Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Chelsea mmepata pa kusemea
Nasikia dogo mwenyewe ndio huyu
IMG_20190825_051416_298.jpeg
 
Hawa Man si wakamchukue Samatta Genk?Hakuna wafungaji pale,hakuna viungo wabunifu.Timu hii ni ya kushika nafasi za kati kwenye msimamo wa ligi
 
OGS anarudia kufanya tactical mistake mechi ya tatu mfululizo na kibaya zaidi yeye bado hajaona kama ni tatizo

Mechi zote ametumia mfumo wa 4-2-3-1 ambao unamfanya Pogba(creative player) anacheza nyuma na timu ina-struggle kutengeneza nafasi licha ya kumiliki mpira kwa sababu anakuwa anacheza kama DM .Game vs Chelsea tulikuwa na advantage alinza Pereira ambaye yeye kiungo so muda mwingi alikuwa anarudi kusaidia kukaba kukamfanya Pogba akawa free na kutengeneza nafasi nyingi ,mechi zilizofuatia badala ya Perreira ameanza James ambaye sio kiungo ni winga so harudi kusaidia kukaba na kuwapa mzigo mzito viungo (Pogba,McTominay) na tumecheza na timu zinazocheza mpira wa nguvu kwa sasa James anafaa awe anaingia second half.
Pia wakati mwingine anapaswa kuswich 4-3-3 ambayo aliicheza msimu uliopita na kujaribu kuwapa nafasi Fred na Matic
Belo, wanavyosema wenye timu yao humu ndani ni kwamba huu mfumo wa 4-2-3-1 ndio uliokuwa unatupa mafanikio kwenye mechi zetu za kujipima nguvu ikiwemo dhidi ya milan brothers, spurs na wengineo hivyo basi kuna uwezekano mkubwa wa kuendelea kutumika kwa mfumo huu. badala ya ule tuliouzoea wa 4-3-3 kwa takribani misimu mitatu iliopita.

unajua kwa kiasi kikubwa sana wengi wetu hatufahamu lolote linalotendeka ndani ya klabu kwa sababu hatuna uwezo wa kuaccess taarifa nyeti zinazoihusu klabu matokeo tumeishia kuwa watabiri kwa yale yanayo na yatakayotendeka mbeleni kwa kufuata zaidi mdundo wa vyombo vya habari.
  • kwa kutumia huu utabiri acha niamini ya kwamba bwana OGS alitegemea ingizo la kiungo mwengine mshambualiaji mfano wa eriksen, bruno fernandez au maddison atakayekuja kucheza namba 10 eneo ambalo tunamtumia jesse lingard kwa msimu huu baada ya kuswitch mfumo wa 4-2-3-1 tokea preseason, lakini ndio hivyo kama kawaida kwa mara nyengine tena ed woodward na rafiki yake matt judge walishindwa kufanikisha usajili wowote wa kiungo huku wakifahamu fika tumempoteza ander herrera na marouanne fellaini.
  • kwa kutumia utabiri huo huo acha pia niamini ya kwamba OGS huenda ndiye aliyefelisha baadhi ya sajili za wachezaji mfano wa bruno fernandez kwa hoja ya kukosa DNA zitakazomwezesha kuipigania klabu kwa jasho lake haijalishi kama atalipwa hela ndogo na kumuona jesse lingard ndiye kiungo sahihi zaidi kucheza namba 10 huku paul na scott wakicheza deep midfields eneo ambalo tumekwishazoea tukiwatumia herrera na nemanja matic.
kuna mwanadamu mmoja tu ambaye huenda akambadilisha fikra bwana ole ili arudishe tena mfumo wa 4-3-3 ambao unamwezesha paul pogba kucheza juu zaidi akitokea upande wa kushoto ambao ndio upande tunaoutegemea zaidi kupika mashambulizi na si mwengine isipokuwa ni fred the red.
kama fred atacheza vizuri pindi atakapopewa nafasi basi tutaswitch mfumo wa 4-3-3 kwa sababu OGS hana uwezo wa kumweka nje paul pogba ili apate kuendeleza mfumo wake wa 4-2-3-1.

