Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

mkuu nimeielewa hoja yako unayoisimamia ila sielewi kwa nini hao wengine wameshindwa kuielewa hoja yako.
umejaribu kuizungumzia man city hii ilioasisiwa miaka 10 iliopita na sheikh mansouri na si ile ilioasisiwa takribani miaka 100 iliopita.

man city hii iliosisiwa miaka 10 hata mimi nakubaliana na wewe ya kwamba wamewekeza miundo mbinu bora sana kwenye sekta ya kusaka vipaji na kwa hali inavyokwenda ndani ya miaka 10 ijayo upo uwezekano wa ndugu hawa wawili kuwa level moja au kaka mkubwa kuzidiwa kwa uzalishaji wa wachezaji kutoka shule wanazozisimamia.

jadon sancho = dortmund
brahim diaz = real madrid
phil phoden = mrithi wa david silva
denis suarez =
amerudi barcelona kutoka arsenal
iheanacho kelechi = leicester city​
Asante, walau kuna mtu ameelewa what i am talking about, wacha Glazer na woodward waendelee na huu upuuzi, hawa wahumu nao watakuja kuelewa what am talking about.

We can laugh about City, but in reality we are jelous of them kwa sababu wana mtu ambae ame invest heavily in football sisi tuna mtu ambae haweki investment but is ripping from our club.

Sasa ivi Fans tunaishia kuzungumzia historia, mambo ambayo yalikuwa yanafanywa na fans wa liverpool.

Najaribu kuwaelewesha kuwa shida ya City ni kwamba makinda hawana game time ndio maana Academy ya United inaonekana inazalisha sana, mfano, solkjear kajipanga na watoto wa academy kibao kuwachezesha, wakati city wanao vijana wa academy lakini hawana time ya kuwapa uwanjani. City wanataka wachezaji waliokwisha iva saiv, they are on the road to build an empire, na guardiola akiendelea kukaa pale, tutashuhudia dream yao ikifanikiwa.

Nakushukuru kuwatajia wachezaji waliotoka City Academy.....

They will realize soon, and i hope it will not be too late!

Watu wanafikiri labda tunataka kuona club ikichukua ubingwa tu, no, tunataka kuona ushindani, kuiona timu ina fight for title hata wakikosa, unajua kuwa dah vijana wamepiga kazi hawa ku give up.

Mtu anakwambia Pogba karudi MUFC kwa mapenzi yake.... 😀 Halafu anatoa statement kuwa anataka challenge somewhere else!!!

Wenye mapenzi na MUFC walibaki hata baada ya matusi ya Babu Fergie....
 
Alirudi MUFC kwa sababu ya mapenzi yake ya Club na aliondoka MUFC kwa sababu ya Mapenzi yake kwa Club, au sio? Yaani mpaka anabembelezwa bado kaondoka halafu unatwambia ana mapenzi ya Club.

Yap Mina Raiola alisema ivi au sio

"
‘For me I have been for three years in Manchester and have been doing great, some good moments and some bad moments, like everybody. Like everywhere else. ‘After everything that happened this season, with my season being my best season as well… I think for me it could be a good time to have a new challenge somewhere else. I am thinking of this: to have a new challenge somewhere else.’

"

- Kasper Schmeichel - Leceister
- Angelino - PSV
- Ben Mee - Burnley
- Jason Denayer - Lyon
- Kirena Trippier - Tottenham
Just to name some...

As i said, ishu ya Man city ni kutowapa makinda mda uwanjani.

