Masha atoweka na samani za ofisi ikiwemo picha ya rais!

Dadayangu Adela wa Madilu huyu angekuwa na hirizi angeshinda ubunge lasivyo aliyempa alimdanganya na imekula kwake........
 
Vingine vyote acha ata Picha ya raisi aliinunua kwa pesa zake?
Ni kujishushia hadhi seriously bse unaweza kuta ivyo vitu havifiki ata 20mil!
 
Duh jamani hawa jamaa wanaongea mno na vyombo vya habari. Sasa kama issue ndogondogo hivi zinashindwa kumalizwa kimya kimya, je complex issues itakuwaje?

Mzee kwa Waziri Aliemaliza muda wake kufanya kitu kama hiki sidhani kama ni kitu kidogo na cha kunyamaziwa. Si baraza zima linaweza fanya kama hv hata kama wamenunua hizo samani wenyewe?
 
Na Frederick Katulanda, Mwanza

Nimeangalia haka kaandishi kalikoandika huwa kanapigwa sana na Green Guard ndiyo maana kanaandika sana tuvitu tudogo mmnoooo, duuuuu ila Nimecheka sana....sijui ni kufulia ama nini?
 
:teeth: :teeth: Taanzaaniiiiiia Tanzaniyaaaa.... Nakupenda kwa moyo woooteeeeee.....:teeth::teeth::teeth:
Tunaimba bila uzalendo... tukijitolea ni kwa maslahi maalum, maslahi yakiisha nasi tunaondosha yalio yetu.... Hapo ndipo tunapomaanisha kwamba UJAMAA na UZALENDO uliisha siku nyingiii... Zile semi za zamani NITATUMIA ELIMU YANGU KWA FAIDA YA WOTE leo ni ndoto za MWENDAWAZIMU! Ninapotazama wapi Tunakwenda huwa sipati majawabu kwa maswali yangu... kwa mana KILA MMOJA SIKU HIZI ANAITAZAMA NAFSI YAKE TU! UJAMAA ULISHAKUFA KITAMBO! WABINAFSI, MAKABAILA na MABWANYENYE wameshika hatamu. HAYO NDIYO MAADILI YA VIONGOZI WANAOPEWA MADARAKA NCHI HII! Heri yao wenye kuimba nyimbo wasizojijua kwa maana ni kama watoto wasioweza kutambua bali yale waambiwayo na wakubwa wao :embarrassed:
Sipendi kusema jambo hapo.... yawezekana alikwiba, yawezekana alitaka kuwa mbunge milele... kwa maana mwingine alijenga nyumba ya spika huko nyumbani!!! yawezekana alitaka wayamalize ikashindikana ndiposa akaamua kwiba "maana ilitakikana wafanye makabidhiano!" nahofu sana kusema "kama ndivo hivi alivo Mh. LM....., sijui ile mikataba aliyoingia kwa niaba ya Serikali ikoje!?" naiogopa sura ya picha hiyo kunijia................:redfaces:
 
Hatimae yule aliyekua Waziri wa Mambo ya ndani Lawrence Masha amehamisha vifaa mbalimbali vya ofisi ya ubunge Jimbo la Nyamagana kwa madai kuwa alivinunua yeye mwenyewe kipindi cha uongozi wake. Masha alidai kua wakati anaingia ofisini alikuta kiti kimoja na Meza tu! vifaa vingine kama Computer,Simu na vitu vingine alinunua mwenyewe. Jamani hivi ofisi ya mbunge awe wa chama chochote kile kilichopata ridha na wananchi kuongoza ni nani anaye gharamia kutengeneza ofisi ya mbunge? kwakua inanishangaza sana kusikia kua bwana Masha siku anakabiziwa ofisi akiwa mbunge kwa awamu iliyopita eti alikuta kiti na meza tu? Waungwana mnaweza kuchangia hoja!:A S embarassed:
 
Hata aking'oa haisaidii, Chadema itapeta tu. Chuki binafsi hizo hazimfikishi kokote. Hovyooooo!!
 
Inauma kukosa ubunge. Mwacheni achukue ndumba zake asije leta mkosi kwenye ofisi ya mh. Wenje

 
Kuna wanaume akimnunulia vitu mwananke wakiachana anadai kurudishiwa "vitu vyake"! Akili ya Marsha ni kama wanaume aina hiyo. Alinunua vitu na kuweka kwenye ofisi ya Umma kana kwamba ni "mwanamke" wake. Wananchi wamenfukuza baaada ya muhula mmoja kakasirika na kuondoka na "vitu" vyake. Akili ya kitoto kweli kweli! Huyu ni mtu ambaye kwenye kijiwe fulani alisikika anasema eti ni "Presidential material!" Hajui akitataka kugombea tena mambo haya yatamrudi?
 
