Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Wakati tatizo lipo kwa wamiliki na mwajiri wao Ed.
Na Ed atafanya hivyo ili abaki msafi.

Mimi sioni Ole akitoboa kabisa kwa hii timu.

Labda tusubiri kuona Fred anarudi katika hali gani,bado timu ni kisanga.

Tuko vizuri nyuma tu,na ikitokea AWB anapata majeruhi tunarudi kuleee.
 
Mkuu Dimaria alii prove Dunia kwamba ni world class, je alipokuja United kina nani walimfanya ashuke kiwango, Falcao, Sanchez wakishushwa na akina nani n.k

Kwa mfano hapa unasema akina Lingard ndio wanamsababisha Pogba asicheze vizuri. Nikikuuliza Lingard na nani sidhani kama utataja hata wachezaji 4 ambao utawaingiza kwenye hiyo blame game

Swali linakuja, akina Degea, Wan Bissaka, Shaw, Maquire, Lindelof, Tony Martial, Rashy, James je wote wanamuangusha Pogba? Je Pogba pale Ufaransa ana world class players tu wanaomzunguka, Pavard, Giroud, namba 3 wao yule n.k

Je pale Juve alikuwa amezungukwa na wachezaji wote world class players? Je unapotaja mafanikio ya Juve kwa wakati ule, ulikuwa unamtaja kama Pogba ndio ameibeba timu au Pogba was just another Juventus player

Pogba kucheza timu yote duniani, sidhani. Ana hiyo potential, KWELI na pengine mpaka anastaafu atabaki kuwa na POTENTIAL tu, lakini sio timu yoyote duniani anaweza kucheza. City hawezi kupata namba, na Pep alimkataa, Madrid pamoja na Luka kuwa kikongwe sidhani kama anaweza kumvua namba. Barca ndio kabisaa.

Hapa nazungumzia uwezo wake uwanjani na influence yake kwenye timu, hivi vitu ukiviunganisha kuna viungo wengi duniani wanaweza kuwa mbele ya Pogba.

I would rather have Ericksen, Madson, BF, Milinkovic than Pogba in my team
Umeongea vema sana. Mou alipo mbrand huyo kijana kama "kirusi" hakuropoka tu bali ashaona vingi toka kwa huyo mtoto asiyekua!
 
Hivi unajua Chelsea sasa hivi wachezaji wake ni level za championship?

Na msipokaza mtamaliza nafas ya 15? Mkikaza mnaweza kumaliza nafas ya 10
Hahaha ngoja uone mziki tutakao washa this weekend ..natamani ingekuwa tunakutana na nyie lile pazia pale golini na beki ndo uyo Luiz yani mungeoga na mvua za magoli..

Mpaka ifike desemba nina uhakika mutakuwa rank moja na wolves au Everton..

Kila la kheri Chelsea
 
Umekosea kuweka neno "yeyote"... rekebisha
Apo sawa lakini ukweli ni kwamba Chelsea tuna vijana ambao wanaingia moja kwa moja tena bila kupingwa kwenye first XI ya Ole ...

Mcheki Mount, ata Rashid anapigwa bench apa jpo yeye ana uzoefu na ligi.

Mcheki Kova apo ata Pogba anaeza pigwa benchi.

Mcheki Tammy ..Marshal apa anaeza kaa bench

Kwa upande Beki muko vizuri ..ila Magwaya anakalishwa vizuri tu na Zouma

Apo kati ndo usiseme Joghihno, Kante nani wa kuwaweka benchi apo Man u? Jibu ni hatuna..

Kepa anaeza mkompiti vizuri tu De gea na soon anachukua kipa namba moja Uspain..

Kila la kheri Chelsea
 
Hivi unajua Chelsea sasa hivi wachezaji wake ni level za championship?

Na msipokaza mtamaliza nafas ya 15? Mkikaza mnaweza kumaliza nafas ya 10
Hahaha wewe juzi unapanga kikosi cha kitoto unapigwa tatu na Liverpool ..sisi tulipanga hao unaowaita championship players na wakakipiga fresh Dakika 120 supercup alafu unajiona una kikosi cha maana.

Hii Arsenal haitusumbui akili kabisa ..hata musajili vip bado mutaendelea kusugua kweny ligi tu. Tena muna bahati sisi hatujasajili maana Pepe angeshatua Darajani..

