Mapadre waanza rasmi kumpigia Magufuli kampeni

Mapadre waanza rasmi kumpigia Magufuli kampeni

Inasemekana rais mkristo atatoka katoliki tu. Na rais muislamu atatoka ------------tu hivyo basi huyu ajaye ni rais wa katoliki ingawa katoliki ilimtaka Pinda sasa inabidi wamsapoti huyu. EL dhehebu pia limemponza tz ni katoliki na shia.
Wazee wa Kurasini ni hatari. Ilibidi Eddo akatwe tu. Niliwahi kumwambia Pasco alinielewa kwa mbaaaaaaaaali
 
Last edited by a moderator:
Unajua mwisho wa siku ktk jamii za kiafrika hatutajua nani ana akili timamu kama Padre anayesemekana ni msomi ingawa mm huwa sina uhakika sana maana nijuavyo mm ELIMU ya mtu yeyote yule hupimwa kwa mawazo na matendo yake kama watu wanasema huyu mtu ni msomi halafu yeye anaongea ujinga na upumbavu waziwazi bila haya wala soni huyo moja kwa moja si msomi na lengo lake ni kutuangamiza ss waamini,kimsingi wenye kufanya shughuli za kiuchumi ni ss na wao mapadre na maaskofu wanasubiri pesa za maangaiko yetu.Ni wakati muafaka kwa waamini kujiongeza na kutokuwaamini mapadri na maaskofu kupindukia tukumbuke tukiwaachia wao kufikiri kwa ajili yetu mwisho wa siku wenye kuambulia mateso ni ss.Mapadri ni binadamu kama ss wanazaliwa kwetu na jukumu la kumjua MUNGU na kumtumikia ni letu sote.Tuamke watanzania wa kabila na dini zote na tukumbuke historia ni mwalimu mzuri,Kikwete tulimshangilia na kumwita chaguo la MUNGU na kumkaribisha Madhabahuni leo hii kila MTU analia kwa maisha magumu,udini,kukithiri kwa ufisadi na utoshaji wa nyara za nchi huku mtu aliyeitwa chaguo la MUNGU na haohao mapadri na maaskofu akilinda uozo kwa gharama zote.Inawezekanaje Leo hii watu walewale waendelee kutuchagulia viongozi nadhani sasa tusemi imetosha na waache kila mwananchi achague alicho ona bila kupotoshwa na MTU awaye yote.Ninawasihi waamini kumwomba MUNGU na kuachana na ujinga wa kuchaguliwa viongozi na baadhi ya watu wasio na Roho Mtakatifu na kuishia kutudanganya.Huu ni mwaka wa kuachana na MAZOEA MABAYA ktk kuchagua viongozi ili tusonge mbele kimaendeleo na tukileta utani na mizaha tutabaki maskini pamoja na kuwa na rasilimali nyingi ktk Afrika.

ama kweli kipofu hawezi kumwongoza kipofu mwenzake wote watatumbukia shimoni,

haya maneno Naona sasa yanachukua nafasi hasa kwa viongozi wa dini wakati mwingine wazuie midomo yao wawapo mimbarini,

wakati mwingine najiuliza hivi tumelogwa na nani?

Maana ni wepesi wa kusahau kwa kudanganywa na tunakubali kudanganyika,

ccm hata haje malaika kwa mfumo ulivyo hawezi fanya chochote, tatizo siyo mtu tatizo ni mfumo,

hawa watumishi wajitathimini sana,wapo walio sema mh kikwete ni chaguo la MUNGU leo wamekula kona,
 
kelao

Acha ujinga,wenye akili na busara wanatambua wapi nchi yetu inatakiwa kukaa.magufuli is the spesho one.viongozi w dini ni binadamu kama sisi na mambo ya kiroho kila MTU a a yake.nakuhakikishia hakuna kiongozi wa dini kwenye kujali utu na maslahi ya taifa anaweza kumkataa magufuli.viva john pombe magufuli.tuache ushabiki wa kijinga.upinzani haujajipanga kuchukua nchi na kama wakimchukua lowasa nakwambia tunarudi chama kimoja ccm.watanzania si wale,sasa wanajua mbivu na mbichi.tusubiri tume ya uchaguzi itangaze siku ya kampeni.
 