lakini hii inapendeza kujua SERIKALI ILIKUWA NA WATU WA AINA GANI JAMANI???HUYU RAIS ALIKUWA AKIAMBIWA UKO NA UCHAFU PEMBENI NA UCHAFU SI LAZIMA UNUKE KIKWAPAATAKI KUAMINI HII AIBU SIJUI ANAIPELEKA WAPI SHAME N U MASHA
 
Nyambala, kwa vile amevinunua kwa fedha zake za mfukoni, basi anavyo haki navyo maana ni jasho lake, lakini hili la kufikia kungoa hadi vitasa, ni umasikini wa roho. Hapa anatuaibisha Wasukuma, ni kabila la watu ambao ni matajiri sana wa roho, hatuna roho za kimasikini na ile roho ya kwanini.

Kwa waliosoma ile tamthilia ya 'Song of Lawino' mwandishi alisisitiza sana from time to time "The Pumpkin of the old homestead must not be aprooted", akimaanisha ukihama makazi, sio lazima ungoe mpaka maboga ambayo kwa kuyang'oa yatakufa na hatakufaidia chochote huko uendako kwenye makazi mapya.

Lets give Mh.Masha the benefits of doubt kuwa hali yake ya kiuchumi ni mbaya sana kwa sasa, hivyo amekosa fedha za kununulia kitasa kwenye makazi yake, na kwa vile kitasa kile alikinunua yeye kwa fedha yake, bora akaking'oe na kukipachika kwake, sambamba na lile zulia, then he is right.

Tafadhali ndugu yangu Masha si Msukuma ni Mshosha! Wasukuma si wajinga kama Masha.
 
unajua mwizi akikosa cha kuiba anawza kutundika hata shati lake dirishani kisha akazunguka nyuma ya nyumba na kuanza kulivizia,
akiwa ananyata taratibu..... masha kakosa magumashi sasa ameanza kuvizia.....hahahhaha
 
Tafadhali ndugu yangu Masha si Msukuma ni Mshosha! Wasukuma si wajinga kama Masha.

masha ni MZINZA wa kijiji cha Nyamatongo wilayani sengerama, mama yake masha ndo tapeli mkubwa huku mwanza ......... anashirikiana na '' mke hewa'' wa marehemu Claus mmiliki wa vivuko vya kamanga ferry.....

baba yake ni dk Fortunatus Lwanyantika Masha... ndo hwa walifukuzwa na mzee wetu MWL miaka ileee ya 1961....

kwa kifupi Lawrence masha ni jizi
 
Lakini hii imekuwa ni tabia ya wanaCCM wengi kwa kumbu kumbu zangu

Mh Waziri mkuu mstaafu ama aliyejiuzulu sijui kufukuzwa Lowasa aliondoka na thamani za nyumba ya waziri mkuu tena usiku alipokuwa akihama.

Mzee Sumaye naye aliondoka na thamani akahamishia kwake

Mzee Jumanne Malecela naye aliamua kung'oa mashine za maji kule Mtera alizoziweka kwa mbwembwe baada ya kushindwa akachukia

Huyu naye Masha anabeba hata picha za ukutani

Kazi kweli kweli
 
ni comment yangu mkuu....

sometimes we have to take a mickey out of the situation hadi tujue kama aliweka yeye au la; pia ni vizuri kupata facts kwani bongo waweza zushiwa chochote

KUMBUKA KUNA MTU ALISEMA MASHA KAKIMBILIA MAREKANI NA NAFASI YAKE IMMMA KAMUACHIA MTOTO WA KARUME


mkuu, Masha keshakiri kwamba ni kweli amechukua kila kilicho chake, kwamba hizo samani alinunua kwa pesa yake.

Sasa hapa tunatakiwa tujiulize na tumuulize Masha, kwamba ofisi ya bunge imeshindwa kuhudumia ofisi za wabunge?

Hebu hata wewe fikria kidogo tu, hata vitasa anang'oa? hata kama alinunua kwa pesa yake haiingii akilini wala si busara kabisa na huyu ndiye alikuwa waziri. Hata huku uswahilini kwenye nyumba za kupanga tunanunua sana vitasa lakini tukihama tunaviacha.
 
Masha ameibua mjadala mzuri. Ikiwa pesa ilitengwa ya kununua thamani, nayo imeliwa na wajanja wilayani, na wakati huo huo alikuwa ni Waziri wa mambo ya ndani ambaye angeweza kuamrisha uchunguzi ufanyike, lkn hakufanya. anatupatia picha kwamba ni mwoga na anakumbatia wabadhilifu. tafadhali JKM huyu dogo hafai. Amenikumbusha stori ya mwanamke aliyetaka mtoto wa mwenzake achinjwe mbele ya mfalme Sulemani, ILI WAKOSE WOTE!
 
Back
Top Bottom