Mapito mawili magumu kwa wanaume ndani ya ndoa

Preamble: For the sake of humility and a long, healthy life, ni busara ndoa zikaangaliwa kwa pande mbili. Moja as perfect intimacy na mbili as disaster against humanity. Ukipata mwenza sahihi, heaven itahamia chini ya dari lenu. Ukikosea kupata mwenza sahihi hakika kuzimu itawafurahia sana na itajidhihirisha kwenu. Msanii

Nimeipenda sana hiyo nukuu ya Msanii kwenye uzi wake kuhusu ndoa yake... Imetoa majumuisho muhimu sana katika uhalisia wake! Very short and very clear

Sasa huko ndoani kuna haya magumu/ mapito mengine nawili kwa wanaume

1. Ukipitia changamoto cha kipato ajira na kazi.. Mwenza wako anaweza kukuvumilia na kukutia moyo lakini kaa ukijua haitazidi miezi mitatu

Mwanzoni mambo yataanza kwa kificho lakini taratibu yataanza kujiinua na kujiweka wazi zaidi

Zitaanza dharau ndogondogo
Vitafuatia vijembe katikati ya utani
Yatafuatia masimango ya kificho na hatimaye ya wazi
Kisha sasa yatakuja matusi na kashfa za wazi..

Kusemwa bila kosa.. Kuvunjiwa heshima, kunyimwa unyumba, kuitwa najina mabaya nknk..!

2. Ukizeeka hali mwenza wako bado ana nguvu

Umetumia nguvu zako maishani kumhudumia na kuihudumia.. familia ukafanya kila la kumfurahisha na kumliwaza kwa uwezo wako! Sasa umezeeka.. Huna nguvu tena za kuhudumu chumbani wala sebuleni.. Mwenza uliyempenda sana na kumpa kila kitu anakuona sasa wewe ni mzigo usiye na faida tena kwake!

Anaweza kukufanyia mambo ambayo hata shetani mwenyewe akiyaona anakimbia... Wengi wamekufa mapema kutokana na hii changamoto ya pili.

Kuchapiwa
Kusimangwa
Kunyimwa vyakula vyote
Kukashfiwa

Kutohudumiwa nknk .. Ni baadhi tu ya mambo yanayoweza kukutokea uzeeni

Naomba nikatishe mada yangu na kurudia nukuu ya Msanii

For the sake of humility and a long, healthy life, ni busara ndoa zikaangaliwa kwa pande mbili. Moja as perfect intimacy na mbili as disaster against humanity. Ukipata mwenza sahihi, heaven itahamia chini ya dari lenu. Ukikosea kupata mwenza sahihi hakika kuzimu itawafurahia sana na itajidhihirisha kwenu.
Ndoa sio mbaya,ni nzuri mno,tatizo ni binadamu ambao ndio huingia kwenye ndoa
 
Hii umekaa vizuri Sana....Mimi nimekuwa na swali moja pia kwamba hao wanawake wazuri wanaweza kuleta mbingu nyumbani wamelelewaje??? Je! Mwanaume ana mchango gani Kwa binti yake kwenda kuwa mke mzuri kule atakapoenda kuolewa?? Au jukumu la kumshape binti kimtazamo,,kihisia na kijamii ni la mama peke yake??

Nakubali kwamba kukiwa na bond katika familia kuna namna pressure inapungua Kwa mwanaume na ule mzigo WA familia unakuwa haumwelemei mtu mmoja.Na future ya waliotoka kwenye Hii familia unakuwa ni tofauti na waliotoka familia ya visasi,,dharau,,kutoheshimiana na infidelity.
Huwezi kumbadilisha mtu mzima mwenye akili timamu malezi uliyompa utotoni hawaya guarantee ya kumfanya kuja kuwa mke mzuri kuna kipindi atakuwa huru atafanya mambo anayotaka yeye bila wewe kujua na hata ukijua huna cha kumfanya!
 
Baba ana nafasi kubwa sana kumuandaa binti yake kuja kuwa mke bora. Wanawake wengi wanamuangalia mume bora kwa kulinganisha baba zao.

Kwa familia za kawaida hadi za hali ya juu mabinti wengi wanapendelea kuolewa na wanaume wenye tabia kama za baba zao au wenye uelekeo wa kufanana nao mienendo au tabia.
 
