Masha atoweka na samani za ofisi ikiwemo picha ya rais!

Nadhani anajisahau anadhani bado ni waziri wa mambo ya ndani, kwa hiyo vitu vyote vya ndani ni vyake.
No. Hakuwahi kutofautisha kati ya fedha yake na fedha za serikali kwani zote zilikuwa zake.
No.Mali ya serikali ni ya wote akichukua yeye na ikibaki pale si sawa tu? Wenje ana roho mbaya.
Samani zina Hirizi si vema kumuachia Wenje Hirizi zitamdhuru.
Ali sota sanawakati wakunua samani hizo vipi Wenje apate raha?
Kila mwaka kuna bajeti ya samani za mbunge huyu wenje vipi? si aende akadai zake?

Mimi naitwaga Masha, Niliishigi Marekani na madingi wangu wakimbizi, naongea makiingreza hayo wee! Hata Mkwere anazimiaga kabisa.Nikaendaga kusomaga UDSM nikaitwaga Mniga kwa sababu ya makiingereza yangu, nikaibiaga rire ribeki rikubwa nikawaga mirionea kupitia rikampuni ra kijani. nikagombeaga uupunge nikashindaga Riraisi rikanipaga uwazir wa miporizi yote pamocha na riporisi rikubwa kabisa riMwema naro rikiwa chini yangu kabisa. Nikapitaga bira kupingwa harafu nikapingwa na riwenje nikashindwaga upunge kwenye makura, nikariaga mimachozi kweri ri mkwere hrikuja kunisaidia,kwa mihasira yangu ya kingosha nikaiba misamani ya opisi ya upunnge mimi naitwaga Lau siongopi riporisi rorote hata rire riMwema.
 
Hata kama ni hasira, kuondoka na kitasa ni rekodi mpya kwa mtu ambaye juzi tu alikuwa waziri wa mambo ya ndani. BBC wanaweza kutangaza suala hili kupitia VISA na MKASA ya Kikeke ya Jumamosi.
 
Mashaaaaaaaaaaaaaaa what a mark you are leaving!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Yuko wapi Willy achangie na hili?
 
How low can he go? That is the question I am trying to ponder. Anyway, people of Nyamagana made a right decision to evict this classless guy from public office. What he did can simply be summarized as despicable and shameless act, totally unbecoming to a person of his stature.
 
Sijui kwa nini Masha amekuwa kwenye "adolescence" kwa muda mrefu? Popote pale utakapomkuta lazima "ataharibu"! Hata baa e.g ukimkuta Rose Garden akishalewa utadhani ni mpiga debe!
 
Nadhani itabidi arudishe ile allowance aliyokuwa anapewa na Bunge ili ku-maintain ofisi yake jimboni.
 
Hawo ndiyo walikuwa mawaziri wachapakazi wa mheshimiwa Dr Jakaya Mrisho Kikwete, hata Dr Slaa alisema kule Bukoba wakati wa kampeni kuwa kuna mbunge mwanamama aliondoka na thamani za ofisi na serikali ikabidi ilipe faini kwa kosa hilo, lakini kwa kulindana hakuchukuliwa hatua yeyote na tena akapitishwa kugombea tena Ubunge kwa hiyo ndiyo maana jamaa ameamua na yeye kuchukua tu maana si ni vya serikali ambayo haijali na hawawezi kumshitaki,sikiliza hata hao wahusika ambao ndiyo walitakiwa kuchukua hatua dhidi ya mali ya umma hamna kitu.
Tutaendelea kutawaliwa sio kwamba hatuoni ila ni ujinga wetu ila mwisho wa yote itakuwa shida maana kila kitu kitakuwa kigumu.
Mpaka kufika 2015 naona ni mbali hebu fikiria tayari gesi mtungi wa kilo 6 imepanda kutoka 14500 mpaka 16000
Ewura wakiulizwa bei elekezi wanasema mtoa habari hayupo ofisini (labda 2014 july wanaanza kutoa bei elekezi)

Jamani watanzania tuamumke na tukatae Tshirt,kovia ,kanga na 10000 ili tujitawale tuondokane na hii mikono ya wanyonyaji