Kama unajua unajua tu na uutakapoenda uta perform vizur? Coutinho aliperform vizuri Liverfools, kaenda Barca tafrani tu. Hii Logic ni nonsense.... kwamba eti kama unajua unajua tu?
Kwa hiyo wa Man United unataka wa tangu 2013

Lakini wa Man City unataja wa tangu Adam na Eva
 
mkuu unataka kutuambia ya kwamba arsenal hawakuhitaji mlinzi wa kushoto?
arsenal hawakuhitaji mlinzi mwenye uzoefu kama david luiz?
arsenal hawakuhitaji kiungo mwenye uwezo kama alionao dani ceballos?
arsenal hawakuhitaji kiungo mshambuliaji na mfungaji mfano wa pepe?

pepe licha ya kufunga magoli mengi msimu uliopita pia ndiye mchezaji wa pili kwa kuhusika na utengenezaji wa magoli kwenye ligi ya ufaransa, kwa viwango vya wachezaji tulionao yupo mwenye uwezo wa kumweka nje pepe?
yupo mchezaji mwenye uwezo wa kumweka nje lacazette na aubameyang?
ukimuondoa pogba yupo kiungo mshambuliaji mwenye uwezo wa kumweka nje ozil huyu aliyeshuka kiwango na hamasa ya upambanaji?

kosa kubwa walilolifanya arsenal ni kumsajili mchezaji kwa fedha nyingi halafu wakambakisha kwa mkopo, dhambi hii ndio itakayowatesa kwa sababu mpaka dirisha linafungwa wameshindwa kupata mlinzi mwengine wa kati mwenye uwezo?

mkuu usisahau msimu uliopita arsenal walimaliza juu yetu kama bado kumbu kumbu zangu zipo sahihi.
Mkuu hapo kuna mambo 2,unaweza kununua mchezaji kuziba pengo ambalo lilikuwepo lakini je hiyo inakuwa ni upgrade au ni kuziba pengo tu ilimradi?

Kwa mfano Man United tulikuwa tunahitaji beki wa kati, je tungemchukua David Luiz ungejihisi comfortable kama tulivyomchukua Maquire? After all David Luiz sio addition ila ni replacement ya Koa scienly ambaye akiwa fit ni mzuri kuliko Luiz

Kwa Tierney nimewapongeza, japo sio premier League proven. Lakini sidhani kama amemzidi kiwango sana yule baunsa wao au Monreal.

Kwa Pepe ndio wamelamba dume for sure
 
sipingi sera ya kuwapa nafasi ya kucheza timu kubwa wachezaji wanaotokea kwenye academy, tatizo ni kwamba hii timu kubwa tulionao ina matatizo mengi ambayo si rahisi kutatuliwa na wachezaji wachanga.

kama tungelifanya usajili wa nguvu kama ule wa real madrid msimu huu halafu tukaingiza damu changa kutoka academy basi nisingelikuwa na khofu yeyote ya kufanya vibaya kwa timu yetu msimu huu.

hawa vijana wetu mfano wa tahit chong, greenwood, gomez wangeliufurahia zaidi mpira wao kama ingelikuwa wamezungukwa na mafundi mfano wa bruno fernandez, pogba, pepe, james madison, harry kane, ndombele,thomas mounir.

Mfumo huu ndio aliokuwa anautumia sir alex ferguson wa kuingiza damu mpya kwenye kikundi cha mafundi wenye kujielewa ndio maana klabu ilifanikiwa kupata faida ya vijana kwa muda mfupi mfano wa ronaldo, scholes, neville brother, beckham n.k
unadhani wayne rooney, beckham, scholes, ronaldo na wengineo ingeliwachukua miaka mingapi kwa kikosi hiki tulichonacho kuufuahia mpira wao?

jaribu kufikiria unazungukwa na ashley young, phil jones, jesse lingard, darmian, rojo kwenye timu unadhani itakuwa ni rahisi kukuza kiwango chako?

angalia mfano mwengine wa barcelona , msimu wa mwisho wa rijkaad barcelona tuliwatoa nusu fainali kwa goli la mtakatifu paulo, hii ina maana ya kwamba barcelona hawakuwa na timu mbovu na ndio maana guardiola msimu wake wa kwanza alifanya mabadiliko madogo sana ya usajili na kimfumo.

