Mradi wa Tanzania wambeba miss world 2024

Wild Flower

Member
Jul 20, 2023
80
96
Krystyna Pyszkova kutoka Jamhuri ya Czech ameshinda taji la Miss World 2024 katika fainali ya mashindano hayo tarehe 9 Machi 2024 jijini Mumbai- India.

Krystyna Pyszkova kutoka Jamhuri ya Czech amejinyakulia taji la Miss World 2024 katika sherehe kubwa iliyofanyika kwenye Jio World Cinema huko Mumbai siku ya Jumamosi kutoka kwa Karolina Bielawska kutoka Poland.

Kupitia mradi wa “ Beauty with purpose” uliopo nchini Tanzania amefanikiwa kujitolea na kuanzisha shule ya kiingereza kwa watoto wasiojiweza nchini Tanzania.

Mbali na mataji yake, Krystyna alipokea Tuzo ya Mbunifu Bora wa Mitindo - Ulaya. Aliwashinda washindani akiwemo Sini Shetty wa India, Aché Abrahams wa Trinidad na Tobago, na Lesego Chombo wa Botswana. Mshindi wa pili alikuwa Yasmina Zaytoun kutoka Lebanon.

Aidha mwakilishi wa Tanzania katika mashindano hayo, Miss Tanzania Halima Kopwe, alifanikiwa kuingia kwenye kundi la mwisho la washindani 40 kati ya 112 walioshiriki.

Mara ya mwisho mwakilishi wa Tanzania Nancy Sumari kufika hatua ya mwisho 40 ilikuwa mwaka 2005.
 
Ninaamini wazazi wa hawa watoto walishirikishwa kabla ya picha zao kuanza kutumika huko Duniani
 
Jamqniiiee
Screenshot_20240310_181455_Instagram.jpg

Mkali
 
Ninaamini wazazi wa hawa watoto walishirikishwa kabla ya picha zao kuanza kutumika huko Duniani
Ikiwa hawajashirikishwa una maoni gani? Kabla ya kwenda kwenye mawazo yako hizi picha hazina ushahidi kama huyu mtoto ni wa flani hata ukifungua kesi unapoteza muda tu mpaka sura itambulike na sio kukisia kisa umeona kichogo.
 
Back
Top Bottom