Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 374,173
- 866,431
- Thread starter
- #21
Ukweli mchungu ni kwamba Wanaume wengi hawafi kwa ajali wala magonjwa wala vita. Wanaume wengi wanakufa kwa msongo wa mawazo, ukimya, na presha ya maisha.
Mwanaume haambiwi pole, haambiwi utashinda, haambiwi jipumzishe kwanza badala yake, kila mtu anamuangalia kama kiwanda cha miujiza – cha kutoa pesa, upendo, msaada, faraja, na subira bila kuchoka.
Anapoamka asubuhi, anawaza:
“Leo watoto wale nini, Leo watoto watatibiwa vipi, Niwapelekee nini wazazi, Kodi ya nyumba imeisha, umeme umeisha, nina kiatu kimoja nacho kimechakaa
Lakini bado atavaa tabasamu.
Ataandika "good morning" status.
Ataambia watu, “tuko vizuri tunaendelea vizuri "
Hawajui kwamba mwanaume huyu usiku analala kitandani lakini hapati usingizi, akiwaza kesho itakuwaje. Anaota ndoto ambazo hazitimii. Anavuta pumzi nzito lakini hakuna anayemsikiliza. Ataomba ushauri, atadharauliwa. Ataomba msaada, ataambiwa “we si mwanaume wa kweli, jikaze mwanaume, mwanaume ni kupambana.
Na mbaya zaidi...
Wanaume wengi wanajitahidi sana kwa wanawake ambao hata hawathamini wala kutambua mchango wao. Wanatoa kila walichonacho kwa mtu ambaye hayuko tayari hata kumshika mkono wakati anadidimia.
Mwanaume anapokata tamaa, halii. Ananyamaza. Akinyamaza – anaumia. Akiumia sana –anapata msongo wa mawazo, anaanza kufa kidogo kidogo tena anakufa kimya kimya.
Hebu leo hata kama bado mwanaume wako hajafanikiwa, msalimie mwanaume kwa upendo. Muambie unathamini sana juhudi zake na unautambua mchango wake. Mtie moyo, msaidie hata kwa neno. Usingoje afe ndio umwite “shujaa”.
Mwenyekiti nasisitiza tena, Mheshimu sana mwanaume wako, wanaume wanapitia magumu mengi sana katika maisha. Tunaelewana lakini?