Masha atoweka na samani za ofisi ikiwemo picha ya rais!

Masha atoweka na samani za ofisi ikiwemo picha ya rais!

Duh jamani hawa jamaa wanaongea mno na vyombo vya habari. Sasa kama issue ndogondogo hivi zinashindwa kumalizwa kimya kimya, je complex issues itakuwaje?

Does not matter Kaka issue ndogo, kubwa zote inabidi ziongelewe na kufuatiliwa na wananchi kufahamishwa, vyombo vya habari vyenyewe ndio kama vitaona issue ni ndogo, na kuna kubwa nyingine za kutangaza basi vitafanya hivyo. Nothing is too small when it involves my Kodi... Eti kanunua kwa pesa zake mwenyewe? kwani alikuwa hapewi posho za mambo kama haya... ? Je na hiyo posho haikutoka kwenye Kodi yangu? this is BS
 
Masha anajaribu kutuonyesha ile "jeuri" yake ambayo ndio iliyomuondoa madarakani! Wakati Masha anakabidhiwa ofisi hiyo, ilikuwa na vitasa, pamoja na samani (furniture). Kwa mtazamo wake, vitu hivyo havikuwa na "hadhi" yake akaamua kuvibadilisha na kuweka vyake binafsi. Kama lengo lake lilikuwa ni kuvichukua vitu vyake mara amalizapo muda wake wa uongozi basi alikuwa anawajibika kuvitunza vile vitu alivyovikuta ambavyo ni mali ya ofisi.

Na kwa binadamu mstaarabu, wakati unachukua vitu vyako unawajibika pia kuvirudishia vile ulivyovikuta, maana hakuna mtu aliyekutuma kuviondoa! Sasa kuacha milango bila vitasa, je yeye alikuta hiyo milango ikiwa hivyo?

Tunapozungumzia viongozi wetu kukosa ustaarabu ni kwasababu ya mambo madogo kama haya, na kama yale mengine ya mgombea ubunge kumpiga mkuu wa polisi wa wilaya!! Na ndio maana sishangai wanapong'ang'aniza waitwe "waheshimiwa" maana kwenye maisha ya kawaida mtu kama huyu hakuna atakayemuita muheshimiwa.

1214116275_salha_masha.jpg
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, samani na nyaraka muhimu zilizokuwa katika ofisi ya mbunge wa Nyamagana, jijini Mwanza, ikiwemo picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete, 'zimetoweka'.

Kutoweka kwa samani hizo zilizogharimu fedha nyingi kutoka ofisi ya Bunge kulibainika jana baada ya mbunge mpya wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (CHADEMA), kuingia rasmi kwa ajili ya kuanza kazi.

Alisema, samani hizo zimeibwa katika kipindi cha siku mbili za hivi karibuni kwa kuwa aliwahi kufika kwenye ofisi hizo na kuzikuta baada ya kutoka bungeni.

“Niliwabana viongozi ngazi ya wilaya na mkoa wanieleze vimeenda wapi hivi vitu… niliambiwa eti vilinunuliwa na mtu binafsi na havikuwa mali ya serikali,” alisema mbunge huyo.

“…Ofisi ya mbunge ni mali ya umma kama ilivyo Ikulu (Ofisi ya Rais), fedha za walipakodi zinatumika kugharamia; sasa hivi vitu nani kaviiba?” alihoji Wenje kwa masikitiko.

Aibu! Aibu!

Kama Masha kazitoa alipewa agizo na nani?

Tutaona mengi.
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, samani na nyaraka muhimu zilizokuwa katika ofisi ya mbunge wa Nyamagana, jijini Mwanza, ikiwemo picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete, 'zimetoweka'.

Kutoweka kwa samani hizo zilizogharimu fedha nyingi kutoka ofisi ya Bunge kulibainika jana baada ya mbunge mpya wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (CHADEMA), kuingia rasmi kwa ajili ya kuanza kazi.

Alisema, samani hizo zimeibwa katika kipindi cha siku mbili za hivi karibuni kwa kuwa aliwahi kufika kwenye ofisi hizo na kuzikuta baada ya kutoka bungeni.

"Niliwabana viongozi ngazi ya wilaya na mkoa wanieleze vimeenda wapi hivi vitu… niliambiwa eti vilinunuliwa na mtu binafsi na havikuwa mali ya serikali," alisema mbunge huyo.

