Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,402
- 1,254
- Thread starter
- #21
---kuna makala nimekutana nayo kwenye gazeti la Mwananchi, maudhui yanafanana fanana na thread hii.... nainukuhu:
SteveD.
Source link: http://mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=6198Posted Date::6/14/2008
Makala: Miss vitogoji ...ukicheza na Nyani utavuna mabua
Na Phillip Nkini
KAMA unazungumzia sekta inayotoa ajira kwa vijana ususani wasichana basi uwezi kuiweka kando mashindano ya Miss Tanzania ambayo tangu kuanzishwa kwake upya yamebadilisha maisha washiriki wengi.
Mashindano haya kwa Tanzania yamejijengea umaarufu siku za hivi karibuni kutokana na watu wengi kuanza kuyafuatilia kutokana na washiriki wake kuanza kutofutwa kuanzia vitogoji.
Mashindano haya yamekuwa na msisimko mkubwa sana kwenye jamii nzima na kila baada ya muda yamekuwa yakibadilisha mwelekeo mara kwa mara na kuongeza msisimko.
Kumeibuka mashindano mengi huku vigezo vikitofautiana kwa mtazamo na vigezo vya awali na mwisho wa mashindano husika.
Mashindano ya Miss Tanzania kama yalivyo mashindano mengine yana vigezo vyake ambavyo hutumika kwa ajili ya usimamizi mzima wa mashindano kwa ujumla.
Moja ya vigezo ambavyo vinatumika ili mrembo aruhusiwe kushiriki mashindano haya ni kwanza asiwe ameolewa, (yaani hana Mume), mwenye umri kuanzia miaka 18 hadi 24 na hasiwe na mtoto.
Nasema haya kwa kuwa nataka nikulete kwenye hoja yangu kuwa uandaaji wa mashindano haya kuanzia huku chini ngazi ya vitongoji ni mbovu na ndio maana mara nyingi tumekuwa hatufanyi vizuri kwenye mashidano kimataifa.
Ni hali ya hatari kwa sasa kama msichana ni mwembamba na mrembo akiwa anakatiza katika mitaa ya jiji la Dar es Salaam kuzongwa na kufuatwa na wimbi la Mawakala wanaoadaa mashindano haya ngazi ya vitongoji.
Mawakala hawa wamekuwa hata wakiacha shughuli zao nyingine na kupanda dala dala moja hadi nyingine huku wakimfuata msichana mmoja ambaye wamemuona anafaa kwa ajili ya shindano lao.
Imetokea mara nyingi kuona kuwa mmoja wa rafiki wa mtu anampigia mwezake ambaye anaanda mashidano haya na kumwambia njoo sehemu fulani uongee na mrembo mmoja ambaye yupo jirani yangu kwenye hoteli fulani nimekaa.
Au wakati mwingine utakuta mrembo ameshiriki vitogoji furani ameshindwa ana rusiwa kushiriki sehemu nyingine bila ya kipingamizi.
Baadhi ya wasichana wanaosoma shule za katikati ya jiji wamekuwa pia ni waathirika wakubwa wa kukimbizwa huku na mara anapokataa kutii amri hii huanza kusumbuliwa kwa maombi ya muda mrefu.
Hoja yangu hapa ni kwamba je vigezo hivyo vinatumika kwa ajili ya maandalizi haya wana juaje kama msichana huyu anakidhi vigezo vinavyotakiwa ili kushiriki ngazi ya Taifa?
Je unapomwangalia msichana unajua kuwa msichana huyu ameolewa au la unajua kama ana miaka zaidi ya 24 au je vyeti huonyeshwa kwa nani na lini kama mtu huyu ni mdogo au mkubwa.
Kwanini kusiwe na misingi dhabiti najua hakuna sehemu yeyote ambayo vyeti vyao vinaonyeshwe ana umri gani au ameolewa au vipi.
Kigezo kikubwa hapa ni kwamba kuna ubovu mkubwa sana kwenye utaratibu wa kuanzia mwanzo wa mashindano haya hadi mwisho kutokana na kutokuwa na mpangilio maalum.
Ni nani anayejua kuwa huyu anayepewa nafasi ya kuwa wakala sehemu moja au nyingine anaweza kupata washiriki wakutosha na wenye vigezo.
Pointi ya msingi inayotumika ni kwamba nani amewahi kuomba nafasi ya kufanya onyesho lake sehemu fulani na akapewa nafasi hiyo kwa kipindi kile.
Mashindano haya hapa nchini yamekuwa hayana faida kubwa baada ya mara nyingi washindi wa nchi hii kushindwa kufurukuta nje ya nchi ambapo wanakuta na na warembo waliopata maandalizi na vigezo vya juu.
Itakuwa kawaida kila mara kuona mshindi wa kwanza ngazi ya Taifa kupatikana jiji Dar es salaam kwa sababu wako karibu na mashindano hayo yanapofanyika kitaifa.
Lini waandaji wataweza kuwa kuna umuhimu wa kufanya mashindano haya kwenye ngazi ya Taifa mikoani ili kutoa semina kabambe na huku nao wajue kuwa kuna haja ya kujipanga na kupata semina ya vigezo husika ili waache kulalamika kila mara kuwa washidi wanatoka Dar es salaam.
Nafikiri ni muda muafaka sasa kabla mawakala hawa hawajapewa nafasi ya kuandaa mashidano katika kitongoji fulani basi wapewe kwanza kazi ya kutafuta wajumbe kabla ya kuanza mchakato huu mzima nikiwa na maana wapate kwanza angalau warembo kumi ambao wataangaliwa vigezo vyao ndio wapewe nafasi ya kuandaa tuone kama kuna hata mmoja atagombania hivi vitongoji.
Kwa sasa imekuwa ni kawaida kwa asilimia kubwa ya kitongoji kukuta kina warembo watatu zikiwa zimebaki siku tano tarehe ya mashindano yake kufanyika na hao wenyewe kuna siku wanakuja wawili na siku nyingine mmoja na wakati mwingine unakuta hata mwandaaji mwenyewe hayupo, je ni kweli kuwa tutapata mrembo mwenye vigezo vya kuwa mrembo wa Miss World.?
Kwa mtindo huu wa ubabaishaji tutaishia kuangalia warembo wakiangaika jukwaani na siku ya mwisho tutabaki tukisema kuwa mrembo wetu amekwenda Ulaya kutalii je msingi tuliweka? wapi alileta cheti kuwa amemaliza kidato cha nne au anauwezo wa kuzungumza kiingereza au tulimfundisha wapi ya kwamba akienda kule nje asizungumze kiingereza kwa kuwa hajua na azumgumze kiswahili na watu watamwelewa.
Mara kwa mara tumekuwa tunafika sehemu ya kulaumu kuhusu mashindano haya bila kuwa na vigezo vya Msingi ni dhahiri kuwa huku nyuma kumeoza na tupatengeneze kwanza ndio tupate nguvu za baadae kuongea.
Ni muda sasa wa kutafuta vyeti vya kuzaliwa vya washiriki kufundishana mchakato mzima wa kuwapata hawa warembo na kuweka kigezo cha elimu ili kulisaidia Taifa letu na warembo wenyewe ili waache kupoteza muda kwa ajili ya shilingi laki mbili za mshindi.
Tuwaheshimu warembo wetu kwa kuwa ni watu wakubwa na wenye hadhi yao na wanahitaji heshima kubwa si kama inavyofanyika sasa tujaribu kufungua macho yetu na kuangalia kwanza tatizo liko wapi ili tuweze kwenda mbele na si kurudia yale yale kila siku.
SteveD.