Mapadre waanza rasmi kumpigia Magufuli kampeni

Mapadre waanza rasmi kumpigia Magufuli kampeni

Ili suala karibu makanisa yote ya kiroma yametangaza hivyo. Hata dsm makanisa mengi baada ya kuhubiri dini leo wamegeuka kumhubiri magufuli. Wanatuchanganya cc waamini.
 
Nikiwa kama Mkatoliki,siwezi kushawishiwa na Kiongozi wangu wa Kanisa kwamba nimchague fulani na fulani hafai,nitachagua kwa utashi wangu Mungu alionijaalia kwa kusikiliza na kuchambua sera zao na kuchanganya na zangu..haya mambo ya viongozi wa imani kuingilia ingilia siasa kwa matamko yao waamini wenzangu na waTanzania kwa ujumla tusishawishiwe nao siku ya uchaguzi ikifika vote kwa mwenye sera nzuri unaeona atatuletea maendeleo kama taifa.

Wewe akili zako ndogo sana.ukikua utapanua upeo.
 
anayepinga kuwa Magufuli kwa hali tuliyonayo sio chagua sahihi basi
1, ana matatizo ya akili
2,hajui taifa hili linamtaka mtu wa aina gani
3,inawezekana ni mkimbizi humu tz
4, siasa za makundi, vyama,ukabila ndo zinamfanya kipofu
5, miemuko ya siasa inamfanya kupoteza wererdi wa kujua wapi na nani anaweza kutupeleka tunapotaka kwenda,

Hapo ulipofikia inaelekea wewe ndiyo huna akili,mawazo yako hayawezi kuwakilisha watanzania wote,wewe ni kama nani? kielimu, kijamii hadi uone kuwa anayepingana na wewe hana akili?

Msifie,mpigie debe lkn kuna watu wengi tu wanajua kasoro zake na makosa yake na udhaifu wake.

Maana hata kupitishwa kwake si kwa kuwa alikuwa bora sana bali ni matokea ya Siasa za makundi, visasi na rushwa katika CCM. Waache watu wamchambue, waone ubora na udhaifu wake ili waje na chaguo bora.

Mkapa wakati anaingia aliitwa Mr Clean akaishia kufanya biashara akiwa ikulu, kujimilikisha mgodi wa Kiwira na kujiuzia Nyumba za serikali akiwa na Magufuli wako.

Kikwete aliitwa chaguo la Mungu watu wakimpamba na kumshabikia kwamba anakuja na tumaini jipya,badala yake watu wanaombea ataondoka lini, sasa wewe na mihemko yako sijui umeanza kufuatilia Siasa karibuni unakurupuka kutuletea hadithi zile zile,si si tuna akili timamu ukiumwa na nyoka ukiona ujiti lazima ushituke muda wa majaribio ya ma CCM umeisha,ukimpenda sana kanywe nae chai
 
Amenikera sana. Namfahamu Fr Mbano. Hawa wanasumbuliwa na tatizo la kumpata rais anayetoka kwenye kanisa lao. Ndio maana wakati mwingine naona waislamu wapo sahihi sana kuhubiri siasa misikitini kuwa tumchague mwenzetu. Huyu anahubiri kwenye kanisa kubwa kama lile lililopo katikati ya mji wakati anajua linakusanya watu wengi sana. Mahubiri haya yatamsumbua sana huyu kasisi. Kwanza anatuhuma za kuombea watu kwa nguvu za giza huyu padre. Anajifanya anponya wakati ameshakutwa kwa mganga wa kienyeji.
 
kelao

Kama ni kweli huyo Padre kahubiri hayo Kanisani, basi amepotoka - mapenzi yake binafsi kwa Magufuli hapaswi kuyatolea hadharani kwenye Mimbari! Kama yeye anaona kuwa Magufuli anatosha, ni swala lake mwenyewe binafsi - aache waumini wake nao watumie uhuru wao kumpima kama anatosha kadiri ya mizania zao!
 
Last edited by a moderator:
Jaman waungwana nawaomben ushaul wenu ninamke wangu nampenda sana ila sasa tatizo kikojoziiiiii!
 
sio wote wapo wengine kama huyu padre wenye jicho la pekee na kutusaidia sisi tunaoendekeza miemuko ya siasa chafu na kupoteza weredi wa kujua kiongozi bora,
Tatizo la mapdre hawa ni wao kujiona wamesoma na wanajua zaidi kuliko sisi waamini wao!! Hili ndilo kosa kubwa wanalofanya. Humo kanisani kuna watu wengi tu tena sana wanaowazidi Elimu na uelewa, kinachotupeleka pale ni kutimiza imani yetu lakini si kutulisha mambo ambayo hayakutupeleka pale, kama wanataka kuzungumza siasa wasubiri mikutano ya hadhara nao watoe yao ya moyoni na kanisani au msikitini ambako kila mtu ana chama chake. Wakiendekeza mambo haya kuelekea uchaguzi mkuu sadaka zitapungu
 
Je yule aliye acha upadri na kukimbilia tamaa ya Mwili?

na huyu makufuli aliyeachanisha ndoa ya dada kabula na yeye kumfamfanya dada kabula kuwa small house yake na huku aliminya mradi barabara yaani kaiba halafu akajenga kebbys hotel bamaga na kummilikisha dada kabula pamoja na viwanja vitatu vya serikali ❕❕ makufuli Ni mwizi mkubwa na malaya aliyejivika ngozi ya kondoo❕❕
 
Siasa ni vurugu mechi hasa wakizivamia mahayawani.