"…Ofisi ya mbunge ni mali ya umma kama ilivyo Ikulu (Ofisi ya Rais), fedha za walipakodi zinatumika kugharamia; sasa hivi vitu nani kaviiba?" alihoji Wenje kwa masikitiko.
kama kafanya ivo basi atakuwa na ROHO YA KIMASKINI SANA!!
 
Kwa waliosoma ile tamthilia ya 'Song of Lawino' mwandishi alisisitiza sana from time to time "The Pumpkin of the old homestead must not be aprooted", akimaanisha ukihama makazi, sio lazima ungoe mpaka maboga ambayo kwa kuyang'oa yatakufa na hatakufaidia chochote huko uendako kwenye makazi mapya.
Samahani natoka nje ya mada kidogo..... Nadhani hapa Okot p'Bitek alimaanisha usiache mbachao kwa msala upitao
 
Halafu huyu DAS anajibu as if ni kitu kirahisi mno...hajui kuwa ni dhamana yake ndiyo iko matatani?
 
Nyambala, kwa vile amevinunua kwa fedha zake za mfukoni, basi anavyo haki navyo maana ni jasho lake, lakini hili la kufikia kungoa hadi vitasa, ni umasikini wa roho. Hapa anatuaibisha Wasukuma, ni kabila la watu ambao ni matajiri sana wa roho, hatuna roho za kimasikini na ile roho ya kwanini.

Kwa waliosoma ile tamthilia ya 'Song of Lawino' mwandishi alisisitiza sana from time to time "The Pumpkin of the old homestead must not be aprooted", akimaanisha ukihama makazi, sio lazima ungoe mpaka maboga ambayo kwa kuyang'oa yatakufa na hatakufaidia chochote huko uendako kwenye makazi mapya.

Lets give Mh.Masha the benefits of doubt kuwa hali yake ya kiuchumi ni mbaya sana kwa sasa, hivyo amekosa fedha za kununulia kitasa kwenye makazi yake, na kwa vile kitasa kile alikinunua yeye kwa fedha yake, bora akaking'oe na kukipachika kwake, sambamba na lile zulia, then he is right.

Mkuu Pasco Hapana, hapa Lau Masha amejidhalilisha na anastahili kuchukuliwa Hatua

1: Ni aibu kwa mtu wa Calibre ya Masha kung'oa Vitasa vya Milango, kwangu mimi kung'oa kitasa cha mlango hakutofautiani na Kuvunja Mlango, huo ni Ujambazi na namshauri aliyeleta hii mada angeandika Heading "Masha avamia na Kuvunja Ofisi ya Mbunge"

2: Naamini kabisa katika hiyo Computer "Ya Masha" alikuwa anatumia kuandika mipango mbalimbali ya Maendeleo kwenye Wizara yake na Kwenye Jimbo lake Pia, sasa unapoondoka na Computer ambayo ilikuwa inahifadhi mambo ya Serikali na wananchi maana wewe ni "Mwizi" tu hapo Masha anastahili kunyang'anywa hiyo Computer na Kukabidhi taarifa zote kwa Mbunge Mpya.

Hili ni Tatizo sehemu nyingi sana watu wanashindwa kutofautisha kati ya Shughuli binafsi na za Ofisi unakuta mtu amepewa computer na ofisi haitumii anatumia ya kwake matokeo yake siku anaondoka taarifa zote zinapotea na anayekuja kwenye nafasi yake anaanza upya
 
Aaaah...! masha amefanya mambo ya kitoto kwa level aliofika angetakiwa hata kama amenunua kwa fedha yake aviache maana yy alibenefit na allowance ngapi za serikali.
 
yaani hiyo ndiyo benefits of the doubt?
Yes Mzee Mwanakijiji, tumpe nafasi ya kunufaika na mashaka yetu kuwa vitasa ni vyake, alikuwa na shida navyo, akaving'oa kuvichukua kwa matumizi yake.

Hii benefit of doubt inatumika sana mahakamani wakati wa kuestablish mensrea dhidi ya actus reus ya dhamira ya mtenda tendo tendo kabla hatatenda tendo husika. Hivyo tuasume Masha ameyatenda hayo in good faith, kuichukua kitasa chake alichokinunua ili akakitumie.
 
kushindwa si mchezo inahitaji moyo,ukizingatia mtu mwenyewe ni mtu wa matanuzi,
 
What next... Je atavunja kile kituo cha polisi na ile shule ambayo allegedly alivianzisha
 
Wana Jf, wasiwasi wangu kama alikuwa anaishi kwenye zile nyumba za serikali kwa mawaziri inawezekana aka sepa na fenicha za ndani vilevile. Kama amekuwa na wivu kwa mbunge anayemwachia atashindwaje kwa waziri ajaye kiofisi na makazi.
 
