Kilimanjaro: Kijana apigwa risasi hifadhini, Familia yadai ushahidi unapotezwa

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,614
Utata umeibuka baada ya familia ya mtoto, Ngatipa Parmao(17) anayedaiwa kuuawa kwa risasi na askari wa wanyamapori wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kudai kuna njama zimefanywa kuondoa risasi mwilini kwa mtoto huyo katika hospitali ya awali alikokimbizwa kwa matibabu.

Familia ya mtoto huyo inasema majibu ya uchunguzi wa kitabibu uliofanywa juzi katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) inaonyesha matobo mawili yanayodaiwa ni ya risasi tumboni na mkono wa kulia.

Mtoto huyo ambaye ni wa jamii ya kifugaji ya kimaasai na mkazi wa kijiji cha Pangaroo, Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro alifariki dunia juzi baada ya kudaiwa kupigwa risasi na askari wa wanyamapori katika hifadhi ya Mkomazi Julai 6.

Juzi, Mkuu wa Wilaya hiyo, Abdalah Mwaipaya alikiri kutokea kwa kifo cha mtoto huyo katika hospitali KCMC alikokimbizwa kwa ajili ya matibabu ambapo mpaka sasa Jeshi la polisi linamshikilia askari mmoja kwa kuhusika na tukio hilo.

Hata hivyo Kamanda wa polisi mkoani humo, Simon Maigwa alisema kiutaratibu uchunguzi utakapokamilika jalada la mashtaka litaandaliwa na kupelekwa kwa mwanasheria mkuu wa Serikali.

Akizungumza na Mwananchi kwa niaba ya familia jana akiwa KCMC baada ya uchunguzi wa mwili wa Ngatipa, kaka wa arehemu Daniel Imani aliiomba serikali kuingilia kati sakata hilo ili haki ya mtoto wao ipatikane kutokana na mashaka waliyo nayo.

“Baada ya mdogo wangu kupigwa risasi na askari wanyamapori alikimbizwa hospitali ya wilaya ya Same kutokana na hali yake kuwa mbaya na alifanyiwa upasuaji, chakushangaza wanatuambia hakuna risasi iliyoonekana, hatuna imani na haya majibu,” alisema

“Na mpaka tulipompeleka hospitali ya KCMC na kufariki jana (juzi), mwili umefanyiwa postmoterm na tumboni pamoja na mkono wake wa kulia kuna mashimo ya risasi na hakuna risasi iliyoonekana ila sisi tuna wasiwasi na hospitali ya Same ambapo ndio waliompokea mara ya kwanza,” alisema

Kaka huyo wa marehemu alisema,”sisi tunachoiomba serikali kwasababu mtoto wetu inajulikana amekufa, tunaomba iingilie kati ili wale wote waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria ili hali ya ndugu yetu ipatikane.”

Awali kaka wa marehemu alidai siku ya tukio wakati ndugu yao akiswaga ng’ombe karibu na eneo la mpakani alikutana na askari hao ambao walilazimisha kuingiza ng’ombe hifadhini na alipojaribu kuzuia alipigwa risasi ya tumbo.

Soma Zaidi: Kijana apigwa risasi na Askari wa Hifadhi ya Mkomazi


Chanzo: Mwananchi
 
Pole mno wote walioguswa na kifo of this young man,KATIBA ndio mwarobaini wa issues nyingi ikiwemo hii,wanausalama yeyote anapokua ni suspect, uchunguzi wake utafanywa na IPID sio police tena,because huwezi kujichunguza mwenyewe!

Ndio maana katiba mpya itatupatia TAASISI imara na zenye kujitegemea including hii IPID (hawa ni police within police na watapewa uwezo wa kisheria wa kuchunguza, kufungua docket, to arrest na kumfikisha suspect mahakamani.

Utendaji wao hautaingilia na police, CEO wake ni lazima aombe na afanyiwe interview na kamati ya Bunge ambayo wajumbe wake watatokana na uwiano wa kila chama kilivyoshinda uchaguzi)
 
Hivi mshasikia story za waliowahi kukutana na masai porini au wakilisha mifugo yao shambani kwa watu? Masai no wajeuri sana. Ukute baada ya ng'ombe kukamatwa alileta ujeuri na kuleta fujo ndo hadi nguvu ikatumika.
 
