Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Ukirudi misimu 10 nyuma tulikuwa na number 10 bora kuliko Lingard. Na mchango wao uwanjani unaonekana.

Sio huyo Lingard wa kumuangalia kwa jicho la 3.

Hovyo kabisa.
Kitakua kichawi hiki ki lingard sio bure mkuu maana hata mbele uchawi upo,tusubiri siku yake ya kufa itafika tuu
 
Na uyo degea goal anazo fungwa nae waku muangalia vzur c o lingard t kuna kna pogba cjui lindelof Rashid uyo martial wte waznguz t c o wapambnaji
Bora wazingue wengine inaleta matumaini lakini sio huyo lingard,Yani mechi nzima unaweza kuta kagusa mpira mara 5;mbili kati ya hizo mpira umemgonga sasa si bora pogba apokonywe ila kazi nzuri tunaiona sio huyo wa kukimbia kimbia tu uwanjani
 
Pogba anaweza kuwa ni mchezaji mzuri lakini mimi uwa namshangaa sana uwajibikaji wake uwanjani, kupoteza sana mipira halafu kutembea.
Kwakweli kiwango anacho ila ili ashine anahitaji waliomzunguka wajitume haswaa.

mpira kitu cha kwanza kocha mzuri wa uhakika sio kufanya majaribio, aaminiwe halafu inafuata usajili.

angalia liverpool na man city unaona kabisa kocha anahusika kwenye usajili.
liverpool waliingia mikenge sana miaka ya karibuni alipoondoka Rafa kabla ya kumpata Klopp. ona tu rafa alivyopambana newcastle haina usajili wa maana sasa ile itashuka ile.

sasa manchester kama kweli kuwaamini kina ole basi walau ingekuwa kama barca yani mtu alikuwa kocha wa vijana anapandishwa kupokea mikoba ya fergi.
hivi ilivyo, hakuna namna hapa lazima aletwe kocha mzuri ndipo tujadiliane mengine
Hata ole alikua kocha wa vijana
 
Mimi lingard namkubali Sana, dogo yupo sharp, alaf mwepesi, Ila sio mtu wa kupush Sana, na ili aonekane vyema, lazima mdfild iwe strong,
 
Anakaba na kuutafuta sana. Kujituma kwake ndio silaha yake kuu
Kukaba sio main role ya Lingard sasa mnapomsifia kwa kuhangaika mpira ukipotea inamaana Lingard ni Box to Box Mid au? Forward hatumii nguvu nyingi kukaba
 
Kukaba sio main role ya Lingard sasa mnapomsifia kwa kuhangaika mpira ukipotea inamaana Lingard ni Box to Box Mid au? Forward hatumii nguvu nyingi kukaba
Usikariri mpira, Kuna kipindi firminho alikuwa anapewa role hio Liverpool na alikuwa Ni false 9 kabisa,

Carlos tevez 2008/09 ligi ya Uingereza kafunga goli 5 katika mechi 29, Ila still tulikuwa tunamuona mchezaji bora, kwanini? Sababu alikuwa Ni fighter muda wote anasaidia midfield yeye na Rooney, na hayo yanakuwa Ni maelekezo ya Kocha.

Refer Pia ji sung park, 2007 man UTD walikutana na AC Milan tukatolewa nusu tulifungwa 3-0 kule Italy, baadae tulivyokutana nao Tena hao AC Milan Fergie akampanga ji sung park amkabe Andreas pirlo, wote tunajua pirlo Ni deep lying playmaker anakaa na mabeki nyuma Kama defensive midfielder lakini anafanya Mambo yake, ili umkabe huwezi tumia defensive midfield wako inabidi utumie mchezaji mwengine, ndio akawekwa Hi sung park, alikuwa anakaba mpaka kivuli, tunawafunga AC Milani 4-0. Huyu park anacheza Kama lingard Attacking midfield RLC, strength yake kubwa Ni kukaba na stamina, anakimbia dakika zote 90.

Hivyo usikariri mpaka mchezaji awe box to box ndio akabe.
 
Mkuu lingard kwa Ferguson alikuwa anaitwa ji Sung park,Huyu jamaa kwenye mechi 204 ana goli 28 na assist 29 tu. Kwa msimu anakupa goli 6 ama chini ya Hapo na assist hivyo hivyo. Ila goli zake Ni muhimu na kwenye mechi kubwa zaidi ana umuhimu zaidi.

Lingard yupo hivyo hivyo, unafahamu mkuu makombe yote ya ligi tuliocheza Wembley Ni lingard alietupa?
1. Fainali dhidi ya Crystal palace Ni lingard aliefunga goli la ushindi na tukachukua kombe Wembley
2. Fainali dhidi ya Southampton Ni lingard kafunga goli la ushindi na kuchukua kombe wembley
3. Fainali ya community shield Ni lingard kafunga goli la ushindi dhidi ya Leicester Wembley.

Hajafunga fainali dhidi ya Chelsea tu, so fikiria tunacheza fainali 4 mchezaji mmoja anafunga fainali 3 Tena goli la ushindi huoni Mchango wake?