Last edited by a moderator:
huyu padre ni mfano wa kuingwa maana mwaka huu kila mgombea tutamuuliza amelifanyia nini taifa hii hadi uzee wake alionao,kama haujawai kuwatumikia wananchi basi hatuna kigezo cha kukupima,basi wamuachie magufuli ambaye amewatumikia watanznaia kila kona,
 
Mapadre ni binadamu kama wewe, kama mimi na kama yule. Ni sehemu ya jamii yetu, wanaona wanasikia na wanahisi kinachotendeka katika jamii walimo. Ni watanzania kama wewe walio na kazi kama ulivyonayo wewe. Machungu na mazuri ya kiongozi mzuri au mabaya ya kiongozi mbaya nao pia wanayapata kama mtu mwanachi mwingine anavyoyapata. Suala la kusema vongozi wa dini wasishughulike na siasa ni ubaguzi kama ubaguzi mwingine wowote. Ni sawa na kusema wanawake au waalimu au watumishi au madaktari wasishiriki siasa. Haya ni amkundi ya wananchi ni kosa kuwabagua kwa sababu ya kundi walilomo. Wote tuna kumbukumbu ya baahi ya maaskofu walivyoshiriki siasa hadi kuleta ukombozi katika baadhi ya nchi hapa Afrika. Askofu Desmund Tutu wa Afrika kusini ni mmoja. Kuna masheik wengi tu walishiriki kutafuta uhuru wa Tanzania. Kama vile haitoshi Mapadre wanajifunza Falsafa ( Logic by definition is a science of thinking). Kuwazuia kushiriki siasa ni sawa na kusema wasifikiri maswala yanayohusiana na siasa. Maana yake siasa ibaki na watu wasiofikiri kisayansi. Maana yake Mapadre na waumini wao wote kwa pamoja waburuzwe na watu wasiofikiri kisayansi ili hali Tanzania ni ya wote. Hoja dhaifu ya kuwagawa wananchi kwa misingi ya dini haina mashiko kwa sababu inatumika tu kuwaondoa wananchi kwenye ajenda. Nchi haiwezi kuwa mali ya wanasiasa peke yao. Nani kawakabidhi?Mapadre wanaongoza kundi kubwa la watu ambao wanashiriki siasa wakiwemo wagombea. Wagombea ni zao la viongozi wa dini, wameshirika kuwajenga watu hao kitabia kimadili hata kimaono ni watu wao. Kuwakataza wasiseme neno juu yao ni sawa na kusema mwanafunzi anapoenda kufanya mtihani mwalimu wake asiseme nen hata la kumtakia kheri, mwanafunzi akifaulu mwalimu asifurahie mafanikio aliyochangia kuyaleta. Magufuli ni mkristo, mkatoliki, mseminari ni zao la mapadre. Kutegemea mapadre wanyamaze ni kuikandamizi furaha ambayo kwa kweli wanayo kwa kuwa wameshiriki kuijenga. Kama watu wanathubutu kutambua mchango wa mke wake amabaye ameanza kuishi aye baada ya kujengwa na viongozi wake wa dini ni wizi wa mchango wa mapadre. Uchapakazi, uadilifu na umakini hujengwa wakati wa utoto. Biblia takatifu inasema ' mfunze mwanao njia impasayo, hataicha hata wakati wa uzee wake' na wahenga wanasema 'usione vinaelea vimeundwa'
Katika kile kinachoonyesha viongozi wa dini kuingilia mambo ya siasa, padre Mbano akihubiri ktk Ibada ya leo j2 kwenye Kanisa kuu Katoliki Songea Mjini amesema ujio wa Magufuli ndio jembe haswa lililokuwa linasubiriwa, akaendelea kusema kuwa anawaomba radhi wapinzani safari hii waachane na urais wamwachie Magufuli aweke mambo sawa. kaendelea kusema, 'wapinzani tutawapa ubunge, lkn urais Magufuli anatosha' hapa kulikuwa na minong'ono kanisani. Najiuliza ni mapadre hawa hawa na maaskofu mwaka 2005 walisema JK ni chaguo la Mungu lkn sote ni mashahidi wa kilichotokea. Kwa nini wasiwaachie wananchi waamue wenyewe? Kwa ushawishi walio nao mapadre kwa waumini wao wapinzani wasipokemea haya basi wasahau urais 2015. pia hawa mapadre wana elimu kubwa sana lkn wanashindwa kutambua kuwa wale waumini wanaowahubiria kuwa ni wafuasi wa vyama mbali mbali..
 