barcelona ile ilikuwa na etoo, henry, hleb, marquez, pique, abidal, toure, xavi, iniesta ndio maana ilikuwa ni rahisi sana kwa wachezaji wenye vipaji mfano wa bosquet, pedro, pique kukuza viwango vyao kwa sababu walizungukwa na wachezaji watakaowafanya waufurahie mpira wao kwa uhuru tofauti na timu yetu ya sasa iliojaa maiti wa soka.
Mkuu huwezi kuwa na sera ya Galacticos halafu ukaweza ku apply na sera ya kutumia wachezaji kutoka academy wakang'ara

Mfano Chong atang'ara vipi ukimletea Pepe (japo mimi pia nilitamani aje), Greenwood atapata vipi playing time ukimletea Lukaku mwingine, Gomes atang'ara vipi ukimletea Griezeman

Diego Dalot mwenyewe tulikuwa hatutaki aletewe Wan Bissaka kwa sababu hizo hizo

Angalia Madrid kwa miaka 10 hii, kuna makinda hata 5 wametokea academy yao na sasa wanang'ara duniani? Labda unikumbushe.

Ndio maana nasema huwezi kuwa na vyote viwili kwa wakati mmoja, kusaini wachezaji wakubwa 5 au 6 kwa wakati mmoja na wakati huo huo kuendeleza vipaji kutoka academy.

Mimi binafsi sikumbuki ni lini mara ya mwisho SAF alisajili wachezaji 4 wakubwa kwa mkupuo. Akijitahidi sana ni wawili halafu anaongezea na potential mmoja au wawili kisha maisha yanaendelea.
 
Mkuu hapo kuna mambo 2,unaweza kununua mchezaji kuziba pengo ambalo lilikuwepo lakini je hiyo inakuwa ni upgrade au ni kuziba pengo tu ilimradi?

Kwa mfano Man United tulikuwa tunahitaji beki wa kati, je tungemchukua David Luiz ungejihisi comfortable kama tulivyomchukua Maquire? After all David Luiz sio addition ila ni replacement ya Koa scienly ambaye akiwa fit ni mzuri kuliko Luiz

Kwa Tierney nimewapongeza, japo sio premier League proven. Lakini sidhani kama amemzidi kiwango sana yule baunsa wao au Monreal.

Kwa Pepe ndio wamelamba dume for sure
kwenye comment yangu ulioinukuu nimezungumzia kosa walilolifanya arsenal la kununua mlinzi wa kati kwa bei kubwa baadae wakakubali kipengele cha kumruhusu abaki klabuni kwake kwa mkopo wa mwaka mmoja, jeuri kama hiyo walipaswa wafanye klabu kama vile juventus iliobarikiwa utajiri wa mabeki wa kati wenye viwango na si arsenal inayoadhibiwa kila msimu kwa kukosa walinzi mahiri wa katikati.

kuhusu tierney sijawahi kumuona lakini ujio wake kama ataonyesha kiwango itakuwa ndio chanzo cha kumrudisha kolasinac eneo la mlinzi wa kati na si kuendelea kucheza upande wa kushoto.

unamuonaje dani ceballos?
 
Traffic Manchester
xcsc4dtafff31.jpg
 
Mkuu huwezi kuwa na sera ya Galacticos halafu ukaweza ku apply na sera ya kutumia wachezaji kutoka academy wakang'ara

Mfano Chong atang'ara vipi ukimletea Pepe (japo mimi pia nilitamani aje), Greenwood atapata vipi playing time ukimletea Lukaku mwingine, Gomes atang'ara vipi ukimletea Griezeman
mkuu kama ni hivyo basi hakuna faida ya klabu kufanya usajili wa wachezaji kama ishu ni kuhofia young players kutoka academy hawatopata game time ya kutosha, hata huyo maguire kwa mujibu wa hoja yako ujio wake utasababisha tuanzebe na vijana wengineo kutoka academy watumie muda mwingi kukaa benchi au kucheza mechi za under 23.

nilichokuwa nakihitaji mimi ni kuona kwanza tunaziba madhaifu yetu kwa kufanya usajili wa sehemu zote zenye ufa baadae ndio tuwape nafasi vijana ila alichokifanya OGS msimu huu ni kuwabebesha mzigo wa misumari vijana wadogo wasiokuwa na uzoefu wa mapambano kwa kuwategemea wawe wazibaji wakubwa wa nyufa zetu.

