Masha atoweka na samani za ofisi ikiwemo picha ya rais! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Masha atoweka na samani za ofisi ikiwemo picha ya rais!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Nov 30, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Nov 30, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Katika hali isiyokuwa ya kawaida, samani na nyaraka muhimu zilizokuwa katika ofisi ya mbunge wa Nyamagana, jijini Mwanza, ikiwemo picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete, 'zimetoweka'.

  Kutoweka kwa samani hizo zilizogharimu fedha nyingi kutoka ofisi ya Bunge kulibainika jana baada ya mbunge mpya wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (CHADEMA), kuingia rasmi kwa ajili ya kuanza kazi.

  Alisema, samani hizo zimeibwa katika kipindi cha siku mbili za hivi karibuni kwa kuwa aliwahi kufika kwenye ofisi hizo na kuzikuta baada ya kutoka bungeni.

  "Niliwabana viongozi ngazi ya wilaya na mkoa wanieleze vimeenda wapi hivi vitu… niliambiwa eti vilinunuliwa na mtu binafsi na havikuwa mali ya serikali," alisema mbunge huyo.

  "…Ofisi ya mbunge ni mali ya umma kama ilivyo Ikulu (Ofisi ya Rais), fedha za walipakodi zinatumika kugharamia; sasa hivi vitu nani kaviiba?" alihoji Wenje kwa masikitiko.
   
 2. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #2
  Nov 30, 2010
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Labda alitumia kasma yake si ya 'sirikali'. Nunua vingine nawe ukifika muda ukapigwa chini unasomba mazagazaga yako na kutokomea!
   
 3. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #3
  Nov 30, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Masha ang'oa vitasa ofisi ya Mbunge Mwanza


  Send to a friend Tuesday, 30 November 2010 01:46 0diggsdigg

  [​IMG]

  Frederick Katulanda, Mwanza

  ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, amehamisha vifaa mbalimbali vya ofisi ya Bunge Jimbo la Nyamagana, kwa madai kuwa alivinunua mwenyewe kipindi uongozi wake. Akizungumza na Mwananchi jana, Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje, alisema baada ya kutoka Bungeni alikwenda kuingia katika ofisi hiyo, lakini baada ya kukabidhiwa alikuta vitasa vya mlango, simu ya mezani picha ya Rais na samani za kukalia vikiwa zimechukuliwa.

  Kwa mujibu wa Wanje, baada ya kufuatilia aliambiwa kuwa vifaa hivyo viliondolewa na Masha kwa madai kwamba, alivinunua kwa fedha zake mwenyewe.

  "Nimefuatilia kwa DAS (Katibu Tawala wa Wilaya) nikaambiwa amechukua Masha, nikafuatilia kwa Katibu Tawala wa Mkoa yeye alijibu kuwa naye alifuatilia suala hilo kupitia kwa Das na kupewaa majibu kama yangu, sasa sijajua ni kwa nini, ninavyojua ofisi haipaswi kukosa samani kwa vile kuna fedha za kununulia vitu hivyo," alisema.

  Kwa Upande wake, Masha alikiri kuondoka na vitu hivyo na kwamba, asingeweza kuacha vifaa vyake binafsi katika ofisi hiyo.

  Masha alisema vifaa alivyoondoka navyo ni vile tu ambavyo ni mali yake.

  "Wakati naingia hapa nilikuta ofisi ikiwa na kiti kimoja na meza tu, vifaa vingine niliweka vyangu, kama kompyuta na meza zake, simu na samani nyingine kulingana na mahitaji yangu," alisema Masha.
  Alisema Wenje anapaswa kuwasiliana na ofisi ya mkuu wa wilaya, ili kupewa vifaa vya ofisi hiyo ambavyo yeye aliviondoa alikuwa havitumii kwa vile wao wanajua vilipo.

