Masikini my ex, kweli malipo ni hapahapa duniani

Masikini my ex, kweli malipo ni hapahapa duniani

Ndo mana unapigwa na chini....kumbe we mwenyewe unapenda makubwa...subiri yakukute basi....kwa nini hui kama muanzilishi wa face book? kijana tajiri lakini yuko down to the earth!
 
mkubalie alafu wait for another round i think its will be more better
 
Nilimpenda sana huyu binti ila siku isiyo na jina alinimwaga tena kwa mbwembwe. Niliumia sana! almanusura nichanganyikiwe!

Sasa jana mchana nikasema nikimbie Mlimani City kwenda kununua kitu fulani, nikamuazima mwanangu gari lake (Range rover evoque) nikamuachia la kwangu (Hyundai Coupe Sports car).

Sasa wakati napark pale Mlimani nikasikia naitwa, kugeuka nakutana uso kwa uso na huyo bibie!

At first alikua kama ametahayari alivoona nashuka kwenye ile ndinga! Nikasalimiana nae vizuri tu, tukaongozana kuingia Mlimani ndani!

Akaanza kuning'ang'ania, ooh Amicus I missed you, leo sikuachi nakwambia, nikazunguka nae mule ndani, nikawa najiuliza mbona yeye hanunui, alifwata nini M/city? halafu alikua 'restless'. Nikajua kapanic akidhani ule mkoko ni wangu, alizoea kuniona na Hyundai yangu.

Mara ooh naomba tuongozane! wakati hajui naelekea wapi!

Sikuwa mkaidi, nikatoka nae, tukazama kwenye ndinga nikampeleka lunch! akawa analisifia sana gari! wakati tunasubiri msosi akaanza kunisimulia yaliyomsibu huku anabubujikwa na machozi! hadi watu wakawa wanatushangaa! na yeye ameachika almost the same way kama alivyoniacha!

Ananisihi turudiane, sasa naogopa asije akawa ameweweseka na ile range, tukarudiana akaja kuleta wenge tena akijua kwamba ule usafiri si wangu! Uongo haufai, kiukweli me bado nampenda.

Ni kama alikua anatamani kuniuliza kuhusu lile gari ila akawa anashindwa!

Jamani hebu nishaurini mwenzenu, nahisi bado nampenda coz tangu tuachane imepita miezi 6 tu ingawa nilikua nimeshaanza kumsahau. Halafu amezidi kuwa mzuri, amekatika vibaya sana!

Ananisumbua sana kwenye simu wajameni!

Yeye yupo Chuo pale Muhimbili anasomea Udaktari.

Nina uhakika hayumo humu JF coz nilimuuliza jana akasema yeye sio big fan wa mitandao ya kijamii kwasababu mara nyingi anapiga msuli, kwa kifupi shule yake ni ngumu sana.

Jamani nishaurini, kwa wale mtakao-comment naomba muwe serious...nataka kesho asubuhi nimpe jibu.

kweli nimeamini biashara matangazo…..... so ulikuwa unajinadi kwamba una gari sio…. oke tumekuelewa.
 
Mchepue mara moja urudi njia kuu kama ipo. Kama haipo akili kumkichwa ukinogewa ndo basi tena gari lenywew alilofwata la kuazima..
 
Hawa viumbe wanatutesa sana,yeye kama anahisi umekuwa matawi kisa gari je siku ndo umeishiwa ndo itakuwa?
fikiria kabla ya yote hata kama unampenda piga moyo konde kama ulikuwa umeshaanza kumsahau basi msahau kabisa.maumivu aliyokuachia naye ayasikilizie,akupigae ngumi ya jicho nawe mpige ya sikio akikuuliza unaonaje nawewe muulize unasikiaje? hapo ngoma droo!
 
Mimi nahisi wewe ndiye wa kuonewa huruma. tafakari kijana la sivyo utaliwa kekundu
 
Back
Top Bottom