Masha atoweka na samani za ofisi ikiwemo picha ya rais!

Lakini hii imekuwa ni tabia ya wanaCCM wengi kwa kumbu kumbu zangu

Mh Waziri mkuu mstaafu ama aliyejiuzulu sijui kufukuzwa Lowasa aliondoka na thamani za nyumba ya waziri mkuu tena usiku alipokuwa akihama.

Mzee Sumaye naye aliondoka na thamani akahamishia kwake

Mzee Jumanne Malecela naye aliamua kung'oa mashine za maji kule Mtera alizoziweka kwa mbwembwe baada ya kushindwa akachukia

Huyu naye Masha anabeba hata picha za ukutani

Kazi kweli kweli

Mkuu, kwahiyo masha alichofanya ni kudumisha mila kwa kuendeleza ule utamaduni wao wa chukua chako mapema.
 
Tuangalie lisiishie ofisi ya Mbunge pekee,hata Nahodha aangalie ofisi yake zisije chuliwa droooo.
:whoo:
 
Sidhani kama Six atafanya hivyo maana sasa hivi hata kama anadhamiria, basi kashasikia jinsi wenzake wanavyokaangwa. Pia hatujasikia kama Mama Makinda akilalamika kuwa kakuta Ofisi au Makazi ya Spika wa Bunge yakiwa meupe. Wanyamwezi tuna kaustaarabu ketu pamoja na umasikini wetu na kuchagua CCM.

Mwisho niseme kuwa Mbunge/Waziri Sitta ni wa URAMBO na si SIKONGE.

Ng'wanangwa, unataka kutuambia nini sasa kituko hiki cha Mwanza? Tena Nyamagana...................
Hivi ile ofisi ya mzee six ya Sikonge siku akiamua kuondoka na samani zote nani ataulizwa
 
Masha ang'oa vitasa ofisi ya Mbunge Mwanza Send to a friend Tuesday, 30 November 2010 01:46 0diggsdigg

anaalongamasha.jpg
Frederick Katulanda, Mwanza
ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, amehamisha vifaa mbalimbali vya ofisi ya Bunge Jimbo la Nyamagana, kwa madai kuwa alivinunua mwenyewe kipindi uongozi wake. Akizungumza na Mwananchi jana, Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje, alisema baada ya kutoka Bungeni alikwenda kuingia katika ofisi hiyo, lakini baada ya kukabidhiwa alikuta vitasa vya mlango, simu ya mezani picha ya Rais na samani za kukalia vikiwa zimechukuliwa.

Kwa mujibu wa Wanje, baada ya kufuatilia aliambiwa kuwa vifaa hivyo viliondolewa na Masha kwa madai kwamba, alivinunua kwa fedha zake mwenyewe.

“Nimefuatilia kwa DAS (Katibu Tawala wa Wilaya) nikaambiwa amechukua Masha, nikafuatilia kwa Katibu Tawala wa Mkoa yeye alijibu kuwa naye alifuatilia suala hilo kupitia kwa Das na kupewaa majibu kama yangu, sasa sijajua ni kwa nini, ninavyojua ofisi haipaswi kukosa samani kwa vile kuna fedha za kununulia vitu hivyo,” alisema.

Kwa Upande wake, Masha alikiri kuondoka na vitu hivyo na kwamba, asingeweza kuacha vifaa vyake binafsi katika ofisi hiyo.

Masha alisema vifaa alivyoondoka navyo ni vile tu ambavyo ni mali yake.

“Wakati naingia hapa nilikuta ofisi ikiwa na kiti kimoja na meza tu, vifaa vingine niliweka vyangu, kama kompyuta na meza zake, simu na samani nyingine kulingana na mahitaji yangu,” alisema Masha.
Alisema Wenje anapaswa kuwasiliana na ofisi ya mkuu wa wilaya, ili kupewa vifaa vya ofisi hiyo ambavyo yeye aliviondoa alikuwa havitumii kwa vile wao wanajua vilipo.

“Jamani vifaa vya ofisi anapaswa kuuliza ofisi ya mkuu wa wilaya, sasa kama anataka nimwachia na vyangu binafsi, mie nimetoa vyangu…hivyo vya ofisi vipo, nadhani amefika na kukutana na kiti kimoja na meza vile vingine vilivyokuwemo pia vilikuwa mali ya ofisi,” alieleza Masha.

