Mei Mosi Mwanza Itafanyika Wilaya ya Sengerema

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

MHE. HAMIS TABASAM AWAKARIBISHA WANAMWANZA KWENYE SHEREHE ZA MEI MOSI ZITAKAZOFANYIKA SENGEREMA

Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mkoa wa Mwanza, Mhe. Hamis Tabasam amewakaribisha wananchi wa Sengerema na Mwanza kwa ujumla kushiriki maadhimisho ya sherehe za Mei Mosi zitakazofanyika Sengerema.

Mbunge wa Jimbo la Sengerema Hamis Tabasam anawakaribisha wakazi wa wilaya ya Sengerema pamoja na wananchi wa mkoa wa Mwanza kuhudhuria maadhimisho ya sherehe za wafanyakazi Mei mosi mwaka huu, zinatarajiwa kufanyika katika viwanja vya mnadani wilayani Sengerema

Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mhe. Hamis Tabasam ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Mwanza unaongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Adam Malima kwa kupeleka Maadhimisho ya sherehe za wafanyakazi mwaka huu (MEI MOS) kimkoa kufanyika wilayani Sengerema.

Kauli Mbiu ya Mei Mosi 2023: "Mishahara Bora na Ajira za Staha ni Nguzo kwa Maendeleo ya Wafanyakazi" Wakati ni Sasa!

Mwaka 2023 Maadhimisho ya Mei Mosi Kitaifa yatafanyika Mkoa wa Morogoro katika Uwanja wa Jamhuri na Mgeni Rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
 

Attachments

  • Fu8tMH-XoAAsBAC.jpg
    Fu8tMH-XoAAsBAC.jpg
    132.9 KB · Views: 4
  • Fu8tNHOWYAE1vPv.jpg
    Fu8tNHOWYAE1vPv.jpg
    176.7 KB · Views: 4
  • Fu8tOlPXsAAaWD9.jpg
    Fu8tOlPXsAAaWD9.jpg
    134 KB · Views: 4
  • Fu8tPtbXgAEPeet.jpg
    Fu8tPtbXgAEPeet.jpg
    122.3 KB · Views: 3
Kila siki watumishi wanalilia mishahara hawawezi kuja na kauli mbiu ata ya ufumbuzi wa ki teknolojia katika utendaji kazi ni chachu ya mafanikio
 
Watumishi wa serikali washakuwa kama watoto.Wanakusanywa na kuahidiwa pipi kila mwaka
 
Back
Top Bottom