Mnawaelezea wanaume kama aina fulani au toleo la watakatifu vile, unataka upendo furaha na amani kutoka kwa mke, je wewe ulitoa hivyo vitu kwake? Ulipokuwa na pesa ulimuonyesha waziwazi kuwa upo nae kibahati mbaya, ulipokuwa na nguvu ulikesha kwa michepuko, ulipigiwa simu hata usiku wa manane ukamuacha na upweke wake, ukiulizwa ulisema wewe ni 'mwanaume', na fimbo juu ulimpiga,,,.....leo sasa umefilisika au umezeeka unataka akuonyeshe upendo na bla bla nyingine nzuri hiyo ni ndoto

Tumieni akili kuishi na wanawake,
 
Wanaume wengi tunabidi tubadili vipaumbele vyetu kwenye maisha ya starehe na furaha. Mfano ukiangalia wanaume wengi sana walio kwenye ndoa sehemu kuu ya starehe yao ni bar wakiwa wenyewe ama na marafiki zao huku mke na watoto wakiwa wamelala nyumbani.

Hapo kuna jambo kubwa sana linapotea katika familia ya hivi, hawa watu ni ngumu kuwa na bond, jiulize kwa kipindi cha miaka hii tano ni lini umetoka out ba familia yako mkafurahi?, linganisha na mara ulizotoka kwenda bar kukaa na washkaji. Alafu tafakari.

Wanawake wengi huwa hata asipokuwa anakuuliza jua anahifadhi hayo mambo anajiapiza na kusema ngoja ufilisike au uishiwe hizo pesa au ustaafu ndio utamkoma, na kweli wanaume wengi hali hizo zikiwapata wanajikuta wapo wenyewe wanaanza kulalamika kutengwa na wake na watoto wao.

Maisha ya familia ni zaidi ya kuwalisha na kuwavisha hao mke na watoto wako, hakikisha ni chini ya 30% ya starehe na muda wa furaha unaufanya mwenyewe au na marafiki ila zaidi ya 70% fanya na familia yako, hautajuta.

Wengi watasema bar ndipo tunapopata ramani za michongo, ila ukikaa na kutafakari vizuri hii sio kweli kwa wengi. Tujitafakari sana wakuu.

Mwisho, wanaume wengi wanaoteseka ndani ya ndoa zao ni wao wamejitakia kwa kiasi kikubwa ama kwa kuoa kwa mihemko, ama kupuuza familia zao ama kwa kuwa wabinafsi ama kwa usaliti kwa kigezo cha urijali na vitu kama hivyo.

Tubadilike wakuu, hatuwezi ishi dunia ya leo kwa mifumo waliyoishi wazee wetu wa 1960s.
Kuna wengi sio wanywaji na wako kwenye stress hzohzo unasemaje
 
Preamble: For the sake of humility and a long, healthy life, ni busara ndoa zikaangaliwa kwa pande mbili. Moja as perfect intimacy na mbili as disaster against humanity. Ukipata mwenza sahihi, heaven itahamia chini ya dari lenu. Ukikosea kupata mwenza sahihi hakika kuzimu itawafurahia sana na itajidhihirisha kwenu. Msanii

Nimeipenda sana hiyo nukuu ya Msanii kwenye uzi wake kuhusu ndoa yake... Imetoa majumuisho muhimu sana katika uhalisia wake! Very short and very clear

Sasa huko ndoani kuna haya magumu/ mapito mengine nawili kwa wanaume

1. Ukipitia changamoto cha kipato ajira na kazi.. Mwenza wako anaweza kukuvumilia na kukutia moyo lakini kaa ukijua haitazidi miezi mitatu

Mwanzoni mambo yataanza kwa kificho lakini taratibu yataanza kujiinua na kujiweka wazi zaidi

Zitaanza dharau ndogondogo
Vitafuatia vijembe katikati ya utani
Yatafuatia masimango ya kificho na hatimaye ya wazi
Kisha sasa yatakuja matusi na kashfa za wazi..

Kusemwa bila kosa.. Kuvunjiwa heshima, kunyimwa unyumba, kuitwa najina mabaya nknk..!