nitatoa mfano mwengine wa manchester city tumeona timu yao jinsi ilivyoimarika kila eneo kiasi ambacho hata ikitokezea david silva amewekwa benchi nafasi yake inazibwa vizuri na kijana phil Foden kutoka academy.

kwa nini phil foden anacheza vizuri?
jibu ni rahisi tu ni kwamba pindi akiwa uwanjani hujikuta amezungukwa na mafundi wa mpira kila pembe jambo ambalo humpunguzia presha ya kuwa tegemeo kwenye mechi husika.

lakini ukija kwetu sisi unapomuanzisha angel gomez au greenwood kwenye kikosi kinachoundwa na dead players mfano wa ashley young, fred,jones, perreira, matic na wengineo wanajikuta wanabeba mzigo mkubwa sana wa matumaini ya kuwa wabebaji wakubwa wa timu kimatokeo.

nikatoa mfano wa barcelona nyakati ambazo kwa muda tofauti wanawakuza kisoka sergio bosquets, messi, gerrard pique,pedro, sergio roberto, thiago alcantara, cristian tello, bojan krkik na wengineo hawakuwabebesha majukumu sana kwa sababu walikuwepo wachezaji watakaowafanya ile presha ya kuibeba timu isiwepo kwenye mabega yao.
yupo henry, etoo, gaucho, deco,guily, abidal, toure, puyol, marquiz,xavi, iniesta, david villa, zambrotta, dani alves,alba na wengineo kwa nini usiufarihie mpira wako?

kama ni young players kwa nini usiufurahie mpira wako kwenye timu inayozungukwa na kevin debruyne, gundogan,aguero, sane, sterling, silva double, concelo, mendy,otamendi, walker, aguero?

kama ni young player kwa nini usiufurahie mpira wako kwenye timu inayoundwa na roy keane, rooney, scholes, giggs, ferdinad, vidic, evra, nistelrooy na wengineo?
 
tulia wewe ..Hivi hii manure tangu asepe mzee fargie kuna mchezaji aliyefikisha goli 20??

Hii manure wataanza kwa kasi sana ila baada ya gemu kama saba iv au nane wataanza kupotena apa..Wewe hauna Lukaku, hauna Herrera una Masho na uyo Rashid unategemea kushindana na big giants kama Chelsea au Liverpool. Uyu ole akatizi October atakuwa amefukuzwa.
Unadiriki kuitaja Chelsea kama giant msimu huu😂

Kwanza nianze kwa kusema nashukuru kama umejua hizi game saba za mwanzo hakuna atakae pona wakiwemo chelsea,

Pili nikukumbushe tuu baada ya mechi saba hatutabadilisha kikosi, moto ni ule ule

Tukutane kesho Ollachuga Oc
 
Washabiki wa man utd mmekata tamaa mapema hata ligi hamjacheza game moja. Tulieni msisahau this is EPL anything can happen. Hii ligi haieleweki wakuu unaweza shangaa umdhaniae atashinda kumbe ndo anayefungwa. Guardiola kachukua makombe mfululizo bila bado mi naamini EPL haina mchawi wake hata yeye na klopp watachemka tu subiri ni muone cha muhimu kila mtu ashinde zake za nyumbani OGS a najua anachofanya muacheni mpeni muda hawa watoto wake wanaweza kufanya maajabu bado na kuwaacha mdomo wazi msiamini.

Remember this is EPL ANYTHING CAN HAPPEN. liverfools wasiwatishe muachieni OGS afanye kazi yake tutamhukumu December.
Yani mashabiki wako bize wanalialia tuu kama vitoto vya ndege,
Nani amewaambia tunataka kufika ilipo Liverpool?