Ukitoa Hapo pia jamaa anafunga Sana big matches,
Jamaa ana goli 17 tu premier league lakini goli 6 Ni against top teams Kama Arsenal, Liverpool na Chelsea.

Wewe unamuona mbaya sababu Hana mtu wa kurotate nae Ila jamaa sio mbaya Kama mnavyosema, na hizo stats zinazosemwa kuhusu jamaa kuto perform toka 2019 ianze ukumbuke lingard aliumia mara 2 Kama sio 3 kipindi Hiko.
Umeeleweka chief
 
Usikariri mpira, Kuna kipindi firminho alikuwa anapewa role hio Liverpool na alikuwa Ni false 9 kabisa,

Carlos tevez 2008/09 ligi ya Uingereza kafunga goli 5 katika mechi 29, Ila still tulikuwa tunamuona mchezaji bora, kwanini? Sababu alikuwa Ni fighter muda wote anasaidia midfield yeye na Rooney, na hayo yanakuwa Ni maelekezo ya Kocha.

Refer Pia ji sung park, 2007 man UTD walikutana na AC Milan tukatolewa nusu tulifungwa 3-0 kule Italy, baadae tulivyokutana nao Tena hao AC Milan Fergie akampanga ji sung park amkabe Andreas pirlo, wote tunajua pirlo Ni deep lying playmaker anakaa na mabeki nyuma Kama defensive midfielder lakini anafanya Mambo yake, ili umkabe huwezi tumia defensive midfield wako inabidi utumie mchezaji mwengine, ndio akawekwa Hi sung park, alikuwa anakaba mpaka kivuli, tunawafunga AC Milani 4-0. Huyu park anacheza Kama lingard Attacking midfield RLC, strength yake kubwa Ni kukaba na stamina, anakimbia dakika zote 90.

Hivyo usikariri mpaka mchezaji awe box to box ndio akabe.

Kuhusu hayo matokeo ya Man U vs AC Milan umekusudia misimu miwili tofauti ama?

Coz 2007 nakumbuka ilikuwa

Home: Man U 3 - 2 AC Milan
Away: AC Milan 3 - 0 Man U
 
Mr. P & Mr.J----Awards.

Mr. P "Hawa Mabwana wamechukua Zawadi sana,Wametawala sana,kila siku wao tu,Tumewachoka sasa.Tunataka sura Mpya"

Mr.J "Lakini kwa sasa sioni Mtu wakuwavuta shati,Naona Mtu Mita kumi kurudi nyuma,kama wanauwezo wapewe hata Miaka 20"

Mr.P " Hawana jipya saizi,yote Marudio,Wakae pembeni,Hapa tunataka sura mpya..Over."

Mr.J "Basi na iwe hivyo..Over"

"I love Football"
Mkuu unataka uniambie hiyo ndio tafsiri ya speech ya the king au?
 
SUTON kuna hawa wamama vinyeo vyao

holjberg ni moto kuliko pogba.

Romeo ni balaa

pogba anaf+*lwa
 
Kukaba sio main role ya Lingard sasa mnapomsifia kwa kuhangaika mpira ukipotea inamaana Lingard ni Box to Box Mid au? Forward hatumii nguvu nyingi kukaba
Mkuu nakubaliana na wewe kwamba traditionally/kwa kasumba, main role ya namba 10 ni kutengeneza nafasi za kufunga na kufunga

Lakini kwa soka la siku hizi ni tofauti, namba 10 anapaswa kutengeneza na kufunga, lakini na kuchafua mipango ya adui punde wanapopata mpira kwenye robo yao (pressing) . Lakini fursa nyingine ni kutengeneza space/nafasi kwa wachezaji wengine waweze kufunga au kutoa pasi za mwisho

Mpira umebadilika sana siku hizi. Hii tumeiona hata kwa makipa na mabeki. Traditionally makipa kazi yao ilikuwa ni kudaka tu, na mabeki kazi yao ilikuwa ni kukaba.

Lakini kwa soka la kisasa, kila mchezaji anatakiwa kuwa active kwa kila role. Ndio maana makocha wa kisasa utasikia wanataka ball playing Goalkeeper au ball playing defender ili kuweza kuanzisha mashambulizi nyuma. Hivyo hivyo na kuzuia, makocha wanataka kuanza kazi ya ulinzi kuanzia mbele kwa adui.

Guardiola aliachana na Joe Hart kwa sababu sio Ball playing Goalkeeper na OGS ameachana/amempa likizo Smalling kwa kuwa sio ball playing defender.

Kuweka kumbu kumbu sawa Lingard alifunga goli mechi ya AC Milan (pre season) hivyo mbadilishe statement. Pia Ole anatuambia kwenye in door game juzi kati, alifunga goli 2.

Mimi binafsi bado nina imani na Jesse lakini ninatamani sana dogo Angel Gomes apewe fursa kwenye role ya namba 10 ili na yeye tuone mchango wake kwani dogo huko chini anakichafua balaa na hata kwenye pre season alionesha uwezo.
 
Back
Top Bottom