1657532844111.png

Mtoto mwenye umri wa miaka 17 na mkazi wa kijiji cha Pangaroo mkoani Kilimanjaro, Ngatipa Parmao amefariki dunia akidaiwa kupigwa risasi na askari wa wanyamapori katika Hifadhi ya Mkomazi.

Mtoto huyo jamii ya kifugaji ya Kimasai anadaiwa kupigwa risasi hiyo Julai 6 kwa madai ya kuswaga mifugo ndani ya hifadhi hiyo, jambo ambalo ni kinyume cha sheria za hifadhi.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa wilaya hiyo, Abdallah Mwaipaya alikiri kutokea kwa kifo cha mtoto huyo jana katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya kaskazini (KCMC) alikokimbizwa kwa ajili ya matibabu.

Kutokana na tukio hilo, Mwaipaya alisema Jeshi la Polisi mkoani humo linamshikilia askari huyo kwa uchunguzi, ili kujua hasa ni nini kilichotokea na kusema baada ya hapo taratibu nyingine za kisheria zitachukuliwa.

“Ni kweli tukio limetokea na tumepata taarifa za huyu mtoto kuwa amefariki, lakini taarifa za awali ni kwamba waliingiza ng’ombe kwenye hifadhi, wale askari wakakamta zile ng’ombe na baada ya kumkamata huyu mtoto akawa ameita wenzake.

“Wakaja na masime jambo ambalo liliwafanya wale askari warushe risasi angani kama 15 hivi kutokana na kwamba wale wafugaji walikuwa wanawafuata,” alisema.

Alisema kuwa wanamshikilia askari huyo na uchunguzi unaendelea, ili kujua hasa nini kilichotokea.

“Polisi wakishakamilisha uchunguzi wao taratibu nyingine za kisheria zitachukuliwa,” alisema Mwaipaya.

Kamishna msaidizi wa uhifadhi Mkomazi, Emanuel Moirana alisema baada ya askari hao kukamata mifugo iliyokuwa ikiswagwa ndani ya hifadhi hiyo, wananchi waliwavamia askari hao ambao walikuwa ni watano na kwamba wakati wakijihami walirusha risasi angani kwa kuwa wananchi hao walikuwa wamebeba masime.

“Taarifa nilizonazo ni kwamba askari walikamata mifugo ndani ya hifadhi ndipo wananchi walipovamia na askari wakafyatua risasi ndipo ilipompata huyu mtoto kwa bahati mbaya kwenye zile purukushani.

“Kiutaratibu huwa mtu haruhusiwi kuingiza mifugo ndani ya hifadhi, hivyo mifugo ikikamatwa huwa kuna taratibu zinafanywa lakini hawa wananchi wakawa wamewavamia askari,” alisema Moirana.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi, Katibu wa chama cha wafugaji wilayani humo, Peter Martine alidai baada ya askari kukamata mifugo hiyo walimtaka mtoto huyo kukabidhi sime na baada ya kukabidhi askari wale wakataka kuondoka na mifugo ile na ndipo palipotokea tukio hilo.

“Jana ng’ombe walikamatwa wakaondoka na nusu ya ng’ombe waliokuwepo, wakawa wananyang’anyana na mchungi ng’ombe ndani ya hifadhi.

“Hawa askari wakawa wanaongea na mchungaji, baada ya muda kidogo wakamtaka atoe sime lake pamoja na simu, vyote akawa ametoa baada ya muda wale askari wakaswaga ng’ombe kuondoka nazo mchungaji kuwakatalia ndipo wakampiga risasi,” alisema Katibu huyo.

Machi 24 mwaka huu, mkazi wa Kibosho Kundi katika Wilaya ya Moshi, Prosper Munish (48) aliuawa kwa kupigwa risasi na mmoja wa maofisa wa wanyamapori akidhaniwa kuwa ni mbwa wanaozurura mitaani.

Mtuhumiwa wa mauaji hayo alitajwa na polisi kuwa ni Honest Ninja (35).