2. Ukizeeka hali mwenza wako bado ana nguvu

Umetumia nguvu zako maishani kumhudumia na kuihudumia.. familia ukafanya kila la kumfurahisha na kumliwaza kwa uwezo wako! Sasa umezeeka.. Huna nguvu tena za kuhudumu chumbani wala sebuleni.. Mwenza uliyempenda sana na kumpa kila kitu anakuona sasa wewe ni mzigo usiye na faida tena kwake!

Anaweza kukufanyia mambo ambayo hata shetani mwenyewe akiyaona anakimbia... Wengi wamekufa mapema kutokana na hii changamoto ya pili.

Kuchapiwa
Kusimangwa
Kunyimwa vyakula vyote
Kukashfiwa

Kutohudumiwa nknk .. Ni baadhi tu ya mambo yanayoweza kukutokea uzeeni

Naomba nikatishe mada yangu na kurudia nukuu ya Msanii

For the sake of humility and a long, healthy life, ni busara ndoa zikaangaliwa kwa pande mbili. Moja as perfect intimacy na mbili as disaster against humanity. Ukipata mwenza sahihi, heaven itahamia chini ya dari lenu. Ukikosea kupata mwenza sahihi hakika kuzimu itawafurahia sana na itajidhihirisha kwenu.
Utaambiwa huna mbele wala nyuma kama mche wa sabuni🤣🤣🤣🤣 vero kokote ulipo baya lolote likukute.
Mungu anisamehe tuu lakini wanawake ni kuwashe yenta tuu yaani na bora sina hela ningekuwa nazo aloh ningekuwa the best bed to bed midfielder hhapa duniani
 
Mnawaelezea wanaume kama aina fulani au toleo la watakatifu vile, unataka upendo furaha na amani kutoka kwa mke, je wewe ulitoa hivyo vitu kwake? Ulipokuwa na pesa ulimuonyesha waziwazi kuwa upo nae kibahati mbaya, ulipokuwa na nguvu ulikesha kwa michepuko, ulipigiwa simu hata usiku wa manane ukamuacha na upweke wake, ukiulizwa ulisema wewe ni 'mwanaume', na fimbo juu ulimpiga,,,.....leo sasa umefilisika au umezeeka unataka akuonyeshe upendo na bla bla nyingine nzuri hiyo ni ndoto

Tumieni akili kuishi na wanawake,
Aise kweli tutumie akili nyingi kuishi na wanawake.
Hapa ni akili ya kitaliban tuu....na akili ya kushenyenta na kuzalisha hakuna ndoa
 
Kama kuna watu kwasasa ndoa zinawatesa basi ni hawa wajeda hasa wenye vyeo. Huku nje utawaona kama wapo imara ila ndan ya nyumba zao wanaishi kama wapo kuzimu.
Hapa mtaan kwetu tayar 2 washazikimbia nyumba zao. Wanawake kwasasa ni kama vile wamejua namna ya kuwakamata hawa jamaa.
 
Huwezi kumbadilisha mtu mzima mwenye akili timamu malezi uliyompa utotoni hawaya guarantee ya kumfanya kuja kuwa mke mzuri kuna kipindi atakuwa huru atafanya mambo anayotaka yeye bila wewe kujua na hata ukijua huna cha kumfanya!
Atakuwa huru Kwa sababu nimekuwa sina bond nae na simfatilii,,Yuko na marafiki toxic namuacha,,sijali anaenda wapi na anarudi saa ngapi,, Sijali yeye kupigiwa simu usiku,,hàpo ndio atakuwa huru na kwenda anavyotaka yeye,,,ila Mimi huwa nazima Moto panapofuka moshi...asipokubali kubadilika ninapoona dalili basi sitoenda mbali kwenye safari...Lakini bado naamini Mtoto WA kike anaweza kustahimili kama Hakuna infidelity katika ndoa akiwa ana background ya malezi mazuri ya wazazi wote.
 
