Elections 2015 UKAWA na Lowassa unganeni mchukue nchi, wakati ndio huu, mkipuuzia huu ushauri basi tena!

Serena

Senior Member
Apr 4, 2014
124
125
Ndugu Wananchi,

Mimi kama mdau wa siasa na mzalendo kwa nchi yangu naomba nitoe ushauri ufuatao kwa UKAWA pamoja na Lowassa. Najua kuna watu inaweza ikawa ngumu sana kuelewa point yangu, lakini wenye ufahamu na mambo ya siasa na mapinduzi wataona point yangu.

Huu ushauri wangu umezingatia hali ya uchumi wa watanzania ambayo imeendelea kuwa maskini huku viongozi wakizidi kutajirika sana (mfano familia ya Rais wa sasa). Naelewa pia kuna watu watakuja hapa na fikra ya ufisadi wa ndugu Lowassa na kwamba hafai kupokelewa UKAWA. Hivi hawa ukiwauliza waweze kuthibitisha huo ufisadi wa Lowassa wanao majibu? Na je ni nani ndai ya CCM ambaye ni msafi?

Je huyu Magufuli ni msafi kiasi gani? Ni kwa vipi tumesahau juzi taarifa za CAG jinsi alivyolidanganya Bunge na upotevu wa billions zaidi ya 500? na je si ni huyu huyu Magufuli ndiye aliyehusika kwenye sakata la uuzaji wa nyumba za serikali? akimuuzia girlfriend wake na kaka yake ambao hawakuwa watumishi wa serikali kinyume cha utaratibu?

Nauliza tena, je ni nani MSAFI ndani ya CCM? Jibu ni HAKUNA MSAFI CCM. Na kwa wale wanaotegemea kuona mabadiliko yoyote hasa ya kiuchumi chini ya kiongozi yeyote ndani ya CCM hao wanajidanganya. Kwa CCM hata uwe msafi kiasi gani ukishaingia utakuwa unafanya matakwa ya CCM ya kulindana hasa ya kulinda wenye pesa na si kwa ajili ya wananchi.

Kwa hakika CCM haipo kwa ajili ya wananchi, kwani chini ya CCM tangu Uhuru, hakika hatujapata nafuu yoyote japo tuna rasilimali nyingi kama madini, maziwa , mafuta na gesi sasa. Naomba wananchi wenzangu mfungue macho na kuona jinsi muswada wa gesi na mafuta ulivyopitishwa juzi kwa hati ya dharura ili kulinda maslahi ya watu na si wananchi.

Ni wakat sasa wananchi wajue kwamba ADUI yao mkubwa ni CCM na mfumo wake na si watu, kwani watu hata wawe wazuri kiasi gani, lkn akishaingia ndani ya CCM, huyo mtu kwisha habari yake.

Baada ya huo utangulizi, sasa naomba niongelee kilichonisukuma mimi kuchukua muda kuandika thread hii. Awali ya yote naomba niseme kwamba mimi sina chama lakini ni mwenyeji wa Kanda ya Ziwa. Na kwasababu natoka eneo moja na Magufuli, wengi wangetarajia mimi pia niwe kati ya watu wanaofurahia uteuzi wake.

Naomba niseme kwamba, kwanza Magufuli ni mtendaji mzuri pamoja na kwamba ana udhaifu wake lakini kwa ccm yeye kidogo ana nafuu. Hatahivyo, pamoja na utendaji wake kuwa na unafuu, lakini HATALETA MABADILIKO yoyote, kwani akishaingia kwenye uongozi, yeye naye ataishia kufanya kama chama kinavyohitaji.

Na kwa msingi huo, mabadiliko ya maana katika nyanja zote yataletwa na chama mbadala na si ndani ya CCM.

Hivyo basi, Ombi langu kwa UKAWA ni kwamba wampokee Lowassa kupitia CHADEMA na Lowassa apewe nafasi ya kugombea Urais kupitia UKAWA. Naomba nirudie tena, Lowassa apewe nafasi ya kugombea URAIS. Hii ndio njia pekee ya kuitoa CCM na kuleta mfumo mpya utakaoleta mabadiliko hapa Tanzania.

UKAWA, kama kuna mtu mwenye value added kwenye mchakato wa kumtoa mkoloni mweusi madarakani ni Edward Lowassa, na wakati ndio huu na mkiacha tu hii nafasi, basi mtaendelea kuwa wapinzani miaka nenda rudi na mbaya zaidi hata wabunge watapunguakwa kasi sana mwaka huu. Hakuna mtu yeyote anayeweza leta thamani kwenye UKAWA na kuipa Ushindi toka CCM mbali na Lowassa pekee.

Faida ni kwamba CHADEMA tayari kina msingi nchi nzima na wafuasi wengi sana. Lowassa naye ana back up ya watu wengi sana na hata baadhi ya viongozi wa CCM katika ngazi zote watakuja naye. Naomba ieleweke kwamba Lowassa anapoingia CHADEMA atakuta mfumo ambao nao uko tayari, kwahiyo atafanya kazi ndani ya huo mfumo, na hivzo mambo ya CCM hatakuwa na impact kwenye mfumo atakaoukuta CHADEMA na UKAWA.