Mei 17 mwaka 2021 katika Wilaya ya Same, Dainess Josephat mkazi wa kijiji cha Mheza alidaiwa kuuawa na askari wa wanyamapori wakati akienda shambani kwake.
 
Huyo Prosper Munish alipigwa risasi akidhaniwa ni mbwa wanaozurura mtaani???aiseee...this is too much... kwahyo Askari hajui kutofautisha mbwa na binadamu?hawa game reserve wakiwa porini huwa wanajikuta sometimes na wenyewe ni simba
 
Kwa sisi tuliobahatikja kupakana na hifadhi ya mlima Kilimanjaro tunapata kadhia sana. Ni kweli watu hawaruhusiwi kufanya shughuli zozote kwenye hizi hifadhi lakini hata akipatikana mtu kaingia hifadhi kumpiga risasi si sawa. Baada ya kuona wanaume wanaharibu sana basi msituni waliruhusiwa akina mama na hawa askari huwa wanabaka wakina mama, tatizo kuonekana kubwa hata wakinamama hawaruhusiwi tena hata kwenda kuokota kuni msituni.

Kama watu wanaopatikana karibu na hifashi hawawezi hata kufurahia ardhi yao basi haina maana kikubwa kuwe na utaratibu maalumu wa kufuata sheria na ikumbukwe sheria zipo kwa wanaovunja pia. .
 
Mbona taarifa ipo wazi, kosa sio la Askari hapo Kama kweli hao madogo waliwafuata na silaha, inaweza kutokea umeshika bunduki kwenye kurupushani ukamlenga mtu hasa kwa mazingira hayo ambapo uhai wa Askari ulikuwa hatarini
Naongelea tukio la Machi 24 la Moshi kama alivyoandika mwandishi
 
Huyo Prosper Munish alipigwa risasi akidhaniwa ni mbwa wanaozurura mtaani???aiseee...this is too much... kwahyo Askari hajui kutofautisha mbwa na binadamu?hawa game reserve wakiwa porini huwa wanajikuta sometimes na wenyewe ni simba
Nimeshangaa pia, au jamaa alikuwa anatembelea mikono na miguu?
 
Wamemkamata na ameita wenzake na wamekuja na silaha. Kwanini auwawe yeye tu na siyo wenzake?
Mbona taarifa ipo wazi, kosa sio la Askari hapo Kama kweli hao madogo waliwafuata na silaha, inaweza kutokea umeshika bunduki kwenye kurupushani ukamlenga mtu hasa kwa mazingira hayo ambapo uhai wa Askari ulikuwa hatarini
 
Soma habari tena utaelewa. Mwingine kapigwa risasi akidhaniwa ni mbwa.

Mbwa akiingia kwenye hifadhi ya wanyamapori ana madhara mpaka apigwe risasi?

Hawa askari inabidi washitakiwe wanamakosa.

Mbona taarifa ipo wazi, kosa sio la Askari hapo Kama kweli hao madogo waliwafuata na silaha, inaweza kutokea umeshika bunduki kwenye kurupushani ukamlenga mtu hasa kwa mazingira hayo ambapo uhai wa Askari ulikuwa hatarini
 
Hiyo mbuga naijua vzr sana
Nakumbuka nlikuwa naingilia
Kutokea kisiwani
Askari wa huko siyo kabisa wakikugumia

Ova
 
Soma habari tena utaelewa. Mwingine kapigwa risasi akidhaniwa ni mbwa.
Mbwa akiingia kwenye hifadhi ya wanyamapori ana madhara mpaka apigwe risasi?
Hawa askari inabidi washitakiwe wanamakosa
Nimeisoma Tena Mkuu😂,Kuna vitu havieleweki Nchi hii aisee, hasa ukizingatia mbwa Ni mnyama pia so akiingia hifadhini hakuna tatizo.

Huenda hao Askari wanafuza bangi
 
Dar!! Nchi yetu imefikia mahali hata wakoloni hawakutufanyia hivi. Tunafanyiwa unyama namna hii kida uwekezaji? Kuna haja ya kuanza mapambano dhidi ya udharimu huu.
 
Back
Top Bottom