Samahani natoka nje ya mada kidogo..... Nadhani hapa Okot p'Bitek alimaanisha usiache mbachao kwa msala upitao
VoiceOfReason, kwanza asante kunikumbusha jina la mwandishi Okot p'Bitek wa Song of Lawino, naamini nawe ni msomi wa litarate, huwa kwenye andiko kuna direct meaning na hidden meaning, mbona hii iko too diect kwamba ukiahama, using'oe maboga maana yatakufa, lakini ukiyaacha yataishi na siku ukipita, utaendelea kula maboga yako. Kwenye context hii, mimi naamini Mhe.Masha sio wa mtu wa shida kihivyo na hicho kitasa hadi kuking'oa, na siamini kuwa anaenda kukitumia, sana sana kukitupa tuu jalalani ili kumkomea ajaye naye aweke mwake, huu ni umimi tuu!.

Usiacha mbachao kwa msala upitao, ni usiache kitu ulichozoe kwa ajili ya jambo la msimu tuu la kuja na kupita, kama 'usidharau dafu, embe tunda la msimu'.
 
Mkuu Pasco Hapana, hapa Lau Masha amejidhalilisha na anastahili kuchukuliwa Hatua

2: Naamini kabisa katika hiyo Computer "Ya Masha" alikuwa anatumia kuandika mipango mbalimbali ya Maendeleo kwenye Wizara yake na Kwenye Jimbo lake Pia, sasa unapoondoka na Computer ambayo ilikuwa inahifadhi mambo ya Serikali na wananchi maana wewe ni "Mwizi" tu hapo Masha anastahili kunyang'anywa hiyo Computer na Kukabidhi taarifa zote kwa Mbunge Mpya.

Hili ni Tatizo sehemu nyingi sana watu wanashindwa kutofautisha kati ya Shughuli binafsi na za Ofisi unakuta mtu amepewa computer na ofisi haitumii anatumia ya kwake matokeo yake siku anaondoka taarifa zote zinapotea na anayekuja kwenye nafasi yake anaanza upya
Dk. Ndege ya Uchumi, kwa computer namuelewa na jamii youte inamuelewa, computer ni pc, ina mambo yake mengi personal. Serikali yatu bado inafanya shughuli zake zote kwa madokeza ya kwenye karatasi, hivyo kila kitu kipo sawa. Tatizo langu ni kung'oa fixed items.
 
Masha ang'oa vitasa ofisi ya Mbunge Mwanza

Send to a friend Tuesday, 30 November 2010 01:46 0diggsdigg

masha%203.jpg

Frederick Katulanda, Mwanza

ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, amehamisha vifaa mbalimbali vya ofisi ya Bunge Jimbo la Nyamagana, kwa madai kuwa alivinunua mwenyewe kipindi uongozi wake. Akizungumza na Mwananchi jana, Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje, alisema baada ya kutoka Bungeni alikwenda kuingia katika ofisi hiyo, lakini baada ya kukabidhiwa alikuta vitasa vya mlango, simu ya mezani picha ya Rais na samani za kukalia vikiwa zimechukuliwa.

Kwa mujibu wa Wanje, baada ya kufuatilia aliambiwa kuwa vifaa hivyo viliondolewa na Masha kwa madai kwamba, alivinunua kwa fedha zake mwenyewe.

"Nimefuatilia kwa DAS (Katibu Tawala wa Wilaya) nikaambiwa amechukua Masha, nikafuatilia kwa Katibu Tawala wa Mkoa yeye alijibu kuwa naye alifuatilia suala hilo kupitia kwa Das na kupewaa majibu kama yangu, sasa sijajua ni kwa nini, ninavyojua ofisi haipaswi kukosa samani kwa vile kuna fedha za kununulia vitu hivyo," alisema.

Kwa Upande wake, Masha alikiri kuondoka na vitu hivyo na kwamba, asingeweza kuacha vifaa vyake binafsi katika ofisi hiyo.

