Marekani: Apigwa risasi baada ya kugonga mlango usio sahihi

Boran Jakutay

Senior Member
Apr 8, 2023
110
255
8d523bed-6026-4726-b3b2-c25dfae39bcf.jpg

Maandamano yalizuka katika Jiji la Kansas, Missouri, mwishoni mwa juma baada ya mwenye nyumba kumpiga risasi mbili kijana mweusi ambaye aligonga kengele ya mlango wao kimakosa.

Ralph Yarl mwenye umri wa miaka 16, alitumwa na wazazi wake kuwachukua kaka zake kutoka katika nyumba ya rafiki yao mnamo tarehe 13 Aprili, lakini akaenda kwa anwani isiyo sahihi.

Mshukiwa alimpiga risasi Bw. Yarl akiwa katika mlango wake.

Kijana huyo alipiga risasi moja kichwani, imesema familia yake na mawakili wao.

Polisi imemwachia huru mtu aliyefyatua risasi kutoka kizuizini lakini hawajawatambua. Bw Yarl aliruhusiwa kutoka hospitalini Jumapili na anaendelea kupata nafuu akiwa nyumbani na familia yake, baba yake Paul Yarl aliliambia gazeti la Kansas City Star.

"Anaendelea kuimarika," baba yake aliliambia gazeti."

Mawakili mashuhuri wa haki za kiraia Ben Crump na Lee Merritt wanawakilisha familia ya Bw Yarl katika kesi hiyo. Waliwakosoa maafisa kwa kumwachilia huru mshukiwa, ambaye wanasema ni mwanaume mzungu.

"Huwezi tu kuwapiga watu risasi bila sababu kisa mtu anapokuja kugonga mlango wako - na kugonga mlango wako sio kosa. Huyu jamaa anapaswa kushtakiwa,"Bw Crump alisema.

CHANZO: BBC

============


Andrew Lester (84) mkazi wa Jimbo la Missouri ameshtakiwa kwa kumjeruhi kwa risasi mbili #RalphYarl (16) ambaye alitumwa na wazazi wake kumuita kaka aliyekuwa kwa rafiki zake lakini akakosea nyumba.

Mtuhumiwa alishikiliwa na Polisi kisha akaachiwa lakini baadhi ya Wananchi waliandamana kushinikiza hatua zichukuliwe wakihusisha tukio hilo na chuki ya ubaguzi wa rangi ndipo Lester akakamatwa tena.

Mastaa wakiwemo Halle Berry, Kerry Washington na Jennifer Hudson wote wametumia kurasa zao za kijamii kuunga mkono Familia ya Yarl.
 
Jamaa mwenyewe aliyempiga dogo ndio huyo hapo kwenye picha kushoto

View attachment 2591680
Yaani nilisoma nikasikitika sana,mimi nyumbani kwangu mara kibao tu watu wamekosea ,mtu anabonyeza kengele ukimuangalia kwenye screen ya camera unamuona hamfahamu,unamuuliza anasema sorry alikosea.Basi anaondoka.Kamwe sijawahi fikiria vibaya.
Nikajiuliza huyu Baba why alipoona mtu hamfahamu akakimbilia kumpiga risasi?Inasikitisha sana.
 
Back
Top Bottom