadhaa zikapita ukafkuzwa kazi wanakuja kukuambia hilo sio jukumu lao kwa vile umevunja sheri za utumishi wa umma ..Ni sawa nyie hizo kesi mnazopambania mpaka mkate watu pesa kila ya mwezi ni zip ? Maana eti wanatetea overtime za wafanyakazi sasa wanatetea nin wakati mtu ni haki yake?




Ukwei mchungu wanaonufaika ni management na dili zote za hivi vyama ni utapeli tupu kuwahadaa na kuwatisha watu eti sijui panaweza kutokea kesi za kiutumishi...Kesi zipi? wakati mtu anatakiwa kufauta taratibu za utumishi yaani mtu achangie mwaka mzima then Mei mosi anapewa T-shirt tu hao viongozi wakuu wapo pembeni hawapo kweny maandamano kama sio wizi n nn?


Hakuna HR wanaodili na maslahi pamoja na matakwa ya wafanyakazi hivi vyama vinakujaje wanalipana mara mbili maana wengine ni wafanyakazi kabisa ila wanapiga pesa kuanzisha hivi vyama.
 
Back
Top Bottom