Masha alisema vifaa alivyoondoka navyo ni vile tu ambavyo ni mali yake.

"Wakati naingia hapa nilikuta ofisi ikiwa na kiti kimoja na meza tu, vifaa vingine niliweka vyangu, kama kompyuta na meza zake, simu na samani nyingine kulingana na mahitaji yangu," alisema Masha.
Alisema Wenje anapaswa kuwasiliana na ofisi ya mkuu wa wilaya, ili kupewa vifaa vya ofisi hiyo ambavyo yeye aliviondoa alikuwa havitumii kwa vile wao wanajua vilipo.

"Jamani vifaa vya ofisi anapaswa kuuliza ofisi ya mkuu wa wilaya, sasa kama anataka nimwachia na vyangu binafsi, mie nimetoa vyangu…hivyo vya ofisi vipo, nadhani amefika na kukutana na kiti kimoja na meza vile vingine vilivyokuwemo pia vilikuwa mali ya ofisi," alieleza Masha.

Hata hivyo, Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza (RAS), Doroth Mwanyika, hakuweza kupatikana kuzungumzia suala hilo kutokana na kuwa nje ya ofisi, lakini ofisa mmoja wa ofisi yake alithibitisha kuwepo kwa malalamiko ya Wenje na kwamba, yalikuwa yakishughulikiwa

Hii inaonyesha jinsi huyu Mzinza alivyo Mbinafi sana.
 
Duh jamani hawa jamaa wanaongea mno na vyombo vya habari. Sasa kama issue ndogondogo hivi zinashindwa kumalizwa kimya kimya, je complex issues itakuwaje?

Iwapo hili lisielezewe au kujulikana katika vyombo vya habari; sijui ni lipi linalofaa kuwa....Hizi tabia za kunyamazisha watu pale kunapo kero na kebehi ndiyo kunako pelekea Taifa letu kuendelea kudidimia... Btw, while at it, you can advise your 'honourable' friend to apply for gagging order!!!

Nyambala, kwa vile amevinunua kwa fedha zake za mfukoni, basi anavyo haki navyo maana ni jasho lake, lakini hili la kufikia kungoa hadi vitasa, ni umasikini wa roho. Hapa anatuaibisha Wasukuma, ni kabila la watu ambao ni matajiri sana wa roho, hatuna roho za kimasikini na ile roho ya kwanini.

Kwa waliosoma ile tamthilia ya 'Song of Lawino' mwandishi alisisitiza sana from time to time "The Pumpkin of the old homestead must not be aprooted", akimaanisha ukihama makazi, sio lazima ungoe mpaka maboga ambayo kwa kuyang'oa yatakufa na hatakufaidia chochote huko uendako kwenye makazi mapya.

Lets give Mh.Masha the benefits of doubt kuwa hali yake ya kiuchumi ni mbaya sana kwa sasa, hivyo amekosa fedha za kununulia kitasa kwenye makazi yake, na kwa vile kitasa kile alikinunua yeye kwa fedha yake, bora akaking'oe na kukipachika kwake, sambamba na lile zulia, then he is right.
Swali ni kwamba: Kitasa kilichokuwepo mwanzoni alikipeleka wapi? Kilikuwa kimeharibika? Kwanini aliking'oa? Bado anacho? Iwapo kilikuwa kimeharibika kwanini hakutumia fungu la matengenezo kununua kingine na badala yake akatumia pesa yake ya mfukoni?

Hiki ni kielelezo mojawapo cha ukiukwaji wa sheria na taratibu za manunuzi ya samani maofisini. Ofisi za serikali zinafanywa mali binafsi. Kiongozi anayepangiwa kutumia chombo cha umma kwa mhula wa miaka mitano anageuza chombo hicho mali binafsi na kuwa chake daima. Je, kila anayeingia au kuchaguliwa akifanya hivi tutafika wapi??
 
"YEYE AONAYE HASIRA UPESI, ATATENDA KWA UJINGA; NA MTU MWENYE HILA MBAYA HUZIRWA" - Mithali 14:17

yaani kubwaga UBUNGE, UWAZIRI ndio anafanya vitu kama mwendawazimu vile?????? jamani mwacheni tu - asije mwisho akajinyonga .....tayari ameathirika kiakili - MASHA - JIKAZE TU NDIO MAISHA - MILIMA NA MABONDE HAYO......................
 
Back
Top Bottom