Nyumba ya babu yake Naibu Rais Kamala Harris yatafutwa Zambia

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,328
8,243
Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris ana nia ya kutembelea nyumba ambayo aliwahi kuishi na babu yake miaka ya 1960, jambo ambalo imesababisha msako wa nyumba hiyo kuanza, gazeti la Times la Uingereza linaripoti.

Bi Harris, ambaye yuko katika ziara ya siku tisa katika nchi tatu za Afrika, ana mpango wa kuitembelea Zambia mwishoni mwa juma - ambapo tayari maafisa wakuu 18 wa Marekani wamezuru bara hilo tangu mwezi Januari mwaka huu.

Aliwahi kumtembelea babu yake nchini Zambia wakati akiwa mtoto, babu yake alikuwa mtumishi wa umma wa India ambaye alitumwa huko kusaidia kuwarejesha wakimbizi baada ya taifa hilo kupata uhuru.

Ubalozi wa Marekani mjini Lusaka umenukuliwa na gazeti la The Times ukiomba umma kusaidia kutafuta nyumba hiyo ya zamani ya Bw Gopalan wakati ambao Bi Harris anataka kuhusianisha enzi za utoto wake na nchi hiyo”.

Safari ya Afrika inatarajiwa kuimarisha ushirikiano wa Marekani katika bara zima kuhusu "usalama na ustawi wa kiuchumi", kulingana na taarifa ya ofisi yake.
 
Back
Top Bottom