Moto Wateteketeza Bidhaa za Wafanyabiashara Karibu na Soko Kuu Katavi

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Moto mkubwa umeibuka katika maeneo ya karibu na soko kuu lililoko manispaa ya Mpanda mkoani Katavi na kuteketeza mali zinazotajwa kuwa na thamani ya Shilingi milioni tano ambapo jeshi la zimamoto na uokoaji limefanikiwa kuuzima moto huo.

Shabani Hassani ni shuhuda wa kwanza kuuona moto huo na kuhamasisha wenzake kuanza kufanya uokoaji huku Thomas Mazingu ni mfanyabiashara katika soko hilo ambapo anasema bidhaa zenye thamani ya zaidi ya milioni tano.

Kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji Katavi Geofrey Mwambungu amesema moto umeteketeza bidhaa zenye thamani ya zaidi ya milioni tano.

Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf amesisitiza wafanyabiashara kukata bima kwa ajili ya bidhaa zao ili waweze kufanyabiashara kisssa zaidi.

Chanzo cha kutokea kwa tukio hilo la moto hakijajulikana.

View: https://www.instagram.com/reel/CyvbRu6NWLg/?igshid=MzRlODBiNWFlZA==
 
Back
Top Bottom