Mapito mawili magumu kwa wanaume ndani ya ndoa

Mapito mawili magumu kwa wanaume ndani ya ndoa

Utaambiwa huna mbele wala nyuma kama mche wa sabuni🤣🤣🤣🤣 vero kokote ulipo baya lolote likukute.
Mungu anisamehe tuu lakini wanawake ni kuwashe yenta tuu yaani na bora sina hela ningekuwa nazo aloh ningekuwa the best bed to bed midfielder hhapa duniani
Hahahaha🤣🤣🤣🤣
 
Ukweli mchungu ni kwamba Wanaume wengi hawafi kwa ajali wala magonjwa wala vita. Wanaume wengi wanakufa kwa msongo wa mawazo, ukimya, na presha ya maisha.

Mwanaume haambiwi pole, haambiwi utashinda, haambiwi jipumzishe kwanza badala yake, kila mtu anamuangalia kama kiwanda cha miujiza – cha kutoa pesa, upendo, msaada, faraja, na subira bila kuchoka.

Anapoamka asubuhi, anawaza:
“Leo watoto wale nini, Leo watoto watatibiwa vipi, Niwapelekee nini wazazi, Kodi ya nyumba imeisha, umeme umeisha, nina kiatu kimoja nacho kimechakaa

Lakini bado atavaa tabasamu.
Ataandika "good morning" status.
Ataambia watu, “tuko vizuri tunaendelea vizuri "

Hawajui kwamba mwanaume huyu usiku analala kitandani lakini hapati usingizi, akiwaza kesho itakuwaje. Anaota ndoto ambazo hazitimii. Anavuta pumzi nzito lakini hakuna anayemsikiliza. Ataomba ushauri, atadharauliwa. Ataomba msaada, ataambiwa “we si mwanaume wa kweli, jikaze mwanaume, mwanaume ni kupambana.

Na mbaya zaidi...
Wanaume wengi wanajitahidi sana kwa wanawake ambao hata hawathamini wala kutambua mchango wao. Wanatoa kila walichonacho kwa mtu ambaye hayuko tayari hata kumshika mkono wakati anadidimia.

Mwanaume anapokata tamaa, halii. Ananyamaza. Akinyamaza – anaumia. Akiumia sana –anapata msongo wa mawazo, anaanza kufa kidogo kidogo tena anakufa kimya kimya.

Hebu leo hata kama bado mwanaume wako hajafanikiwa, msalimie mwanaume kwa upendo. Muambie unathamini sana juhudi zake na unautambua mchango wake. Mtie moyo, msaidie hata kwa neno. Usingoje afe ndio umwite “shujaa”.

Mwenyekiti nasisitiza tena, Mheshimu sana mwanaume wako, wanaume wanapitia magumu mengi sana katika maisha. Tunaelewana lakini?
View attachment 3445807
Kaka MShana, kwanza shukrani 🙏 huwa unatupatia madini sana.

Hapa nimesoma maneno yakaniingia mpaka ndani. Ni kweli wanaume wengi wanakufa taratibu kwa heartaches na kukosa pa kusemea yale wanayoyapitia.

Huwa nawaangalia watoto wangu wa kiume, najisikia huzuni maana najua mizigo inayowasubiri kuibeba watakapokua watu wazima.

Kama jamii na pia sisi wanawake, kuna haja ya kujirekebisha.
 
tatizo pia wengi hawaishi maisha ya Kikristo, sijawahi kukutana na familia inayoishi Kikristo ikawa na shida kwenye ndoa na kifamilia yao.

hivyo tatizo la tanzagiza ni mila, wengi wanajiita Christian lkn hawaishi Christian life bali wanafwafa mila zao na hapo ndipo mateso yalipo bila ya kumkubali na kuishi Kristo ni tabu na mateso tu …
 
Hapo safii!
Ila akijuwa valangati lake mpaka kwa mjumbe!
Aise nimeshuhudia best akiraruriwa na makucha home nilipowaalika bbq, jamaa alijifanya kumpitisha mke kwenye kiwanja alichomficha miaka, halafu ndio wakaja home, mwanamke baada ya kammweso ka kutosha aligeuka TIGER!
Jamaa alivaa shati jeupe, lote lilijaa damu! A scene I would never forget in my life!
Mkuu hii ime niumiza pia.
 
Boss mimi ilitakiwa nipeleke "mahali" mwezi ulio pita niliwapa taarifa ukweni j4 kwamba j2 nakuja kutoa walicho hitaji

Jibu lao subiri tujiandae hadi week ijayo yaani j2 inayofuata

Nilijikuta nafsi inapata amani ghafla najiskia uhuru

Sijaenda tena na sijui nitakwenda lini
Nili takiwa kumu ambia mama kuhusu uchumba fulani, trust me since niache I don't think about it tena.
 
Kaka MShana, kwanza shukrani 🙏 huwa unatupatia madini sana.

Hapa nimesoma maneno yakaniingia mpaka ndani. Ni kweli wanaume wengi wanakufa taratibu kwa heartaches na kukosa pa kusemea yale wanayoyapitia.

Huwa nawaangalia watoto wangu wa kiume, najisikia huzuni maana najua mizigo inayowasubiri kuibeba watakapokua watu wazima.

Kama jamii na pia sisi wanawake, kuna haja ya kujirekebisha.
Asante Dada nina mifano hai mingi ya kuhuzunisha sana
 
Hiyo namba mbili,ni kiherehere chenu na jeuri ya pesa,tena mnyanyaswe mpaka akili iwakae sawa!
 
Dah Jana tu ndo nimetoka kupeleka barua ya uchumba sehemu na kitangulizi cha mahali..... (True story)
Halafu Leo post ya kwanza nakutana na hii🥺

Mpaka nafsi imekufa ganzi
Tatizo hata uambiwe vipi kuhusu ndoa huwezi amini hadi uingie ushuhudie.
Wewe endelea tu maana huwa hazifanani ya kwako itakuwa bora ya mfano.
 
Wana tabia ya kujihesabia Haki,unakuta kamnyanyasa mkewe kipindi ana hela zikiisha akisemwa kidogo Tu anaona ananyanyaswa!
Wanapenda kujitirisha huruma utafikiri wao ni malaika..!!
Kuchit wao, gubu wao, kuzaa nje wao..!!
Wao wakiguswa kidogo milio mingi..!!

Watulie dawa iwaingie nyambafu..!! 😹
 
Bro kwa afya ya akili nyuzi zingine sio za kufungua kusoma😂😂

Unaweza jikuta umesalitiana na mipango ya mwaka mzima kisa fact za jf
Maana mm mwenyew nimejikuta naanza kufikiria upya kuhusu huyu mwali,,,,, asije kuniua baadae kama madai ya mleta Uzi😃
Kaka bora usome tu mimi kuna vioja hatari kwanza kaniambia hampendi sister wangu na anamchukia
 
Nili takiwa kumu ambia mama kuhusu uchumba fulani, trust me since niache I don't think about it tena.
Daaah mwanangu mimi full vioja acha tu man sema naona nikiandika yote ntakua nimeshindwa kuwa na kifua cha kiume😂
Ila kwaajili ya afya ya akili mimi nimesitisha zoezi rasmi pesa ya mahali ntakula mwenyewe
 
Back
Top Bottom