Acha ujinga,wenye akili na busara wanatambua wapi nchi yetu inatakiwa kukaa.magufuli is the spesho one.viongozi w dini ni binadamu kama sisi na mambo ya kiroho kila MTU a a yake.nakuhakikishia hakuna kiongozi wa dini kwenye kujali utu na maslahi ya taifa anaweza kumkataa magufuli.viva john pombe magufuli.tuache ushabiki wa kijinga.upinzani haujajipanga kuchukua nchi na kama wakimchukua lowasa nakwambia tunarudi chama kimoja ccm.watanzania si wale,sasa wanajua mbivu na mbichi.tusubiri tume ya uchaguzi itangaze siku ya kampeni.

mkuu wamekusikia ,wengi wanazani rais anapatika kwa ushabiki tu maana hata diamond anawatu wengi ,lakini viongozi wa dini ni miongoni mwa makundi machache yenye kujua nani anatakiwa kuwa rais na ndo maana baadhi ya makundi hayo yamempendekeza MAGUFULI, na hakuna mtu wa kumzuia kuwa rais kwa faida ya watanzania wote,
 
Corruption can make heaven to be hell and a hell to be heaven...
 
sio wote wapo wengine kama huyu padre wenye jicho la pekee na kutusaidia sisi tunaoendekeza miemuko ya siasa chafu na kupoteza weredi wa kujua kiongozi bora,
Tatizo la mapdre hawa ni wao kujiona wamesoma na wanajua zaidi kuliko sisi waamini wao!! Hili ndilo kosa kubwa wanalofanya. Humo kanisani kuna watu wengi tu tena sana wanaowazidi Elimu na uelewa, kinachotupeleka pale ni kutimiza imani yetu lakini si kutulisha mambo ambayo hayakutupeleka pale, kama wanataka kuzungumza siasa wasubiri mikutano ya hadhara nao watoe yao ya moyoni na kanisani au msikitini ambako kila mtu ana chama chake. Wakiendekeza mambo haya kuelekea uchaguzi mkuu sadaka zitapungua sana na mahudhurio pia.
 
Kumkomesha padre kama huyo kama atatoa mahubiri kama hayo msuse kutoa sadaka ndo atajua mmekasirika, hatarudia tena.

Wewe unafikiri wote tuko pamoja na wewe??? Sadaka tutatoa wewe ni nani? wakutuzuia tusitoe sadaka?? Amesema maoni yake kama binadamu ni juu yako kufuata au kutofuata!! Mbona mahibiri mengine waumini pia huwa hawafuati kama vile watu wanaambiwa wasizini au kuiba lakini wakitoka tu Kanisani wanaendelea na makosa yaleyale tuuu!!!! Acheni siasa ukwara hapa??!!! Magufuli ndo raisi wa TZ.
 
ama kweli kipofu hawezi kumwongoza kipofu mwenzake wote watatumbukia shimoni,

haya maneno Naona sasa yanachukua nafasi hasa kwa viongozi wa dini wakati mwingine wazuie midomo yao wawapo mimbarini,

wakati mwingine najiuliza hivi tumelogwa na nani?