Ningekuwa na nguvu ya Umma ningeitisha maandamano nchi nzima kudai au kuilazimisha serikali kuhusu mpango wa kubadili katiba
Haiwezekani watu wanatoka jasho (Dr Slaa mfano) kwa ajili ya maslahi ya watu wote lakini wapo ambao hata wakiomba ubalozi wa nyumba kumi hawapati (Sofia Simba na wengine mifano hai) eti wanakuwa maMP na Mawaziri pamoja na wakuu wa mikoa ,wilaya,makatibu wakuu,wawakilishi wa nchi nk

jamani watanzania katiba maana bila katiba mpya hakutakuwa na mabadiliko hata miaka 30 ijayo

katiba katiba katiba!!!!!!
 
Wamfungulie kesi ya wizi tu ili aje athibitishe kuwa hivyo vitu alivinunua kutokana na fedha yake yeye mwenyewe; this is so petty!
 
Duu...!! huyu ndio miongoni mwa mifano ya viongozi wetu,
kwa lugha simple unaweza kusema huyu ni kiongozi mwizi..
 
Wamfungulie kesi ya wizi tu ili aje athibitishe kuwa hivyo vitu alivinunua kutokana na fedha yake yeye mwenyewe; this is so petty!

Wenje anaitaki kufanya upembuzi yakinifu na akipata data kamaili then anaweza kwenda kutafuta haki kwa kina 'pilato'. Lakini level ya uchakachuaji kwenye idara za umma sishangai kibao kikigeuka ... ukifikiria nje ya boksi ..hili suala laweza kuwa zaidi ya samani hizo mfano a calculated move to annoy and make someone commit defamation et al kisha kupigwa faini ya 'visenti'
 
Kukosa Ubunge ni kufunga milango iliyokadiriwa kufunguka kwa wakati.
Kinyongo chake si kidogo. Nyani Ngabu, usemi wako wa Miafrika..... napata wakati mgumu kuukataa

Afunguliwe kesi ya wizi pamoja na mkurugenzi wa Manispaa aunganishwe hapo kwani ndiye aliyeruhusu Masha aingie ofisi ya mbunge wakati si mbunge.
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, samani na nyaraka muhimu zilizokuwa katika ofisi ya mbunge wa Nyamagana, jijini Mwanza, ikiwemo picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete, 'zimetoweka'.

Kutoweka kwa samani hizo zilizogharimu fedha nyingi kutoka ofisi ya Bunge kulibainika jana baada ya mbunge mpya wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (CHADEMA), kuingia rasmi kwa ajili ya kuanza kazi.

Alisema, samani hizo zimeibwa katika kipindi cha siku mbili za hivi karibuni kwa kuwa aliwahi kufika kwenye ofisi hizo na kuzikuta baada ya kutoka bungeni.

"Niliwabana viongozi ngazi ya wilaya na mkoa wanieleze vimeenda wapi hivi vitu… niliambiwa eti vilinunuliwa na mtu binafsi na havikuwa mali ya serikali," alisema mbunge huyo.

"…Ofisi ya mbunge ni mali ya umma kama ilivyo Ikulu (Ofisi ya Rais), fedha za walipakodi zinatumika kugharamia; sasa hivi vitu nani kaviiba?" alihoji Wenje kwa masikitiko.

Na wenje nae basi anunue vyake na akiondoka nae aondoke navyo...

tunapenda sana vineno-vineno,
 
Masha ang'oa vitasa ofisi ya Mbunge Mwanza

Na Frederick Katulanda, Mwanza
ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, amehamisha vifaa mbalimbali vya ofisi ya Bunge Jimbo la Nyamagana, kwa madai kuwa alivinunua mwenyewe kipindi uongozi wake. Akizungumza na Mwananchi jana, Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje, alisema baada ya kutoka Bungeni alikwenda kuingia katika ofisi hiyo, lakini baada ya kukabidhiwa alikuta vitasa vya mlango, simu ya mezani picha ya Rais na samani za kukalia vikiwa zimechukuliwa.

Kwa mujibu wa Wanje, baada ya kufuatilia aliambiwa kuwa vifaa hivyo viliondolewa na Masha kwa madai kwamba, alivinunua kwa fedha zake mwenyewe.

