Masikini my ex, kweli malipo ni hapahapa duniani

Masikini my ex, kweli malipo ni hapahapa duniani

mademu wa vyuo vya afya huwezi kaa naye in a relationship mkafika popote. Wana stress nyingi zinazowafanya wawe wepesi kuona kama wanazinguliwa pale anapoona humjali vile ye anataka. Labda awe amemaliza chuo. Ni rahisi sana kupitiwa na mshikaji atakayemjali kidogo akiwa na stress zake. In short ni padua kichwa. This is my 5 years experience with female medical students
yaani huu ndo ushauri nilitaka kumpa jamaa, kama ulikuwa kwenye akili yangu,ongezea na hii.. Wanahisi maisha wanayo tayari
 
Kabla haujamkaribisha tena ndani ya moyo wako....mchukulie kawaida na umchunguze kama kweli anakupenda ama analipenda gari la kuazima......
 
Mtu kakuacha kaenda kwa mwingine. Akapigika anarudi kwako? Aisee kitu kama hiki ni mwiko. Si mke huyo. Sasa kama ameweza kukuacha hujamweka ndani je ukioa. Ndoa si lelemama.
 
Kama namuona hivi huyo bint..sasa hivi anawaza hivi "akinikubalia poket money kwangu si tatizo, alafu kila siku ntakuwa napelekwa chuo na bonge la mgarii, watanikomajee mashosti zanguuuu!!!!"
 
Midemu mingine buwana yanaleta za kuleta alafu yanaumbuka kuanza kurudia matapishi,kikubwa mchape nao wakatai bado yunaendelea kum-screen.
 
Sikuizi vijana wa kiume wanatumika nao.. Mtu anafuata magari mazuri..yakiisha anarudi kwako.. Muhimbili nimepita hapo.. Watoto wa hapo si wote hawajui mapenzi.. Kupenda.. Alafu wana admit sana..
 
Hahaha, wakati ukimshusha hukumuachia spare tyre ya range jamani? Mchoyo wewe!
 
Nilimpenda sana huyu binti ila siku isiyo na jina alinimwaga tena kwa mbwembwe. Niliumia sana! almanusura nichanganyikiwe!

Sasa jana mchana nikasema nikimbie Mlimani City kwenda kununua kitu fulani, nikamuazima mwanangu gari lake (Range rover evoque) nikamuachia la kwangu (Hyundai Coupe Sports car).

Sasa wakati napark pale Mlimani nikasikia naitwa, kugeuka nakutana uso kwa uso na huyo bibie!

At first alikua kama ametahayari alivoona nashuka kwenye ile ndinga! Nikasalimiana nae vizuri tu, tukaongozana kuingia Mlimani ndani!

Akaanza kuning'ang'ania, ooh Amicus I missed you, leo sikuachi nakwambia, nikazunguka nae mule ndani, nikawa najiuliza mbona yeye hanunui, alifwata nini M/city? halafu alikua 'restless'. Nikajua kapanic akidhani ule mkoko ni wangu, alizoea kuniona na Hyundai yangu.

Mara ooh naomba tuongozane! wakati hajui naelekea wapi!

Sikuwa mkaidi, nikatoka nae, tukazama kwenye ndinga nikampeleka lunch! akawa analisifia sana gari! wakati tunasubiri msosi akaanza kunisimulia yaliyomsibu huku anabubujikwa na machozi! hadi watu wakawa wanatushangaa! na yeye ameachika almost the same way kama alivyoniacha!

Ananisihi turudiane, sasa naogopa asije akawa ameweweseka na ile range, tukarudiana akaja kuleta wenge tena akijua kwamba ule usafiri si wangu! Uongo haufai, kiukweli me bado nampenda.

Ni kama alikua anatamani kuniuliza kuhusu lile gari ila akawa anashindwa!

Jamani hebu nishaurini mwenzenu, nahisi bado nampenda coz tangu tuachane imepita miezi 6 tu ingawa nilikua nimeshaanza kumsahau. Halafu amezidi kuwa mzuri, amekatika vibaya sana!

Ananisumbua sana kwenye simu wajameni!