  "Jamani vifaa vya ofisi anapaswa kuuliza ofisi ya mkuu wa wilaya, sasa kama anataka nimwachia na vyangu binafsi, mie nimetoa vyangu…hivyo vya ofisi vipo, nadhani amefika na kukutana na kiti kimoja na meza vile vingine vilivyokuwemo pia vilikuwa mali ya ofisi," alieleza Masha.

  Hata hivyo, Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza (RAS), Doroth Mwanyika, hakuweza kupatikana kuzungumzia suala hilo kutokana na kuwa nje ya ofisi, lakini ofisa mmoja wa ofisi yake alithibitisha kuwepo kwa malalamiko ya Wenje na kwamba, yalikuwa yakishughulikiwa
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Nov 30, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Draaaaama
   
 5. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #5
  Nov 30, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Duh jamani hawa jamaa wanaongea mno na vyombo vya habari. Sasa kama issue ndogondogo hivi zinashindwa kumalizwa kimya kimya, je complex issues itakuwaje?
   
 6. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #6
  Nov 30, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  La hila lahilalaa waradhimu............
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  Nov 30, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Sometimes huwa najikuta naanza kuamini ule usemi unaoupenda miafrika.........
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  Nov 30, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Hiyo kauli mbiu ina ukweli na nadhani wengi ukweli wake wanaukubali kimoyomoyo......
   
 9. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #9
  Nov 30, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Just imagine, of all the things! hata kitasa, zulia (used) du? And this is the guy we were told have all the credentials to make things happen like neva before!!! Ndiyo maana watu humu wanapoimba imba humu Januari, Januari I completely dobt if he's an exception.
   
 10. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #10
  Nov 30, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Holly Molly!! gvhs vhpof;!! what a greedy living creature!:frog:
   
 11. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #11
  Nov 30, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hivi ile ofisi ya mzee six ya Sikonge siku akiamua kuondoka na samani zote nani ataulizwa
   
 12. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #12
  Nov 30, 2010
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Masha aache utoto,ina maana muda wote aliokuwa mbunge alikuwa halipwi posho?? .Hadi vitasa !!!! :teeth: ??
  Eti huyo ndiye alikuwa waziri wa Mambo ya Ndani lol !! aibu kwa Serikali ya KJ
   
 13. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #13
  Nov 30, 2010
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Masha ana wivu "wakike"....!

  NB: kwa akina dada/mama msinitoe roho hiyo ni nahau tu..!
   
 14. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #14
  Nov 30, 2010
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Mwizi hachagui cha kuiba
   
 15. M

  Mutu JF-Expert Member

  #15
  Nov 30, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wewe unadhani kuwa huna haki ya kujua................there is no issue ndogo hapa.
   
 16. M

  Mutu JF-Expert Member

  #16
  Nov 30, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  kweli noma maana haikuwa lazima sana kutoa mpaka kitasa
   
 17. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #17
  Nov 30, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mara nyingi huwa najiuliza akili za mawaziri wetu mtu hadi unaaminiwa kushika wadhifa huo still unakuja kufanya vituko vya kijinga namna hii, naviita vya kijinga kwa sababu kitasa ni sh. ngapi ukilinganisha utu wako, sasa huyu ndiye tuliyemtegemea kushughulikia ID za taifa angetupeleka wapi, bora amepigwa chini.
   
 18. simbaulanga

  simbaulanga Member

  #18
  Nov 30, 2010
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ok, lets say he bought those items from his own pocket, which i dont buy it, does he have any receipts to show where and when were bought and how much was it, and also he has to prove that the money came from his bank account with the bank statement showing the transactions on that particular time. and not from his budget or allowance that he was geting from the government. just a simple proof will do, otheriwse he has to retun them back to the office as part of the office furnitures or get charged for theft
   
 19. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #19
  Nov 30, 2010
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Kweli kusoma sio kuelimika; nadhani cha msingi hapa ni kumfunglia mashtaka kwa kuiba bali ya umma.
   
 20. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #20
  Nov 30, 2010
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Kuiba bali ya umma sio ishu ndogo, kuna watu wamekuwa addicted na wizi.
   
Loading...