Chanzo kikuu cha matatizo yote ya binadamu, shida , dhiki, migogiro na yote yasio leta furaha ni ubinafsi wake na kujipendelea.
Mwanadamu yeye anataka apate hiki na kile kutoka kwa binadamu mwingine pasina kuangalia yeye anatoa nini kwa huyo mwenzake maana nae anahitaji kama lake.
Ujumla wa maisha ya mwanandamu na pengine kila kiumbe chenye nafsi na utashi ni furaha, kila unae muona anatafuta furaha.
Sasa maisha yako yanaweza kuwa magumu sana kwa sababu ya mategemeo ya kupata furaha kwa ambaye nae anatafuta furaha huku akiwa na udhaifu wa kibinadamu wa ubinfsi.
Ni katika hali hio mimi binafsi ninapokaribia mwaka wa kumi wa ndoa ukiachana na zile changamoto za maisha ya binadamu katika utafutaji sijawahi kuhisi kuteseka au kupata usumbufu wa ndoa .
Hii ni kwa vile mimi nikiwa na haja fulani sitahitaji kumsumbua mke anifanyie Bali nafanya mwenyewe, njaa ikiuma chakula hamna napika, nguo chafu nafua mwenyewe, maji hamna naenda kuteka, nyumba chafu nasafisha, vyombo vichafu naosha, kiu inauma nafata mwenyewe, mtoto hajaoga naogesha, mke hajisikii sina napotezea nk nk.
narudia tena , huwezi kupata furaha nje ya wewe kamwe.