Masha atoweka na samani za ofisi ikiwemo picha ya rais!

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, samani na nyaraka muhimu zilizokuwa katika ofisi ya mbunge wa Nyamagana, jijini Mwanza, ikiwemo picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete, 'zimetoweka'.

Kutoweka kwa samani hizo zilizogharimu fedha nyingi
kutoka ofisi ya Bunge kulibainika jana baada ya mbunge mpya wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (CHADEMA), kuingia rasmi kwa ajili ya kuanza kazi.

Alisema, samani hizo zimeibwa katika kipindi cha siku mbili za hivi karibuni kwa kuwa aliwahi kufika kwenye ofisi hizo na kuzikuta baada ya kutoka bungeni.

"Niliwabana viongozi ngazi ya wilaya na mkoa wanieleze vimeenda wapi hivi vitu… niliambiwa eti vilinunuliwa na mtu binafsi na havikuwa mali ya serikali," alisema mbunge huyo.

"…Ofisi ya mbunge ni mali ya umma kama ilivyo Ikulu (Ofisi ya Rais), fedha za walipakodi zinatumika kugharamia; sasa hivi vitu nani kaviiba?" alihoji Wenje kwa masikitiko.

- Wakuu Great Thinkers, chonde chonde jamani naomba kuuliza all this 7 pages ni kwa sababu ya hii habari hapa au kuna nyingine imeondolewa katika hii habari?

- I mean eti ni wapi hapa kwenye hii habari kuna FACTS 100%, kuthibitisha kwamba Mheshimiwa Masha, ameiba hivyo vifaa na vilikuwa ni vifaa vya serikali?


William.
 
Wivu wa Kike ??? Inanikumbusha when Margret Thatcher alipo muonya Norma Major akome kuvaa mkufu wake wa almasi aliopewa zawadi na Oman Sultan .

Sioni ubaya wa masha kung'oa alivyo nunua, utajuaje labda vya bei mbaya , aliwekea wakfu au kutambikiwa na mizimu yake?
 
- Wakuu Great Thinkers, chonde chonde jamani naomba kuuliza all this 7 pages ni kwa sababu ya hii habari hapa au kuna nyingine imeondolewa katika hii habari?

- I mean eti ni wapi hapa kwenye hii habari kuna FACTS 100%, kuthibitisha kwamba Mheshimiwa Masha, ameiba hivyo vifaa na vilikuwa ni vifaa vya serikali?


William.
Wewe unapoletaga habari zako huwa unatupa evidence 100% acha uzushi wako na wewe.
 
Hiyo inadhihirisha maana halisi ya ARI ZAIDI, KASI ZAIDI, NGUVU ZAIDI......
Kibwagizo........... Wizi zaidi, Ufisadi zaidi, Utapeli zaidi, Usanii zaidi...
 
Back
Top Bottom