Mashindano ya 'U-Miss' Yamezidi. Michezo Mingine Tumeisahau?...Twisted Priority?

Dah mkuu naona umesahau kidogo juzi kati hapa kulikuwa na mashindano ya ngumi Kitaifa viwanja vya Leaders hakuna hata kampuni lililo zamini wala hata maji ya kunywa nashangaa wamejikita kwenye mashindano ya vichupi na wanayapa kipaumbele sana kuliko michezo mingine.

vichupi vinalipa maana wabongo kwa kupenda kuona nyeti na kuvuta hisia za ngono na mwishowe kungonoana kiukweli, hilo tu. we angalia zamani netball ilikuwa na wapenzi wengiii kisa tu ilikuwa ni vile visketi vifupii na chupi ndani mtu akiruka mambo yote hadharani, lakini siku hizi tangu zije skin tight wanawake wanavaa hadi magotini, hakuna tena mvuto wa kuona mapaja netball imekufa kabisaaaa. na urembo wakileta uvaaji wa magauni na skirt ndefu, baibui n.k. utashangaa Lundenga atkosa dili tu! Two weeks ago nilikuwa na workshop pale Giraffe hotel na hao walimbwende walikuwapo hapo basi ilikuwa mtafaruku mtupu!
 
Dah mkuu naona umesahau kidogo juzi kati hapa kulikuwa na mashindano ya ngumi Kitaifa viwanja vya Leaders hakuna hata kampuni lililo zamini wala hata maji ya kunywa nashangaa wamejikita kwenye mashindano ya vichupi na wanayapa kipaumbele sana kuliko michezo mingine.
Hayo ni matokeo ya viongozi na wanamchezo huo kukosa ushawishi katika kutafuta udhamini.

Hao wanadondi kwanza wamejisafisha na kashfa yao ya kubeba unga?
 
"........how long shall they...........while we stand a side and look? ohh some say its just a party of it..................." Bob Marley. How long?
 
Asante sana kwa kunifungua macho, na kidumu chama cha maf. Nimefurahishwa na jinsi jamii ya wana JF wanavyo jadili mambo. Hata hivyo nina maoni kidogo.

Mi ni mmoja wa wanariadha mstaafu ambaye siye rasmi, na nina machungu mno na nimechoswa sana na hoja na hoja zenu za nyingi za kisomi na kisiasa ambazo huwa zinaishia kwenye magazeti, pamoja na jamvi la wana JF, wakati hali halisi hamuijui.

KIBUNANGO sijui wewe ni kigogo gani? lakini ngoja nikumegee fikra zangu japo kwako ni pumba "What I have discovered in my one-and-a-half-year stay in Tanzania is that athletics is dead. Nobody is taking care of it, bodies concerned talk too much about it but no action is taken," he told The Guardian on Sunday. hiyo ni nukuu ya Hans-Peter Thumm.

kimsingi huyu muheshimiwa anasema hivi! "Nobody is taking care" au no body cares, kwani hiyo lugha ni ngumu kuilewa? na kisha anaendelea "talk too much about it but no action is taken" kama wana JF katika kujadili kwao hawakumuelewa muheshimiwa huyu, basi tunatatizo katika jamii yetu yakujazana maofisini na elimu ya "upe"

Inasikitisha kuona kigogo kama wewe unawalaumu vijana wa boxing kubebeshwa unga, wakati unajua kuwa wabebeshaji ni vigogo kama wewe? ni kweli hujui kama njaa mbaya? mambo yenyewe too much talk, sio kwamba nna halalisha fikra zangu.

Je boss unajua sababu inayo wafanya vigogo wawe too much talk, less action kwenye boxing na riadha, halafu vigogo hao hao wanakuwa less talk, too much action kwenye ulimbende?

Hapo bado najiuliza inakuwa vipi watu hawaoni hili? "Local long distance athletes have been doing well in the international races because of their own individual efforts but there were no proper developmental plans to make them maintain those standards," Hans-Peter Thumm. Mbona huyu mtaalam wa kijerumani anasema mambo ambayo ndiyo ambayo mimi nayazungumzia? Hakuna budget kwenye riadha wakimbiza upepo wa mbio ndefu ni juhudi zao tu.

Kwa ufupi mimi niliwahi kujifunza mbio, 100, 200, nilikuwa Znz hapo Amani. wakati naanza nilikuta vijana wanakimbia 10.9, 10.7, 10.6. mita 200- 21. fulani. Niamini mimi kaka hii ni kweli, nilikaa miaka miwili kule nilicho kishuhudia ni vijana kufanya mazoezi na njaa pamoja na vifaa duni. wengi wao walikuwa wanakuja kwangu kula chakula cha mchana ili waweze kukimbia.

Niliukimbia na mchezo wenyewe kabisa, nilipo rudi Zenji baada ya miaka minne nilikuta wale vijana wameacha riadha wameoa, jobless na wengine wanauza madafu. Nilitamani kulia niamini mimi kaka.
Wakati huo mchumba wangu alikuwa anafanya research ya athari za media kwa jamii ya kitanzania, hasa the influence of western media to Tanzanian youth. Nikaanza kufatilia nae mashindano ya ulimbwende kuanzia vitongojini, huwezi kuamini kaka pesa iliyokuwa ikiingia huko. sasa hivi nasoma kwenye magazeti tu pesa inayotumika kuandaa mamis vitongoji hata siamini.

wakati huhuo wanariadha wetu wa mbio ndefu wanakimbia kwa juhudi binafsi. Kilichoua riadha sio ulimbwende ila ni vigogo wetu, wamewekeza kwenye ulimbwende. Je motisha yao ni nini? Ahh mjomba unataka tuje kukuomba nauli?
 
Mimi nauliza hawa Vodacom wanalipa kweli kodi inayostahili maana kila mahali ni wao wadhamini. Vituo vya watoto yatima ni wao ( jambo jema ) lakini haya mashindano ya umiss ni kuzidi kulididimiza taifa kwa namna moja au nyingine. Mabinti hawasomi shule kazi ni kujiandaa kuwa mamiss sasa tunajenga kweli au tunabomoa kweli taifa letu.. Ukiangalia hao mamiss ndio wenye vituko vingi mjini. Ukimwi bongo hauwezi kuisha kwa mtindo huu. Vodacom kama mna hela nyingi basi jengeni barabara au mashule mtakuwa mmefanya la maana kwani ni wengi watafidika sio umiss tu kila siku kama si kuendeleza uzinzi kwa kwenda mbele. Nchi zilizoendelea hawafanyi hivi kama bongo umiss imekuwa kama ajira ambayo kwa upande mwingine hailipi bali inaua taratiiiiiiiiibuuuuu!!!
 
Back
Top Bottom