Na ukizingatia mfumo wa CHADEMA unavyojali wananchi, hivyo watanzania tutafaidika sana hasa kiuchumi. Lowassa akiwa mgombea Urais wa UKAWA atasaidia sana hata majimbo mengi ya ubunge kwa Wana UKAWA.

Mapendekezo yangu kwa wagombea wa UKAWA ni huu hapa:

1. Lowassa agombee urais kupitia CHADEMA.

2. Prof. Lipumba agombee Umakamu wa Urais.

3. Dr. Slaa akagombee ubunge ili aje awe waziri mkuu.

NB1: Naomba ieleweke kwamba mpaka sasa majimbo ya CHADEMA hasa za maeneo wanakokaa wasukuma (Kanada ya Ziwa) kwa kiasi kikubwa yatarudi CCM kwasababu ya Magufuli kuwa msukuma. Asiyetaka kukubaliana na mimi asubiri October. Na kura za urais vivyo hivyo. Na kwa msingi huo, ni lazima CHADEMA na UKAWA wawe na target ya kura za nyanda za juu kusini, kusini, kati na kaskazini. Na watu wa kusaidia UKAWA kukusanya kura za kutosha katika maeneo hayo ni Lowassa (Kaskazini, Kusini, kati, na nyanda za juu kusini) na Lipumba hasa kanda za magharibi na Kusini.

Najua kuna watu watakuja na hoja hapa ya Muungano kuhusu nafasi ya urais na makamu wake. Hapa UKAWA walenge kuondoa mfumo wa CCM na hivyo wanatakiwa watu wenye ngu (influencial people). Na kwa kuzingatia hilo, kwa CUF ukiondoa Lipumba anakuja Hamad amabye anagombea Zanzibar. Na kwasababu hiyo, wana-UKAWA wa Zanzibar wakubali tu wagombea wote watokee Bara, kwani matunda ya mfumo wa UKAWA utawafaidisha wananchi wote.

NB2: Lowassa atasaidia pia urais wa Seif Hamad kwa upande wa Zanzibar, kwani kuna wtu kule ambao hawajakubaliana na maamuzi ya CCM ya kuwaondoa akina Bilal. Na pia Lowassa na Karume ni kitu kimoja.

Naomba nimalizie kwa kusema kwamba hii ndio nafasi pekee ya CCM kuondolewa madarakani. Na njia pekee ni kupitia kwa Lowassa na UKAWA. Chadema na UKawa kubalini huu ushauri na hakika watanzania tuko nyuma yenu, kwani tunaamini kwamba uchumi wa Tanzania utabailika kwa mfumo ulio nje ya CCM na CHADEMA na UKAWA wanaweza kutumia nafasi hii sasa ya kumkubali Lowassa ili tupate mabadiliko.

UKAWA mnatakiwa kuwa makini, acheneni na propaganda za watu wengi hapa JF na mkubaliane na hali halisi. Wakati ndio huu na mkiuachia basi watanzania wasahau mabadiliko kwa kipindi kirefu sana.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki UKAWA.

Ahsanteni.
Ni mimi Mpenda nchi.

Watanzania,
Hatimaye ombi langu kama thread hii inavyosoma inaelekea kutimia muda si mrefu. Nalo ni Lowassa kuingia UKAWA na kugombea nafasi ya URAIS. Nataka niwaambie UKAWA tena, hili ni pigo kubwa sana kwa CCM na wale wote wasiopenda kuona mfumo CCM ambao ni mfumo mbaya kupita yote duniani ikiondolewa madarakani. Naomba nirudie tena, kwasasa Watanzania wanatakiwa kumtoa mdudu CCM bila kujali nani mgombea wake, kwani CCM ni mfumo usio na tiba kwa mtu anayeshinda uongozi kupitia CCM.

Na kwa wale wote mliodhani Lowassa hana impact, sasa subirini muone mwisho wake. Pia niwaombe tu muache kulalamika sasa, si mlimtema kwamba hafai, na hata wale waliokuwa upande wake wote ndani ya CCM nao wanaangushwa kwenye kura za maoni (rejea Nchimbi, Pindi Chana, n.k.) ikiwa ni maagizo toka kwa Mwenyekiti wa CCM na Wazee wa Kitengo maalumu? Sasa mnalilia nini tena, kwani Lowassa ndio huyooo?

Yaani ni raha mstareheee kila kona kwa UKAWA, ebu jaribu kufikiria, Lowassa anapiga Kampeni sehemu moja ya nchi, Dr. Slaa naye anapiga kampeni sehemu nyingine, Prof. Lipumba naye ndani ya Nyumba, Lissu kama kawaida, Mbowe naye anapiga kotekote, n.k. Naomba CCM mje hapa mniambie huu mziki wa UKAWA utatulizwa na nani????? Je Mzee Pombe Magufuli na kauli mbiu yake SITAWAANGUSHA atauwezaaa?????? Thubutu yake.