Kila la kheri Chelsea
 
Apo sawa lakini ukweli ni kwamba Chelsea tuna vijana ambao wanaingia moja kwa moja tena bila kupingwa kwenye first XI ya Ole ...
Mcheki Mount, ata Rashid anapigwa bench apa jpo yeye ana uzoefu na ligi.
Mcheki Kova apo ata Pogba anaeza pigwa benchi.
Mcheki Tammy ..Marshal apa anaeza kaa bench
Kwa upande Beki muko vizuri ..ila Magwaya anakalishwa vizuri tu na Zouma
Apo kati ndo usiseme Joghihno, Kante nani wa kuwaweka benchi apo Man u? Jibu ni hatuna..
Kepa anaeza mkompiti vizuri tu De gea na soon anachukua kipa namba moja Uspain..
Kila la kheri Chelsea
Hawazidi wa'4 hao wengine ni level ya DANIEL JAMES wetu.
Yaani Chelsea kupigwa 4-0 na hao akina Rashid we hukuona mtakavyoteseka season hii? ...
Huyo Kepa anafukuzana na kipa wa West ham kuruhusu magoli... labda awe kipa namba moja wa Spain ya London.
Zouma anamueka benchi P.JONES kule nje kwenye benchi kusogeza matako foleni ya sub.
 
CARABAO CUP FIXTURE

  • Wolves v Reading
  • Oxford United v West Ham
  • Watford v Swansea City
  • Brighton v Aston Villa
  • Sheffield United v Sunderland
  • Colchester United v Tottenham
  • Portsmouth v Southampton
  • Burton v Bournemouth
  • Preston v Manchester City
  • MK Dons v Liverpool
  • Manchester United v Rochdale
  • Luton v Leicester
  • Chelsea v Grimsby/Macclesfield
  • Sheffield Wednesday v Everton
  • Arsenal v Nottingham Forest
  • Crawley Town v Stoke City
 
Bado najiuliza kwanini Uingereza wamekimbilia kufunga dirisha la Usajili mapema hivi.

Sababu ni zipi labda?
Klabu zilipiga kura zikataka dirisha litafungwa kabla ligi haijaanza
 
Katika kipindi hiki ambacho hatuna Lukaku na hakuna usajili uliofanyika kuziba pengo lake,kusema Sanchez hana umuhimu ni kucheza kamari.

Timu haina namba tisa halisi, Martial na Rashford hawa sio #9 halisi. Sanchez alicheza kama #9 kwa mafanikio pale Arsenal.

Fikiria Martial ameumia,hatokuwepo mchezo ujao. Mchezo ujao aumie tena Rashford awe nje kwa miezi kadhaa, hapa si unamaliza nafasi ya 13? Utamtegemea Greenwood kama mshambulizi pekee akufanye umalize top4?

Hawa watoto sio wa kutegemea kwa kiasi kikubwa kama unavyotaka tufanye mkuu. Greenwood mpe dakika 10 za mwisho wakati unaongoza,akiingia kwa presha ndio mipira itakuwa ikimgongagonga mpaka anachanganyikiwa.

Nasubiri, mpaka December Ole atakuwa ameshaanza kusukumiwa jumba bovu.
Yani mkuu Rashford na martial sio namba 9 halisi kuliko Sanchez?

Japo Sanchez ndio alikuwa mzuri na kiwango kikubwa Ila sio namba 9, anachezeshwa tu hio namba Ila sio natural position yake. Siku zote kuanzia udinese, Barcelona Hadi arsenal alikuwa anatokea pembeni.

Na sisi tulikuwa tunataka ole atoe deadwoods kamtoa Lukaku, Sanchez, Sasa Hivi hata Jones na Smalling benchi tu hawakai, kwenye picking order Tuanzebe yupo juu Yao, si ndo Ole anafanya kazi yake?

Hizi mechi 2 za wolves na palace zisitufanye tupanick, mechi zote tumecheza vizuri zaidi ya wapinzani na Ni bahati mbaya tumepoteza point kwa kukosa penalty kila mechi, pamoja na maamuzi mabovu ya marefa.

Timu yetu ipo muelekeo mzuri na kutokea Hapa Sasa tutaanza kusajili kwa ku improve timu na sio kubadili wachezaji kama miaka iliopita.
 
Back
Top Bottom