Wafanyabiashara Soko la Sinza walalamika kufanyiwa ubabe wa kulazimishwa kusaini mikataba viongozi wa Halmashauri ya Ubungo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Wafanyabiashara wa Soko la Sinza Makaburini wamedai kuna uonevu mkubwa wanafanyiwa na uongozi wa Halmashari ya Ubungo kwa kuwalazimisha kusaini mkataba ambayo hawajairidhia.

Baadhi ya Wafanyabiashara wamesema viongozi wa Halmashauri hiyo wakiongozana na Askari Polisi, Mgambo na Mwanasheria anayefahamika kwa jina la Kisa wamefanya zoezi hilo jana Februari 16 na leo Februari 17, 2023.

Wanachofanya ni kufika kwenye vibanda vya wafanyabiashara na kuwataka wasaini mikataba kwa lazima bila kujali anayesaini amesoma au hajasoma, pia bila kujali ni mhusika wa biashara ua la, ilimradi wamemkuta sehemu husika akiwa anasimamia wao wanamlazimisha.

Wafanyabishara ambao waliweka ugumu walikamatwa na kuweka chini ya ulinzi, hali hiyo ikawafanya wengine pia walazimike kusaini ili kujiokoa.

Moja ya jambo ambalo Wafanyabiashara wanapingana nalo ni kuwa hawajafanya mazungumzo yoyote na mamlaka hiyo, hivyo kinachoendelea wakati huu ni ubabe na kibaya zaidi wamepandishiwa kodi, awali walikuwa wakilipa Tsh. 200, kisha wakaambiwa walipe Tsh. 25,000 na Tsh. 50,000

Lakini katika mkataba hiyo mipya kod imepanda na kugawanya katika viwango vya Tsh. 25,000, 50,000, 75,000 na 150,000.

==========


Akielezea kinachoendelea, Yusuf Nyahori ambaye ni Mwenyekiti wa Vibanda wa Soko la Sinza, amesema:

“Kinachofanyika ni aina fulani ya uonevu, hawa watu (Halmashauri) baada ya kutusumbua sana wakitupa masharti kadhaa, Novemba 1, 2022 walikuja na kuweka tangaza Sokoni wakitutaka sisi tuanze kulipa Elfu 25 kwa mabanda ya ndani na elfu 50 kwa mabanda ya mbele.

“Kabla ya hapo tuliwahi kuwafikisha Mahakamani kupinga walichokuwa wanataka kukifanya, suala hilo lilifika hadi kwa Mkuu wa Wilaya wa wakati huo, lakini baadaye wakatubembeleza tufute kesi.

“Tulifuta tukiamini kuwa tutakaa chini tuzungumze, tunajua kweli ardhi ni ya Serikali na wao ni wasimamizi lakini wanachokifanya ni ubabe.

“Aliyekuwa akiongoza msafara huo ni Mwanasheria wao anaitwa Kisa pamoja na Meneja Masoko anaitwa Geofrey.

“Walikuwa wanafika kwenye banda yeyote wanayemkuta wanamwambia asaini mkataba hata kama siyo mhusika, kibaya zaidi hakuna muda wa kuusoma huo mkataba, unaambiwa Saini kama hautaki ondoka kwenye biashara kisha wao wanaleta mtu mwingine.

“Kibaya zaidi walichokuwa wakifanya wakikuta kuna msimamizi wanamwamia aandike jina la mmiliki wa kibanda kama linavyosomeka kwenye leseni, kisha shahidi anakuwa huyohuyo msimamizi.

“Malalamiko yetu sisi siyo kulipa bali hakuna utaratibu na bei imekuja ya juu kuliko uhalisia wa biashara, na wao wenyewe ndio wanaoanga bei inayotaka.”

===========

MWANASHERIA WA HALMASHAURI YA UBUNGO

Kissah Mbilla, ambaye ni Mwanasheria wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo amesema: “Hili zoezi tumelifanya kihalali kabisa hakuna uonevu wala matumizi ya ubabe, hawa tulishakaa nao vikao zaidi ya 10 na taarifa zote zipo wazi.

“Bei wanayolalamikia wameshapewa taarifa tangu Mwaka 2009/10.

“Malipo ya kodi ya wafanyabiashara wengi siyo nzuri, kila tunapotaka kufanya zoezi hili tukiwapa taarifa wanaenda Mahakamani, ndio maana tukaamua kufanya kwa kuwashtukiza bila kuwashirikisha hata viongozi wao wa soko kwa kuwa ukiwaambia wanakimbilia Mahakamani.

“Asilimia kubwa wanaolalamika ni wale ambao wameshika vibanda kisha wamepangisha watu wengine kwa bei kubwa mfano Tsh. 300,000 hadi 400,000 lakini hao ambao wana leseni hawaendi kulipa, tukitazama kwenye mahesabu wana madeni mengi.

“Uongozi wa Manispaa tukaamua kuacha ubabaishaji, kinachofanyika sasa hivi ni uamuzi ambao tumeupitisha kwenye vikao.

“Mwanzoni kabla ya zoezi hili tuliwashirikisha hao wafanyabiashara lakini ushirikiano haukuwa mzuri.

“Zoezi hili ni endelevu kwenye masoko yote ya Manispaa ya Ubungo, hakuna anayelazimishwa, tunawapa mikatana na kuwapa muda kadhaa wa kusoma kisha wakiridhia wasaini.”
 
Ugumu uko wapi? Kama unaona kodinya manispaa sio rafiki kwako c unaachia eneo wafanye wengine kwa manufaa ya taifa lako.
 
Back
Top Bottom