Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,402
- 1,261
Tanzania yetu kwa kweli imeneemeka na kutunukiwa, maana warembo ni kede wa kede, kanda zote na mikoa yote ya nchi kuna warembo wa kumwaga. Hadi jirani zetu hutubu juu ya neema hii. Kwa nyakati mbali mbali nimebahatika kukutana na watu, tena akina dada toka Zambia na Kenya wote wakisifia Tanzania kwa kuwa na akina dada wengi walio warembo kuliko huko makwao. Ma'braza' ndiyo kabisaa usiseme.... wanakodolea da'zetu utafikiri kuna jinamizi lililojitokeza na kumeza akina dada wote huko makwao, kisha wakafunuliwa macho na kutahamaki kuona Tanzania bado kuna madada wana exist!!
Nikiwa mmoja wa wapenzi wa kuona dada zetu wanapendeza, kung'ara, kujawa na utashi, utanashati na madoido mbalimbali yenye kuzingatia maadili ya jamii katika urembo, mapenzi yangu haya kinamna yanaonekana kuingiliwa. Maana ghafla bin vuu, nimebakiwa na mshangao ulliochangamana na kero kutokana na kuongezeka kwa matukio ya 'u-miss'. Hivi kulikoni Waheshimiwa? Hivi nini kimetokea na imekuwaje siku hizi?!!!....
Kila kukicha tunasikia mashindano ya u-miss...kila kona, kila blog inaongelea u-miss, utasikia mara:
-miss mwananyamara, miss tabata, miss peramiho,
-miss kinondoni, miss kantalamba, miss ibadakuli, miss mabibo
-miss rukwa, miss kivukoni, miss bugurunikwamanyani, miss kyela
-miss mikoroshoni, miss mabatini, miss kahama, n.k..
Si hivyo tu, pia pameanza kujitokeza ma-miss matukio:
-miss wasomi, miss whatever.. n.k..
Cha kushangaza kama si kusikitisha ni kule kuona jamii nzima iko ndani ya wimbi hili, ikielea nalo bila kuuliza. Yaani inavyoonekana sasa ni kuwa kila mmoja amekuwa shabiki. Kwa kweli nadhani ni wachache wanaoona kuwa hapa kuna jambo lililojitokeza bali limefichika, ni jambo lenye madhara katika jamii, ni jambo la 'twisted priority'.
Katika twisted priority hii ni kwamba, uwezo wa kuwepo mashindano haya tunao, mazingara na malengo ya kuwepo mashindano haya yapo. Tatizo ni kwamba, vyote hivi vimevurugika au kukaa shaghalabagala na hivyo nia, malengo na madhumuni ya kumwendeleza Mtanzania kupitia mashindano katika sanaa hii nako kumevurugika kama si kuingia dosari.
Sitoendelea kuandika mengi kuhusiana na ma-miss wetu, ila nina wito kwa taasisi husika na wadhamini wa mashindano au sanaa hii:
Taasisi/Wizara:
==>Je, wanataarifa gani za kutupatia wanajamii kuhusiana na mchipuko huu wa mashindano? (wanaukubalia au kuukataa..)
==>Kama Wizara imeona jambo hili la kuongezeka kwa ghafla si jema, je imeandaa mkakati gani kulikabili?
==>Je Wizara na Taasisi husika zinashirikiana vipi na waandaji wa mashindano haya? (swala la vibali..)
Wadhamini:
==>Kwa vile wana uwezo wa kumudu udhamini, je ni mpango gani wanao katika kuchochea taaluma za vijana mashuleni kupitia mashindano mbalimbali?
==>Je, wanafikiria nini kuhusiana na swala la kuanzisha mashindano katika jamii ambayo yatatoa motisha kwenye mambo ambayo yanailenga jamii na mazingira yake kwa kuzawadia vijana au makundi ya vijana. Mfano katika:
---- Ujenzi wa vyoo
---- Usafi wa mazingira
---- Upandaji miti
---- n.k..
==>Ukiachilia mbali kuwezesha kujulikana kwa warembo wa Kitanzania ndani na nje ya nchi, je, wanampango gani na kuwawezesha warembo hawa kushiriki katika shughuli za maendeleo yanayogusa jamii moja kwa moja?
==>Ukiachilia mbali zawadi wanazowapatia washindi, je ni mpango gani wanao katika kuwezesha sanaa hii kuliingizia taifa fedha za kigeni bila kukiuka maadili yetu?
Napenda kumaliza kwa kusema kwamba, nia na madhumuni katika hayo yote niliyouliza ni kujua sisi kama wanajamii tuna mpango upi katika kuwawezesha vijana wawe wabunifu, washirikiane katika sekta mbalimbali ili 'hela hizo' za udhamini zisiende tu kwenye 'vipaji' vya watu ambavyo wamezaliwa navyo, bali hela na zawadi nyinginezo ziambatanazo na u-miss zitumike katika kuongeza tija, ubunifu na ufanisi wa kazi za vijana.
Shukrani; Naomba kutoa hoja.
SteveD.