Hata hivyo, Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza (RAS), Doroth Mwanyika, hakuweza kupatikana kuzungumzia suala hilo kutokana na kuwa nje ya ofisi, lakini ofisa mmoja wa ofisi yake alithibitisha kuwepo kwa malalamiko ya Wenje na kwamba, yalikuwa yakishughulikiwa.
 
Hiyo ndiyo picha halisi ya viongozi wa CCM. Wanadhani uongozi ni hati miliki yao na kamwe hawakutarajia wapinzani kuwang'oa. Kama ni mali yake kweli, ina maana ofisi haina samani, kwa maana hiyo ina maana fedha alizokuwa anapewa kuendeshea ofisi yake yabkibunge kainywa na tafsiri sahihi ni ufisadi black and white.

Ningedhani anasema hakukuwa na ofisi ya bunge na iliyopo ilikuwa ni nyumba yake au alipanga kwa hela yake na mpangaji akiondoka kwa kweli huondoka na mali yake. Sasa kama ni ofisi ya Bunge anatakiwa kufuatiliwa na ofisi ya Bunge imshitaki kwa uharibifu huo. Anapoondoka kiongozi inaeleweka kwamba ofisi inabaki na samani zake za kiofisi zilizonunuliwa kwa madhumuni hayo. Sasa kunyofoa ni wizi.
 
mbona hata malecela aling'oa mabomba na mashine aliyofadhili huko jimboni mtera?
au hawa wanachama kawaida yao?


nakumbushwa ule wimbo maarufu:

kamnunulia simu mpenzi wake,
walipoachana akamnyang'anya!
 
Du! Nimesikia hata picha ya Rais kaondoka nayo, it seems he is so stubbon and selfish!! lack of qualities as a leader....
 
Too bad Masha. Siasa za visasi za nini? Kama pesa unayo nyingi. Unafikiri unajenga taswira gani kwa wananchi hata kama vitu ulivinunua wewe?

Iga mfano wa Diallo. Watu wanamfagilia kuwa ni Muungwana pamoja na kushindwa.

Uongozi ni kuonyesha njia. Vitu ulivyonunua hata kama vyako ni kwa faida ya umma, so why take them back?
 
Masha kanikumbusha maisha ya hostel, mtu akigombana na mate wake na akaamua kuhama chumba, anachana kapeti nusu alilochangia na pazia nusu ili mradi wote wakose na kukomoana. Ila huu ni utoto. Tajiri mzima unabeba 5 years used furnitures????

MASHA UNA WIVU MEZA KIWEMBE TUJUE MOJA........
 
Ndiyo Madhara ya Kuchagua Wafadhili kuwa Wabunge Badala ya Kuchagua Wawakilishi, Anaweza asiishie hapo , msije Shangaa wananchi wanatozwa mia mia kwa ndoo kuchota maji kwenye visima alivyochimba Masha
 
Ni kweli kabisa, hiyo ndio picha halisi ya viongozi wa CCM. Ila hakusema kama alikuta ofisi bila vitasa!!!!
 
CCM ndivyo walivyo hata Malecela aling'oa mashine ya maji aliposhindwa kura za maoni Mtera.
 
kwanza si wa-issue a trespass notice na conversion! wanasheria wote bongo wanafanya nini?
 
Masha Lawrence

Najua WW NI MEMBER WA JF

Ww ni Mjinga tena huna Akili..........kukosa Ubunge ndio uondoke mpk na Picha ya Raisi ambaye ni Mshkaji wako wa Karibu.Vtasa huna Kwako ama? Ni njaa au ni nini Unategemea tutakufikiria vipi?

Serikali inatoa fedha kwenye bajetikwqa ajili ya kununulia Samani za Ofisi zake wewe unaondoika nazo........ni Hasira ya Kushidwa Ubunge..........

M2 msomi kama ww unafanya mambo kama Hujaenda Skuli yaani siamini macho na masikio yangu

Umenikere sana kwani nilikuwa nakuheshimu sana Kumbe Buree kabisa
 
Muache apore hizo ndio sera za chama chao I hope anataka kufungua nazo ofisi Rose Garden maana alikua hakauki pale
 
Hata kama hivyo anadai ni vyake (although alipewa posho hence kodi zetu) basi aturudishie vile alivyovikuta wakati anaingia Je? alivipeleka wapi
 
Masha na Sophia simba wanavyopendwa humu ndani?????
cheki hii sredi itakavyokwenda!:party::party:
 
Back
Top Bottom