Ufadhili wa ugaidi, hawa magaidi wote wakubwa duniani, vile vikundi vikubwa vya ugaidi kama HAMAS, HOUTH, HEZBOLAH n.k mfadhili wao mkuu ni Iran.
Sasa wewe jiulize mfano HAMAS walimuulia nini yule Mtanzania? Kijana akawa mpaka anawaomba msamaha analia wasimuue ila wakamuua. Yule kijana ana nini anakijua kuhusu ugomvi wao na Israel hadi wamuuwe.
Yeyote anayefadhili ushenzi kama huu anapaswa kuangamizwa. Sasa Iran anataka amiliki Nuclear, akimiliki Nuclear ni hatari kwa dunia tena sana. Israel yeye hataki Iran amiliki Nuclear sababu Iran alishaapa kuifuta Israel ktk uso wa dunia. So anahakikisha Iran hamiliki hizo silaha.
Wacha kuropoka wewe.
Hamas haijaanzishwa na Iran,Hamas iloanzishwa na hao hao Israel kwaajili ya kuipunguza nguvu PLO.
Pia Hamas kutetea ardhi yao wanakuwaje magaidi!?
Hizbollah haijaanzishwa na Iran,bali ilianzishwa kipindi Cha Beirut crisis 1959 ambapo Israel alichochea civil war ndani ya Lebanon.
Hizbollah kutetea Lebanon wanakuwaje magaidi!?
Houthi haikuanzishwa na Iran,bali ilikuja kuungana na Iran pale ilipotaka msaada wa kuondoa utawala wa Mansour ambaye ni mshirika wa Saudi Arabia na USA ilhali raia 99% wa Yemen hawamtaki.
Iran haikuwahi kuvamia taifa la mtu,ila Israel imewahi kuvamia mataifa kibao na kuanzisha migogoro katika hayo mataifa ikiwemo Syria na Lebanon.
Iran haikuwahi kutaka kumiliki nuclear,ila tangu 1995 Israel wanamuundia espionage Iran kumsingizia kuhusu nuclear.
Hivi ninyi mnatugeuza sisi watoto!?
Mnadhani hatusomi na hatufuatilii mambo!?
Kama USA asingekua anaiingilia masuala ya MIDDLE EAST basi kusingekuwa na vita.
Iraq ya Saddam Hussein walimzushia ana mabomu ya mass destruction,kumbe hana silaha za sumu zozote,wameenda wameua raia wasio na hatia na kuharibu nchi.
Libya wameiharibu hivyo hivyo, Gaddafi aliwakosea nini!??
Aisee tunasoma na tunafuatilia mambo muwache kudanganya watu.
Gaidi mkuu ni USA na Iran.