CCTV Camera zafungwa Soko la Mchikichini Karume (Dar) kubaini wanaochoma moto masoko

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Kufuatia mfululizo wa matukio ya moto ambayo yaliyokuwa yakitokea kwa nyakati tofauti kwenye soko la Mchikichini eneo la Karume, Dar es Salaam kwa sasa soko hilo linadaiwa kuja na mikakati mipya kwa lengo la kuthibiti matukio hayo yasitokee na hata yakitokea kusiwepo na athari kubwa zaidi kama ambayo imewahi kutokea Mwaka 2022 ambapo ilidaiwa katika makisio Wafanyabiashara walipata hasara ya Tsh. Bilioni 7.

Imeelezwa kuwa mkakati huo unahusisha mifumo ya ulinzi na usalama ambapo kwa sasa imeelezwa wameweka Miundombinu ambayo inahusisha mifumo ya Teknolojia ya kisasa.
photo_2023-10-07_11-22-08.jpg

Sehemu ya muonekano wa CCTV Camera

Akizungumzia miundombinu hiyo Mwenyekiti wa Soko hilo, Geoffrey Milonge amesema kwa sasa wamefunga vifaa vya kisasa ikiwemo CCTV Camera ambayo inawawezesha kuona kinachoendelea hususani kwenye kona zote zinazozunguka soko hilo.

Amebainisha wazi kuwa kuna mtambo maalumu ambao ikitokea janga la moto wanabofya kwa uharaka taarifa zinafikia Jeshi la Zimamoto ili kusaidia kufika sehemu ya tukio kwa uharaka kabla moto haujaleta athari zaidi.

"Kwa sasa tokea tukumbwe na moto Mwaka jana (2022), tumeamua kuja na mikakati ambayo itasaidia kumaliza haya majanga au yakitokea kusiwepo na athari zaidi.

“Ukiangalia kwa sasa tumefunga CCTV Camera kila kona tunaona kinachoendelea kuna mtaalamu anakaa kazi yake ni kuangalia kinachoendelea kwenye soko letu hata kama kuna mtu ana nia mbaya ni rahisi kumuona, lakini hatujaishia hapo tumeweka mtambo ambao kwenye ofisi zetu nje ambapo ukibonyeza tu Jeshi la Zimamoto wanafika kuzima moto kabla haujatuletea madhara kwa kiwango kikubwa," anasema Mwenyekiti wa Soko hilo.

Pia ameweka bayana tayari wataanza kuzungusha uzio na kuweka milango kwenye maeneo ambayo ni karibu na makazi ya Wananchi ili kuzuia mwingiliano ambao unaweza kuwa na madhara.

"Kama tunavyojua soko letu kuna maeneo limepakana na makazi ya watu, sasa tunajitahidi ili kuzungusha uzio na kuweka milango maalumu ili kuruhusu mwingiliano ambao kwetu tunaona unaweza kutuletea athari maana mtu anaweza kutoka kwenye makazi akaingia sokoni kinyemera kwa sababu ya ukaribu uliopo sasa tumeanza kulishughulikia hilo," alisema Mwenyekiti wa Soko hilo.

Aidha, Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara wenyewe Ulemavu Dar es salaam, Juma Hamis Malecha amepengeza jitihada ambazo zimekuwa zikifanyika ikiwemo kuweka walinzi wa kutosha kutoka kampuni ya ulinzi ili ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuepusha matukio mbalimbali ikiwemo janga moto ambalo amesema kuwa limekuwa likipelekea kilio kwa wengi.

Ameongeza athari za moto zimekuwa zikigusa moja kwa moja watu wenye ulemavu ambapo amesema "Yanapotokea matukio ya moto kama vile Mwaka 2022 sisi Wafanyabiashara wenye ulemavu tunaathirika kwa kiwango kikubwa, wapo wenzetu hawakurudi tena hapa sokoni maana akija kupata mtaji upya kujipanga na kurejea ni lini wapo waliokata tamaa kuna waliokuwa wanashona nguo wengine viatu lakini vifaa vyao viliathirika."
photo_2023-10-07_11-22-04.jpg

Mtambo unaotumika kutoa taarifa Zimamoto inapotokea kuna changamoto ya moto.

Kufuatia mkakati wa kuthibiti matukio hayo Julai 6, 2023, Mwenyekiti amedai mtu mmoja ambaye ni kijana wa kiume alikamatwa na walinzi wa soko hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi majira ya saa saba usiku akiwa na vitu ambayo inadaiwa alida alitaka kuvitumia kuchoma moto soko hilo.

Katika maelezo ya Mwenyekiti inadaiwa kijana huyo alikili aliagizwa na Mfanyabiashara mmoja anayefanya biashara kwenye soko hilo ikidaiwa alimuahidi Tsh. laki nane mara baada ya kukamilisha mpango huo huku sababu ya kumuelekeza kufanya hivyo ikidaiwa alikuwa na mkopo beki.

Ameeleza mipaka yao ilishia baada ya kumkabidhi kwenye Jeshi la Polisi, ambapo amedai baada ya uchunguzi wa Jeshi hilo kukamilika watuhumiwa wawili walifunguliwa kesi kwenye Mahakama ya Wilaya Ilala iliyopo Kinyerezi Jijini Dar es salaam.

Kesi tayari imeanza kusikilizwa na inatarajiwa kuendelea Oktoba 10, 2023 huku watuhumiwa wote wawili wakiwa nje kwa dhamana.

Itakumbukuwa Soko la Mchikichini Karume kwa sasa lina Wafanyabiashara zaidi ya 1,000 ambao wamekuwa wakijihusisha na mauzo ya bidhaa mbalimbali hasa bidhaa za mitumba ikiwemo nguo na viatu vya mitumba.

Biashara katika eneo hilo inadaiwa kudumu kwa miaka zaidi ya 20 huku watu mbalimbali kutoka mikoa tofauti pamoja na nje ya Tanzania wamekuwa wakifika eneo hilo kuchukua bidhaa.

Hata hivyo, matukio ya moto kwa nyakati tofauti yamekuwa yakisababisha sintofahamu licha ya hatua mbalimbali kuchuliwa ikiwemo kuundwa kwa Tume maalumu kwa ajili ya uchunguzi.
 
Wakiamua mambo yao hizo Camera si kitu , Eneo aliloshambuliwa Tundu Lissu kulifungwa Camera kama hizo pia
 
Baada ya Tundu Lissu kumiminiwa risasi Dodoma kwenye majengo ya viongozi , CCTV CAMERA zilinyofolewa
 
Back
Top Bottom