ATCL yatoa hamasa, yatangaza kumsafirisha Miss Tanzania 2023 kwenye daraja la 'Business Class' kwenda kushiriki Miss World

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Ili kuongeza hamasa zaidi kwa vijana kutimiza ndoto zao na kuendelea kulinda hadhi ya mashindano ya 'Miss World' kwa washiriki wanaopeperusha bendera ya Nchi duniani, Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imeweka wazi kuwa itamsafirisha Miss Tanzania Halima Kopwe kwa kutumia daraja la hadhi ya juu ya ndege zake kwenda kushiriki shindano hilo.

Akizungumza wakati akitangaza mashirikiano kati ya ATCL na waandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania, The Look Company Limited, Mkurugenzi Mtendaji Mha. Ladislaus Matindi amesema mashindano ya Miss World ni fursa sahihi ya kukuza sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini na imekuwa na mchango mkubwa sana kwa vijana na Taifa.

“Ni imani yetu kuwa, kwa heshima Air Tanzania tuliyompa Halima Kopwe kutumia Daraja la Biashara (Business Class) kutoa Dar es Salaam, Tanzania hadi Mumbai nchini India, kutamuongezea hamasa na ujasiri zaidi na kuhamasisha vijana wengi nchini kuendelea kupigania ndoto zao”, amesema Matindi.

Aidha Halima Kopwe ambaye anatarajia kwenda kushiriki shindano hilo ameahidi kuendelea kutangaza vivutio vya nchi kikamilifu kwenye mashindano ya Miss World na kupeperusha bendera ya Tanzania kimataifa.

Shindano a kumsaka Mrembo wa Dunia maarufu kama “Miss World” linatarajiwa kufanyika mwezi Machi 2024, nchini India.

Itakumbukuwa ATCL imekuwa ikishiriki katika masuala mbalimbali katika jamii ikiwemo kutoa sapoti kwa baadhi ya wadau pamoja na kuingia mashirikiano.

Halima Kopwe alitwaa taji la Miss Tanzania 2022, ambapo mshindi wa shindano hilo upata tiketi ya moja kushiriki shindano la “Miss World”, ambapo shindano linatajiwa kufanyika mwanzoni mwa Mwezi March nchini India.
View attachment 2842188View attachment 2842189
JOS_0303.jpg
 
Haya ndiyo mambo mepesi kufanyikaga na kuamuliwa nchi
Nawashauri pia atc wawazungushe misomisondo dunia nzima pia
Waitangaze nchi hii

Ova
 
Back
Top Bottom