Vipi kwa Ole?
Sijatumia public opinion haya ni maoni yangu binafsi.
Ulipaswa uniulize kwa nini nimemchagua Julian Nagelsmann? Na sio tuendelee na Ole au Mauricio Pochettino?
Nimetumia mathematical model approach kumchagua Julian Nagelsmann dhidi ya niliomshindanisha nao akiwemo Ole na Mauricio Pochettino.
Evaluation index zangu zilikuwa muda wa ukocha, asilimia za ushindi, mara walizoingia mashindano makubwa (UCL) na kiwango cha uwekezaji wa fedha ktk vikosi vyao.
Nilipotumia hivyo vigezo hapo juu nikaona Julian (56%) alianza akafuatiwa na Mauricio (47%) na wa mwisho Ole (43%). Hapa nimefanya selection kwa kutumia namba tu. (evaluation index zangu zilikuwa nne tu)
Kigezo kikubwa kilichoni-trigger ni mapungufu tulinayo kwa sasa na benchi letu la ufundi yaani upangaji wa kikosi na usimamizi wa mchezo, kujua nini kifanyike kwa sasa na nani aingie au atoke.
Haya ni maoni yangu binafsi maana uliniuliza nani anafaa kumbadili Ole. Nilimchagua Julian kwa kutumia vigezo vinne na uwezo wake wa game management skills sikuangalia umri wake.