Preamble: For the sake of humility and a long, healthy life, ni busara ndoa zikaangaliwa kwa pande mbili. Moja as perfect intimacy na mbili as disaster against humanity. Ukipata mwenza sahihi, heaven itahamia chini ya dari lenu. Ukikosea kupata mwenza sahihi hakika kuzimu itawafurahia sana na itajidhihirisha kwenu. Msanii

Nimeipenda sana hiyo nukuu ya Msanii kwenye uzi wake kuhusu ndoa yake... Imetoa majumuisho muhimu sana katika uhalisia wake! Very short and very clear

Sasa huko ndoani kuna haya magumu/ mapito mengine nawili kwa wanaume

1. Ukipitia changamoto cha kipato ajira na kazi.. Mwenza wako anaweza kukuvumilia na kukutia moyo lakini kaa ukijua haitazidi miezi mitatu

Mwanzoni mambo yataanza kwa kificho lakini taratibu yataanza kujiinua na kujiweka wazi zaidi

Zitaanza dharau ndogondogo
Vitafuatia vijembe katikati ya utani
Yatafuatia masimango ya kificho na hatimaye ya wazi
Kisha sasa yatakuja matusi na kashfa za wazi..

Kusemwa bila kosa.. Kuvunjiwa heshima, kunyimwa unyumba, kuitwa najina mabaya nknk..!

2. Ukizeeka hali mwenza wako bado ana nguvu

Umetumia nguvu zako maishani kumhudumia na kuihudumia.. familia ukafanya kila la kumfurahisha na kumliwaza kwa uwezo wako! Sasa umezeeka.. Huna nguvu tena za kuhudumu chumbani wala sebuleni.. Mwenza uliyempenda sana na kumpa kila kitu anakuona sasa wewe ni mzigo usiye na faida tena kwake!

Anaweza kukufanyia mambo ambayo hata shetani mwenyewe akiyaona anakimbia... Wengi wamekufa mapema kutokana na hii changamoto ya pili.

Kuchapiwa
Kusimangwa
Kunyimwa vyakula vyote
Kukashfiwa

Kutohudumiwa nknk .. Ni baadhi tu ya mambo yanayoweza kukutokea uzeeni

Naomba nikatishe mada yangu na kurudia nukuu ya Msanii

For the sake of humility and a long, healthy life, ni busara ndoa zikaangaliwa kwa pande mbili. Moja as perfect intimacy na mbili as disaster against humanity. Ukipata mwenza sahihi, heaven itahamia chini ya dari lenu. Ukikosea kupata mwenza sahihi hakika kuzimu itawafurahia sana na itajidhihirisha kwenu.
Nimeandika nimefuta nimeandika nikafuta ila kiukweli Hii ndiyo maana halisi ya kuitwa platinum member we kichwa sana mkuu
 
Atakuwa huru Kwa sababu nimekuwa sina bond nae na simfatilii,,Yuko na marafiki toxic namuacha,,sijali anaenda wapi na anarudi saa ngapi,, Sijali yeye kupigiwa simu usiku,,hàpo ndio atakuwa huru na kwenda anavyotaka yeye,,,ila Mimi huwa nazima Moto panapofuka moshi...asipokubali kubadilika ninapoona dalili basi sitoenda mbali kwenye safari...Lakini bado naamini Mtoto WA kike anaweza kustahimili kama Hakuna infidelity katika ndoa akiwa ana background ya malezi mazuri ya wazazi wote.
Sawa mwenzangu unaishi na mtoto wako wa kike anayesoma chuo ili kutengeneza bond,uendelee kumfuatilia na kumchagulia marafiki!
 
Kuna wengi sio wanywaji na wako kwenye stress hzohzo unasemaje
unywaji ilikuwa ni mfano, ila pia bado kuna ubinafsi mahali na ndipo tunapouponzea. Wanaume wengi wanapuuza sana hisia za familia zao, wakitetereka baadhi wanagundua makosa yao wengine hawagundui wanabaki kulalamika.
 
Mwanaume usijisahau, jikumbuke, jilipe, jiwekee akiba ya kwako, kuwa na backup plan. Nina mjomba wangu mpaka chakula alikuwa anajipia ndani ya nyumba yake mwenyewe. Wakitoka nje wanashikana mikono kabisa, ila ndani ni moto.

Wanawake wengi wanapenda heshima ya kuitwa mke na mama nje, ila ndani hawajibiki kama mke.
 
Back
Top Bottom