Pengo aliposema viongozi wa dini hawana mamlaka ya kuwaamulia waumini wao juu ya kupiga kura ya NDIO/HAPANA kwa katiba pendekezwa alitukanwa na Gwajima na woote mkamuunga mkono Gwajima eti Viongozi wa dini wanapaswa kuwaongoza waumini wao hasa kwenye mambo yanayohusu mstakabali wao.(au mmesahau?)

Nashangaa hamueleweki hata mnachokisimamia au kwa kuwa hajamtaja mnayemshabikia?

Msipende kusikia mnachokitaka tu hii ndiyo demokrasia.
 
kelao

Leo nimesali hapa parokia ya makuburi ubungo padre amemponda sana lowasa mojakwamoja hamna shaka sasa ni maelekezo kutoka kwa maaskofu kumsaport magufuli.
nimekasirika sana mpaka nimetoka kanisani kwa hasira kabla misa haijaisha
 
Last edited by a moderator:
Siasa ni vurugu mechi hasa wakizivamia mahayawani.

Pengo aliposema viongozi wa dini hawana mamlaka ya kuwaamulia waumini wao juu ya kupiga kura ya NDIO/HAPANA kwa katiba pendekezwa alitukanwa na Gwajima na woote mkamuunga mkono Gwajima eti Viongozi wa dini wanapaswa kuwaongoza waumini wao hasa kwenye mambo yanayohusu mstakabali wao.(au mmesahau?)

Nashangaa hamueleweki hata mnachokisimamia au kwa kuwa hajamtaja mnayemshabikia?

Msipende kusikia mnachokitaka tu hii ndiyo demokrasia.
Bavicha huwa wasahalifu kabisa...
 
mwisho wa siku watamlaani na kumuapiza.

sitoshangaa na wala halinishangazi
 
Wewe mtoa mada ndo mchawi,kama kimetokea kwako nyumbani wewe na mkeo,munayaongea nae padre wenu mnamfuata mnamtonya Usirudie hivi na hivi. Hata wewe ukikosana na mkeo unaongea nae taratibu na mnapata suluhisho sasa wewe unamwaga mtama kwenye kuku na hatujui kama ni ukweli.Watu kama nyie msio na common sense ni hatari sana katika jamii.Heri kufungiwa jiwe na kutupwa baharini.

Haya kayasema hadharani mkuu, tena mbele ya waamini wasio pungua elfu moja.. Ni ktk kanisa kuu la mt. mathias mulumba kalemba Songea Mjini.. Mapema leo asubuhi.
 
Haya kayasema hadharani mkuu, tena mbele ya waamini wasio pungua elfu moja.. Ni ktk kanisa kuu la mt. mathias mulumba kalemba Songea Mjini.. Mapema leo asubuhi.

Sasa kama kayasema kwa elf moja, yeye asingeweka nani angejua. Heri elf moja kuliko mtandaoni. Yeye tu ndo kaweka,
 
Katika kile kinachoonyesha viongozi wa dini kuingilia mambo ya siasa, padre Mbano akihubiri ktk Ibada ya leo j2 kwenye Kanisa kuu Katoliki Songea Mjini amesema ujio wa Magufuli ndio jembe haswa lililokuwa linasubiriwa.

Akaendelea kusema kuwa anawaomba radhi wapinzani safari hii waachane na urais wamwachie Magufuli aweke mambo sawa. kaendelea kusema, 'wapinzani tutawapa ubunge, lkn urais Magufuli anatosha' hapa kulikuwa na minong'ono kanisani. Najiuliza ni mapadre hawa hawa na maaskofu mwaka 2005 walisema JK ni chaguo la Mungu lkn sote ni mashahidi wa kilichotokea. Kwa nini wasiwaachie wananchi waamue wenyewe?

Kwa ushawishi walio nao mapadre kwa waumini wao wapinzani wasipokemea haya basi wasahau urais 2015. Pia hawa mapadre wana elimu kubwa sana lkn wanashindwa kutambua kuwa wale waumini wanaowahubiria kuwa ni wafuasi wa vyama mbali mbali..


kulitenganisha kanisa katoliki na dr. magufuli ni sawa na kumtenganisha mama na mtoto wake wa kumzaa mwenyewe. kitu ambacho hakiwezekani. tuvumiliane tu kwa sasa!
 
Mkuu@kelao usemalo nikweli Mimi naabudu KKKT kimara namuheshimu sana Mchungaji wangu bt nasikitika aneleta HISIA zake kwamba MAGUFULI atafaa hii naichukia sana Km unavyojua viongoz wa Imani wanaushawishi mkubwa kwa waumini wao Mbaya zaidi CCM wanapoendelea kuumiza hii NCHI wanakuwa kimya hii sisawa CCM kuwa madarakani hata aje MALAIKA kupitia chama hicho hakuna Jipya litakalofanyika
 
Back
Top Bottom