Maana ni wepesi wa kusahau kwa kudanganywa na tunakubali kudanganyika,

ccm hata haje malaika kwa mfumo ulivyo hawezi fanya chochote, tatizo siyo mtu tatizo ni mfumo,

hawa watumishi wajitathimini sana,wapo walio sema mh kikwete ni chaguo la MUNGU leo wamekula kona,


nikusaidi hakuna mfumo unaomuongoza rais duniani kama rais ni dhaifu basi ataongozwa na mfumo,lakini kama ni hodari basi anauwezo wa kubadili mfumo,
pia nikusaidie ukishakuwa rais hakuna anayekwambia chagua mawaziri wa aina furani ,awakuu wa idara wa aina furani,wewe mwenyewe ndo unapanga yupi unaweza kufanya nae kazi,kama wewe ni dhaifu utachagua baraza la mawaziri zaifu kama ndo walikuchangia hera ili upate madaraka ndo watakuongozi ,
lakini kama wewe ulisimama mwenyewe utaweza kuweka watu ambao wanakufanana,
 
Wewe unafikiri wote tuko pamoja na wewe??? Sadaka tutatoa wewe ni nani? wakutuzuia tusitoe sadaka?? Amesema maoni yake kama binadamu ni juu yako kufuata au kutofuata!! Mbona mahibiri mengine waumini pia huwa hawafuati kama vile watu wanaambiwa wasizini au kuiba lakini wakitoka tu Kanisani wanaendelea na makosa yaleyale tuuu!!!! Acheni siasa ukwara hapa??!!! Magufuli ndo raisi wa TZ.

mkuu achana nao wengi hawajui ni aina gani ya rais tunaemtaka na kama wanajua basi miemuko ya makundi ya ulaju wao yanawafanya kuwa vipofu kiasi cha kushabikia mtu abaye hata hana lolote alilolifanya katika taifa hili.magufuli hakuna wa kumzuia wanye jicho la peke wameishaona ndo mtu pekee anayetakiwa kwa sasa na sisi tunawaunga mkono,
 
anayepinga kuwa Magufuli kwa hali tuliyonayo sio chagua sahihi basi
1, ana matatizo ya akili
2,hajui taifa hili linamtaka mtu wa aina gani
3,inawezekana ni mkimbizi humu tz
4, siasa za makundi, vyama,ukabila ndo zinamfanya kipofu
5, miemuko ya siasa inamfanya kupoteza wererdi wa kujua wapi na nani anaweza kutupeleka tunapotaka kwenda,
 
Mie ni mkatoliki tena mseminari lakini niseme tu kuwa Padri huyo ni mpu.mbavu kama alivyokuwa Kilaini mwaka 2005.

Wewe kama mseminari maliza kwanza shule ndo ujilinganishe na kaka yako. Kuna distance kubwa kati ya padre na seminarist kwahiyo chunga sana, huwezi kujua kesho huyu padre anaweza kuletwa shuleni kwenu akaja kukufundisha "moral theology"
 
Ndio tatizo dini bandia zimefunga ndoa na serikali za Wanadamu
 
Nikiwa kama Mkatoliki,siwezi kushawishiwa na Kiongozi wangu wa Kanisa kwamba nimchague fulani na fulani hafai,nitachagua kwa utashi wangu Mungu alionijaalia kwa kusikiliza na kuchambua sera zao na kuchanganya na zangu..haya mambo ya viongozi wa imani kuingilia ingilia siasa kwa matamko yao waamini wenzangu na waTanzania kwa ujumla tusishawishiwe nao siku ya uchaguzi ikifika vote kwa mwenye sera nzuri unaeona atatuletea maendeleo kama taifa.
 
Kwani mabavicha yana akili? Zaidi ya viroba vichwa vyao vitupu sana.

Mabavicha ndio nini? Sina namna ya kukujibu maana umeandika kitu nisichokielewa na bila shaka wengi pia hawakielewi. Au umenena/kuandika kwa lugha mpya? Ndo ulivyojifunza kanisani Tanganyika parkers?
 
Kama ni kweli, padri kanikwaza sana. Kala maharage ya wapi huyu!
 
Back
Top Bottom