Yeye yupo Chuo pale Muhimbili anasomea Udaktari.

Nina uhakika hayumo humu JF coz nilimuuliza jana akasema yeye sio big fan wa mitandao ya kijamii kwasababu mara nyingi anapiga msuli, kwa kifupi shule yake ni ngumu sana.

Jamani nishaurini, kwa wale mtakao-comment naomba muwe serious...nataka kesho asubuhi nimpe jibu.
Fanya kwanza haya
1. Mtafute ukiwa na kihyundai chako, halafu mwambie ile vogue uliazama.. halafu sikiliza matokeo
2. Muulize sababu ilimfanya akumwage, na anadhani ni nini kimebadirika hadi atake kukurudia

By the way....We unadhani yeye ana kitu gani tofauti na mwanzo..?? Hivi huko alikopigwa kibuti, kama mambo yangeendelea kuwa mazuri angekung'ang'ania..?? Huu ubaba huruma huu, sometimes siyoo kabisaaaa

 
Hivi vistory kama vya form two vile.ww una mtoto mkubwa hadi anamiliki aina ya gari ambayo haijawahi kumilikiwa na binadamu mwingine zaidi yako eti evoque bado huna mwenza.kwa umri uyo dada hadi leo ndo eti anasoma chuo cjui ni matured entry ipi lipita kujiunga na chuo.Pia gari hizo `evoque' siyo za kutisha cku izi kama unavyotaka kutuaminisha

Bei yake si lolote utujie na mbwembwe au ww unatokea ile kabila ya kanda ya ziwa?!Kwa kauli yako tu muachane na mtu muda huo mrefu simply tu unakutana nae jiji la mlimani nanakung`anga`nie eti kisa evoque na wewe unatuletea visa vya shigongo kutushirikisha ,kama ingekuwa kweli hujui huyo hafai?
Hapo kwenye body... MWANANGU ni RAFIKI, na si mtoto kama ulivyoitafsiri wewe

 
Fanya kwanza haya
1. Mtafute ukiwa na kihyundai chako, halafu mwambie ile vogue uliazama.. halafu sikiliza matokeo
2. Muulize sababu ilimfanya akumwage, na anadhani ni nini kimebadirika hadi atake kukurudia

By the way....We unadhani yeye ana kitu gani tofauti na mwanzo..?? Hivi huko alikopigwa kibuti, kama mambo yangeendelea kuwa mazuri angekung'ang'ania..?? Huu ubaba huruma huu, sometimes siyoo kabisaaaa


Nimekuelewa mkuu

Nitaufanyia kazi ushauri wako
 
Hapo kwenye body... MWANANGU ni RAFIKI, na si mtoto kama ulivyoitafsiri wewe


Nashukuru kwa kumuelewesha mkuu manake hizi fake ID's ndio tatizo humu

Mnaweza mkajikuta hamuelewani kumbe unajibizana na lizee
 
What a desperate woman...enewei rudiana nae ila jiandae kubwagwa upya baada ya kurudisha hyo range
 
What a desperate woman...enewei rudiana nae ila jiandae kubwagwa upya baada ya kurudisha hyo range

Naona wengi mmenishauri niachane nae

Akili kumkichwa, akili ya kuambiwa changanya na ya kwako

Let me 'act' like a man...

Ila hata mimi nimeanza kuwa na hisia kwamba hanifai huyu
 
Naona wengi mmenishauri niachane nae

Akili kumkichwa, akili ya kuambiwa changanya na ya kwako

Let me 'act' like a man...

Ila hata mimi nimeanza kuwa na hisia kwamba hanifai huyu
Na hakufai kabisa huyoo... Yaani yeye badala ya kuchanganyikiwa na wewe, anachanganyikiwa na gari... Sasa kwa jinsi hawa madizaina wa magari walivyo bize na kuyatoa mapya kila mwaka, lazime atakumwaga tena, labda kama utawazuia madizaina waache mambo yao

 
mademu wababaikaji wa shughuli gani wewe,zinduka,achana na msomi mshamba anayebabaikia vitu,angalia dem understanding
 
Back
Top Bottom