Mbarakiwe sana, kwani hatimaye naiona Tanzania mpya nje ya mdudu CCM ikizaliwa chini ya mfumo mpya unaojali maslahi ya Watanzania UKAWA.
 
Naona huna nia njema na Lowasa.
Kwa maoni yangu UKAWA yatosha.
Ushauri wa bure kwa Lowasa: akapunzike, siasa kwake basi. Ya CCM ikimshinda kwenda kutangatanga uzeeni hakutamfikisha popote isipokuwa atajizolea aibu na kuporomoshwa zaidi.
 
Ukawa hatuwezi kula matapishi yetu…NO NO NO to Lowassa….Aende kwenye chama chake cha ACT
 
Yaani uko sahihi 10000%..

Lowassa aki team up na Ukawa CCM ndio kwaheri bye byeeee....!!!

Lowassa ndio kila kitu sasa hivi kwa wananchi, UKAWA inabidi wamtumie vema sana sasa hivi, waache ujinga wa maneno ya uzushi, waungane na Lowassa sasa hivi, wasichelewe... na UKAWA watashinda kwa urahisi sana sanaaa...

Nilisema, CCM ndio wamejiweka pabaya mnooo, watu hawakujua, sasa watajua muda si mrefu...!!!
 
Uzi wako una mantiki nzuri sana, sema UKAWA wanaanzaje kumsafisha kwa wananchi ili aeleweke vizuri?
 
Serena

Uzi wako una mantiki nzuri sana, sema UKAWA wanaanzaje kumsafisha kwa wananchi ili aeleweke vizuri?
 
Last edited by a moderator:
Naunga Mkono Hoja... ILa Lowassa yampasa kuweka bayana yote hadharani .... anatakiwa kuweka mbinu zote na mikataba yote ya kijinga ya CCM kwanza ... Lowassa ana timu Imara ... akishirikiana na UKAWA hakika CCM itaondolewa tu ...
 
Kuna logic kubwa sana kwenye thread yako let's consider it ila lowassa yupo tayari?
 
Hongera sana kwa uchambuzi wako imara Hakika hii ndo namna pekee ya kupambana na ccm, vinginevyo, vinginevyo wapinzani watagaragazwa kwenye uchaguzi mkuu, ni muda kwa wenye maamuzi kufanya hesabu Nzuri za kisiasa, sehemu nyingi mno ambapo chama tawala kilingolewa unakuta Kuna mtu aliyekuwa chama tawala kahama, na uzuri ni kwamba lowassa akienda upinzani ataenda kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chadema, atakua chini ya uangalizi wa chama.
 
patamu hapa kiasi flani kuna mashiko kumuweka lowassa sio issue
issue ni miiko ambayo vyama vya upinzani vinayo ndo kasheshe
Na tusije kudhani eti CCM hayo yote hawayajui au hawayaoni
wanaona sana na wenyewe wanajipanga
 
Ushauri mzr ila naona bora ajiunge ukawa awape mbinu zaidi na kutoboa siri za chin ya uvungu kw weledi wa kiwango cha juu haki ya Mungu akidhamiria ccm itakuw bhaaaaas...
Hii nchi nahama khaaah!bora nikapange ughaibuni Hahahahaaaa. ...
 
Uzi wako una mantiki nzuri sana, sema UKAWA wanaanzaje kumsafisha kwa wananchi ili aeleweke vizuri?

Kama lowassa anao ushahidi wa kutokuhusika waziwazi na Richmond kama anavyodai basi ni rahisi sana kusafishwa!
 
Naunga mkono hoja pls!!!!! UKAWA viongoz fanyen hima sisi wananchi tutawapen kura za kutosha yan hii ni turufu nzur sana hata kama el alikuwa fisad ndan ya ukawa atakuwa mtu safi kwan hata dhahabu ikipita kwa moto lazima ing`are tuu fanyieni kaz mawazo hayaa msipuuuuuuze pls!!!!
 
Ngoja tuone,inawezekana kuna kitu kinachoendea sisi hatujui,tunaanza kujua taratibu. Upinzani wa kweli utatoka ndani ya ccm. Nakuunga mkono.
 
Mkuu, hata mimi naunga mkono wazo lako! Kwa Kweli Lowasa angetinga UKAWA tungewanyoosha CCM. Kwanza tungeongoza bunge na hata wangeiba kura za rahisi tungemchapa bungeni na kumwondoa. Spika angekua wetu UKAWA na tungeweza kufanya mabadiliko makubwa kwenye nchi hii pamoja na kuifutilia mbali miswada ya gesi iliyopitishwa juzi kimagumashi na kuirudisha katiba pendekezwa ya mzee wetu Warioba. UKAWA fursa hii ya Lowasa itumieni. Ataleta nguvu kubwa ndani ya UKAWA. Tukumbuke maneno ya baba wa Taifa '' Mpinzani wa kweli atatoka CCM" naye ndiyo anaweza kuitoa CCM.
 
Back
Top Bottom