Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Hapo kwa Mctomney ndipo kilipo kidonda, ila maeneo mengine yote ya mwili najisikia niko vizuri kabisa.

Naombeni nitafutueni tiba ya eneo hilo, huyo De Jong naona kama munanitibu kichwa ilhali mimi naugua kiuono.

Chonde chonde doctor, okoa maisha ya mgonjwa mimi, bado Dunia naipenda.
 
Cavani amevuna fedha ya kutosha United,akienda timu ya taifa yuko fit akirudi Manchester anajifanya majeruhi,kuna kipindi RR alilazimika kumchezesha CR7 sababu hakuwa na option Greenwood yuko jela,Martial yuko Seville,Rashford confidence/kiwango kimeshuka aliyekuwa available Cavani anajifanya majeruhi.

BTW :Ilikuwa mistake kubwa sana kuwa na CR7 & Cavani kwa pamoja si sawa na kuwa na striker 2 wazee kwa pamoja,makosa mengi yalifanyika huko nyuma wachezaji walikuwa na power sana .United imesajili wachezaji wengi lakini ilishindwa kuwatumia
 
Attitude ya Cavani mwishoni ilikuwa inatuonyesha kukerwa na ujio wa CR7,hii ndio point yangu.

Ni kweli hatukustahili kuwa na Cavani na Ronaldo kwenye timu moj bila kujali suala la umri hasa ukizingatia siku hizi mfumo wa kuwatumia washambuliaji 2 kwenye mechi kuanzia mwanzo au mara kwa mara ni nadra sana.
 
Mkuu unajicho kali sana......
Huyo (Ronaldo) ndio kachangia kuturudisha nyuma

Hata kushuka kwa Fernandez kunachangiwa na huyo huyo jamaa.... aende tu, aagh.
 
Kuzuiwa kuondoka kwa Lingard,Pogba na sasa Ronaldo (kama atabaki) ni kwa sababu za kibiashara zaidi kuliko faida za uwanjani.
United itachukua muda sana kutoka kwenye hali iliyopo sasa.
 
Tena mshahara wake tutalipa wachezaji watatu wapya,.Ila Man u tujifunze kutosajili wachezaji kibiashara,huyo ronaldo mwaka jana hakua kwenye plan,na huenda tungemtemea Cavani tungemaliza vizuri tu
Omeona eee!
 
Ila Mkuu sifa ya ETH ni kutumia Alichonacho, Ajax ya kina FDJ na De Ligt striker alikuwa Tadic.
 
Ronaldo amesababisha tubadili Tactics, tulikuwa tunacheza low Block kwa success nzuri tu, system ambayo ilificha madhaifu ya wachezaji wetu, na sababu mbele tulikuwa na msingi mbio wengi ilikuwa ni kawaida kutoa mpira golini kwetu mpaka kwa adui na kufunga kwa sekunde chache.

Msimu unaanza si Haba tulianza vizuri kiasi fulani, mwisho wa mwezi akaja Ronaldo.

Ikabidi timu ianze kucheza Highline, ili kum accomodate Ronaldo mzee ambaye kupanda na kushuka hawezi tena, kutokana na kucheza Highline Maguire akawa Exposed hana Speed, Telles na Dalot vimeo pembeni kukaba hawajui, Hatuna Dm etc tukaanzq kufungwa magoli ya Kutosha tu.

Na mtu akisema Ronaldo amefanya Tucheze vibaya haimaanishi Ni mbaya, akiwa kwenye Timu yenye Midfield za maana kama Chelsea mbona anaweza cheza vizuri tu.
 
Huyu De Jong ni EtH mwenyewe anamtaka binafsi nilimkata na nitaendelea kumkataa.
Habari za Frenkie De Jong zinanikera sana sio siri. Huu usajili tutajutia sana hata kama baba yake anamtaka.

Kwa nini tucheze kamari ya gharama wakati tuna cheap & best option? (Ruben Neves).
Huu usajili wa De Jong tunawasaidia Barcelona kutatua matatizo yao. J'5 Barca watamtambulisha Franck Kesssie, tayari wamempa mkataba mrefu Pedro Gonzalez 'Pedri' then lastly they have a big contract for Pablo Gavira 'Gavi'. Technically, they don't have space for De Jong.

Narudia tena na tena na tena huu usajili wa De Jong ni win win situation kwa Barcelona. De Jong ana option mbili tu ajiunge United au apunguze mshahara. Mimi chaguo langu daima ni Ruben Neves huyu ni proven EPL player. Gharama yake ni pound 50M tu plus $150 - 200k weekly vs De Jong pound 73M plus $250k - 300k weekly.
 
So alikuja kufanya nini kama hakuna timu ya kuimplement tactics?

We nimekuona mbishi, simply.
Yeah, mi mbishi. Why should i comply with your bullshit?

Why do you think so? Who are you?

I'm saying for the last time. United haina hiyo timu kwasababu wachezaji ni walewale. Hawafundishiki na hakuna usajili wa kueleweka umefanyika.

Ralf alikuja akafundisha na hawakufundishika.

Atleast we should have 5 key players signed already. Huko ndo tungeanza kuona uelekeo mzuri wa kuibadili United.
 
Yeah. Upo sahihi.

Hilo fungu alilopewa angegusa maeneo yote muhimu.

Kuna namba zinahitaji replacement ASAP.

Tukianza msimu hatujazifanyia kazi, we're finished before we start.
 
Ila Mkuu sifa ya ETH ni kutumia Alichonacho, Ajax ya kina FDJ na De Ligt striker alikuwa Tadic.
Ajax ipo farmers league.

Man Utd ipo ligi ngumu sana duniani, tena wakati huu kuna timu kubwa 4 zinajielewa.

Kila match ni muhimu kuliko.

Na isitoshe kuna makombe manne tunagombania.

Nioneshe kikosi cha United cha kutoa challenge.
 
Tumpe kocha nafasi.

Aje na kila mtu anayemtaka.

Ila baada ya msimu wa pili, hakuna atakaekuwa na uvumilivu.
 
Ajax ipo farmers league.

Man Utd ipo ligi ngumu sana duniani, tena wakati huu kuna timu kubwa 4 zinajielewa.

Kila match ni muhimu kuliko.

Na isitoshe kuna makombe manne tunagombania.

Nioneshe kikosi cha United cha kutoa challenge.
Tuna Beki wa kati 7, Full back 5, viungo washambuliaji 2 wa kati na bado kuna wa tatu pengine akaja, Mawinga 6 etc.

Sehemu pekee ambayo ambayo tupo ovyo ni kiungo wa kati, na Akija FDJ na Garner akibaki napo pia tutakuwa na Depth nzuri.

Kikosi Kilichotupa nafasi ya Pili mtoe Greenwood muweke Sancho thats it.

Kifupi bado kikosi chetu kipo bloated kuna wachezaji kibao bado wanatakiwa wauzwe.

Na hayo mashindano manne, matatu si makubwa Europa na kina Carabao ni sehemu ya kuwapa watoto experience, watarotate kina Hanibal, Garnacho, Garner etc.
 
inasemekana fulham na baadhi ya timu walimtaka ila eth aligoma kasema anampangonae kwenye kikosi chake cha kwanza me nimechoka kabla ligi haijaanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…