uchezaji wetu wa tahadhari uliopitiliza nao ni kikwazo kikubwa sana kwa timu yetu kudominate game kwa dakika 5-10, kama tunahitaji kuzicontrol hizi mechi kubwa kama wafanyavyo liverpool au man city tunahitaji kuwa na utulivu wa kiuchezaji and organised time with the ball.
Binafsi naunga mkono mbinu alizokwenda nazo Ole dhidi ya liverpool bila ya kusahau fikra na heshima na taadhima kubwa dhidi ya adui yetu. Kuna baadhi ya makocha na timu zao huwa hawana heshima dhidi ya wapinzani wao na inapotokezea wamedhalilishwa kimatokeo ndipo mashabiki wao huanza kumyooshea kidole mlengwa fulani.
naambatanisha na mifano
- mechi ya liverpool dhidi ya atletico madrid: kuanzia wachezaji, benchi la ufundi hadi mashabiki hawakuwaheshimu atletico madrid baada ya kumalizika kwa dakika 90 pale vicente calderon, wachezaji wengine walifika hatua ya kusema mutakuja anfield na huko tutawafunza adabu kama mabwana zenu barcelona(hapa nimetumia uswahili). kilichotokezea ni kulaumiwa kipa namba mbili
- barcelona dhidi ya liverpool + bacelona dhidi ya AS ROMA: (mechi zote mbili barcelona hawakuonyesha heshima dhidi ya maadui zao ndio maana wakakumbana na comeback ya aibu)
kuna watu walitaka Ole aende Anfield akiwa uchi wa mnyama na ikitokezea dhahama waje wamnyooshee kidole huku wakimkumbusha baada ya mechi:
- wewe Ole unakwenda uchi anfield huku ukijisahaulisha takwimu za liverpool za kutofungwa pale anfield kwa takribani misimu mitatu, kwa wachezaji gani ulionao hata ukacheze total football na wazee wa higher line defensive?
- wewe Ole unakwenda uchi anfield huku ukijisahaulisha takwimu za liverpool za kutokushindwa kufunga goli pale anfield kwa takribani misimu miwili, kwa walinzi gani ulionao hata ukacheze uchi na utatu mtakatifu wa klopp?
nimesema hapo juu tahadhari na uoga dhidi ya adui yako ni muhimu lakini kama mwalimu unahitaji kuyasoma mazingira au tension ya huyo adui yako unayepambana naye. kwa mfano kipindi cha kwanza takribani wachezaji wetu wote walishindwa kuidhibiti pressing ya liverpool na matokeo yake tukawa tunalose possession na mipira ovyo mara kwa mara, lakini kadri dakika zilivyokuwa zikisogea kuelekea kipindi cha pili tulishuhudia baadhi ya wachezaji wakirudisha utulivu na hatimaye tukaanza kubypassing pressing ya liverpool na kwa hapa nimpe heshima yake scott mctominay kwa kurudi mchezoni kwa haraka zaidi kuliko mchezaji mwengine yeyote.
mpaka dakika ya 70 wapinzani wetu walishakata moto(hawakuwa na nguvu ya kutengeneza nafasi yeyote ya hatari ndani ya boksi letu), kilichonikera ni kuendelea kuushuhudia uoga na tahadhari iliopitiliza dhidi yao, wachezaji wetu wakiongozwa na scott, pogba, shaw na hata fred walishafanikiwa kuivunja pressing ya liverpool kwani tulishuhudia mara kwa mara wakivunja central line ya majogoo ila kilichokuwa kinakosekana ni muunganiko wa pale mbele.
ningelikuwa Ole ningelimtoa scott/ fred ndipo nikamuingiza edison cavani.
hii ndio substitution pekee iliohitajika, baada ya hapo ningeliangalia zaidi mwenendo wa rashford na martial.
====================
tunamuhitaji zaidi jack grealish ili tuwe na 4-4-2 inayonymbulika hadi 4-2-2-2 ya hatari, tunachokikosa kwa bruno na pogba tutakipata kutoka kwake na huu utakuwa ni usajili bora zaidi
uoga na tahadhari zipunguzwe,
Darmian aliandika vizuri sana hapo juzi akinasihi benchi la ufundi litafute njia sahihi ya kiuchezaji baada double pivot ili kuongeza ukali wa safu ya ushambuliaji