pia tufahamu si nemanja matic, perreira wala fred atakeyekuwa na uthubutu wa kumfanya OGS abadilishe msimamo wa kifikra kwa kumweka nje scott mctominay kwenye eneo la kiungo mkabaji kwa sababu hao wote hawana DNA za kimanchester ukilingansha na scott hivyo basi wapenzi wa nemanja matic kwa msimu huu mujiandae kisaikolojia.
OGS na benchi lake wanamuona scott mctominay kama ndiye roy keane wetu mpya.​

  • fred ndiye aliyeshikilia ufunguo utakaomwezesha OGS abadili style ya kiuchezaji mara kwa mara msimu huu.
  • fred ndiye aliyeshikilia ufunguo wake mwenyewe utakaomwezesha kufungua au kufunga chumba chake cha kuhifadhia vifaa pale AON complex a.k.a carrington, kama atacheza vizuri basi msimu ujao ataendelea kuwepo klabuni ila kama ataendelea kucheza ovyo kwa ninavyomtazama solskajer na hii recruitment yake ya karne ya 20 aliyokuja nayo huenda nafasi yake rasmi akapewa gardner au yule mjinga anayetokea newcastle united anayeitwa sean longstaff
1566708576460.png
 
√Huu ni utani..tunafungwa na Palace nyumbani..WTF

√Kuna watu wanasema Pogba kisa hajazungukwa na World Class Players basi ni haki yake yeye kupoteza poteza mipira na kufanya madoido madoido mengi yasiyokuwa na msingi..we all know Pogba uwezo anao ila kuna muda huyu jamaa anaicost timu na pia sababu ya yeye kuzungukwa na average player haiwezi kustand out..

√McTominay anapiga kazi ila bado sio standard ambazo zinahitajika kwenye DM kama kweli timu hii ipo serious..same applies to Lingard..Hatuitaji mtu anayepiga tu kazi bali mwenye uwezo wa kusoma mchezo na kufanya vitu tofauti ili kuinfluence matokeo.

√The more you create the more the chance to score..timu haitengenezi nafasi za kueleweka magoli yanatoka wapi??..ukichanganya na straika wetu Martial ambaye ni kama anacheza soft soft sahau kabisa magoli.

√Kipindi cha mwishoni cha Mourinho pale United kabla ya kutimuliwa alikuwa ameshapoteza imani na Lukaku,Rashford alianza kutumika na Ole pia akaendeleza kilekile..Lukaku kuondoka kwangu sio big deal,,ishu ni yeye kuondoka kisha tunampa jukumu Martial la kutufikisha mawinguni...

√Daniel James naona ni bora awe anatokea kushoto atleast kuna kitu anakionyesha akitokea huko

√Five more games,and Shi.t Perfomance kama leo,then the season is over


√Falsafa ya Ole ni ipi haswa au ni mapema kuuliza hili swali??
Dah na mimi ninechoka Mkuu, yaani boko ametoa Pogba lawama wanapewa wenzake eti sio world class players. Na Pogba sio mara ya kwanza kupoteza mpira either ukai cost timu au ukakaribia kui cost timu.

Na kutokana na hilo mimi naona it's not a good idea kumchezesha Pogba nyuma yeye na Scot, achezeshwe kule mbele kama ilivyokuwa msimu uliopita OGS alipopewa timu. Kuchezeshwa nyuma, inasababisha anapopoteza mpira kuwa na risk zaidi ya kufungwa goli kuliko akichezeshwa mbele

Lingard pia anapaswa kubadilika especially kwenye kuimprove his attacking ability (creating chances and scoring goals). Kutokana na uwezo wa Gomes au Mata katika kutengeneza nafasi kuliko Lingard, na kutokana na Cristal Palace kutokuwa timu kubwa yenye kuleta hatari sana, sikuona sababu ya kumuanzisha Lingard na ukawaacha wachezaji creative zaidi yake.

Lukaku was still clinical compared to Tony na Rashy. Ninakubali huko duniani wapo kweli wachezaji clinical kuliko Rom lakini si wengi kama watu wanavyosema. Hata yule Inaki wa Bilbao sio clinical kiivyo, na asingeweza kufanya jambo tofauti sana na akina Tony. Kwa sasa duniani sidhani kama kuna ma strikers zaidi ya 15 wanaomzidi Lukaku uwezo wa ku score.
 
Back
Top Bottom