"Nimefuatilia kwa DAS (Katibu Tawala wa Wilaya) nikaambiwa amechukua Masha, nikafuatilia kwa Katibu Tawala wa Mkoa yeye alijibu kuwa naye alifuatilia suala hilo kupitia kwa Das na kupewaa majibu kama yangu, sasa sijajua ni kwa nini, ninavyojua ofisi haipaswi kukosa samani kwa vile kuna fedha za kununulia vitu hivyo," alisema.

Kwa Upande wake, Masha alikiri kuondoka na vitu hivyo na kwamba, asingeweza kuacha vifaa vyake binafsi katika ofisi hiyo.

Masha alisema vifaa alivyoondoka navyo ni vile tu ambavyo ni mali yake.

"Wakati naingia hapa nilikuta ofisi ikiwa na kiti kimoja na meza tu, vifaa vingine niliweka vyangu, kama kompyuta na meza zake, simu na samani nyingine kulingana na mahitaji yangu," alisema Masha.
Alisema Wenje anapaswa kuwasiliana na ofisi ya mkuu wa wilaya, ili kupewa vifaa vya ofisi hiyo ambavyo yeye aliviondoa alikuwa havitumii kwa vile wao wanajua vilipo.

"Jamani vifaa vya ofisi anapaswa kuuliza ofisi ya mkuu wa wilaya, sasa kama anataka nimwachia na vyangu binafsi, mie nimetoa vyangu…hivyo vya ofisi vipo, nadhani amefika na kukutana na kiti kimoja na meza vile vingine vilivyokuwemo pia vilikuwa mali ya ofisi," alieleza Masha.

Hata hivyo, Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza (RAS), Doroth Mwanyika, hakuweza kupatikana kuzungumzia suala hilo kutokana na kuwa nje ya ofisi, lakini ofisa mmoja wa ofisi yake alithibitisha kuwepo kwa malalamiko ya Wenje na kwamba, yalikuwa yakishughulikiwa.

My Take: Hivi huu ndio utamaduni wa vingozi wetu au ni baadhi tu? Vp naye mkuu wa kaya akifanya hivi pale jumba jeupe?


Source: Mwananchi 30/11/2010
 
MHHH... Hebu niwaze kidogo....
Lau ni mwanasheria..anajua kabisa quid quid plantatur solo solo cedit!..... sijui kama kang'oa kilichomo kwenye jengo au kainua kitu alichokibeba na kukiingiza ndani ya ofisi .. chenye kuhamishika. Kama kang'oa - huo ni uharibifu na ni kosa la jinai... sheria ichukue mkondo wake. Kama kahamisha alichokileta basi hapo tutamshangaa tu kwa kutokutumia hekima lakini hatuwezi kumshutumu maana ni mali yake.
Masha umejiangusha na kujidhalilisha sana.Hivi kweli wewe uliwapenda wapiga kura wako? Kama uliwapenda si ungewaachia huto tusamani? Ulivyo na uchache umeshindwa nini kutoa hata donation ndogo ya used samani kwa wapiga kura waliokupigia 2005 na hatimaye kukuwezesha ukawa mbunge na hatimaye waziri?Ni manufaa mangapi uliyapata kwa uwaziri wako ? Umeshikwa na nini hadi uwe na mtimanyongo ivo? Ni hasira za kuukosa Ubunge 2010? SHAME!
 
Na wenje nae basi anunue vyake na akiondoka nae aondoke navyo...

tunapenda sana vineno-vineno,

Mkuu, siamini kama huuu ndio ushauri unaoweza kutoka kwako, nadhani hujaisoma vizuri comment yako, hebu i-review!!
 
mi si dhani kam ni ustarabu kutoka na dhamani za offisi hata kama ulinunuwa kwa pesa yako,huo ni ukilitimba na hasira za kukosa nafasi ya uwakilishi,tunatakiwa kuikemea ili isitokee kwa watawala wengine

mapinduziii daimaaaaa
 
Ni haki yake ya msingi kuchukua vifaa vyake binafsi!lakini, angefanya ustaarabu kwa kutotoa vitasa kwa kuwa hivi ni vitu vidogo sana havitamsaidia lolote zaidi ya kujiaibisha mbele ya jamii!
 
Back
Top Bottom