Lengo ni kufanya vizuri na kushinda mataji, wimbi la mashabiki wa timu pinzani kuja kulinganisha timu zao na timu yetu limechukua akili za wenzetu kiasi kwamba na sisi tuko bize tunalinganisha timu yetu na Liverpool, Barcelona, madrid, man city

Tunasahau kama kuna sterling wa man city hawezi kuwepo na wa man u, kwamba wacheze mchezo unaofanana, kila mtu atumie raslimali alizo nazo, mwisho wa siku tukumbuke panga na shoka vyote vina ncha kali na vinaweza kukata mwanzi ni suala la utumiaji tuu.

Kwani goli akifunga greenwood mwenye miaka 17 na akifunga sterling si bado ni goli?
 
mkuu kama ni hivyo basi hakuna faida ya klabu kufanya usajili wa wachezaji kama ishu ni kuhofia young players kutoka academy hawatopata game time ya kutosha, hata huyo maguire kwa mujibu wa hoja yako ujio wake utasababisha tuanzebe na vijana wengineo kutoka academy watumie muda mwingi kukaa benchi au kucheza mechi za under 23.

nilichokuwa nakihitaji mimi ni kuona kwanza tunaziba madhaifu yetu kwa kufanya usajili wa sehemu zote zenye ufa baadae ndio tuwape nafasi vijana ila alichokifanya OGS msimu huu ni kuwabebesha mzigo wa misumari vijana wadogo wasiokuwa na uzoefu wa mapambano kwa kuwategemea wawe wazibaji wakubwa wa nyufa zetu.

nitatoa mfano mwengine wa manchester city tumeona timu yao jinsi ilivyoimarika kila eneo kiasi ambacho hata ikitokezea david silva amewekwa benchi nafasi yake inazibwa vizuri na kijana phil Foden kutoka academy.

kwa nini phil foden anacheza vizuri?
jibu ni rahisi tu ni kwamba pindi akiwa uwanjani hujikuta amezungukwa na mafundi wa mpira kila pembe jambo ambalo humpunguzia presha ya kuwa tegemeo kwenye mechi husika.

lakini ukija kwetu sisi unapomuanzisha angel gomez au greenwood kwenye kikosi kinachoundwa na dead players mfano wa ashley young, fred,jones, perreira, matic na wengineo wanajikuta wanabeba mzigo mkubwa sana wa matumaini ya kuwa wabebaji wakubwa wa timu kimatokeo.

nikatoa mfano wa barcelona nyakati ambazo kwa muda tofauti wanawakuza kisoka sergio bosquets, messi, gerrard pique,pedro, sergio roberto, thiago alcantara, cristian tello, bojan krkik na wengineo hawakuwabebesha majukumu sana kwa sababu walikuwepo wachezaji watakaowafanya ile presha ya kuibeba timu isiwepo kwenye mabega yao.
yupo henry, etoo, gaucho, deco,guily, abidal, toure, puyol, marquiz,xavi, iniesta, david villa, zambrotta, dani alves,alba na wengineo kwa nini usiufarihie mpira wako?

kama ni young players kwa nini usiufurahie mpira wako kwenye timu inayozungukwa na kevin debruyne, gundogan,aguero, sane, sterling, silva double, concelo, mendy,otamendi, walker, aguero?

kama ni young player kwa nini usiufurahie mpira wako kwenye timu inayoundwa na roy keane, rooney, scholes, giggs, ferdinad, vidic, evra, nistelrooy na wengineo?
Kuhusu Tuanzebe ipo tofauti na context ninayoongelea mimi. Kwa kuwa ameleta mtu mwenye quality na wanaondoka watu wenye experience lakini bado hawajawa na quality Man Utd anayoitaka

Tuanzebe bado hajawa tayari, lakini lazima atapata game time. Na ili kuhakikisha anapata game time ndio maana Man Utd Baada ya kumleta Maquire sasa hivi kwa udi na uvumba wamemuweka sokoni Rojo na Smalling (japo mimi nilitaka iwe Rojo na Jones) sokoni. Yote hiyo ni kumpa nafasi Tuanzebe

Lakini hii ya kutaka kununua timu nzima huwezi saidia vijana wanaokuja. Ndio maana hujawahi kuona Barca wananunua karibu galactico nusu timu
 
Ningekuwa niko kwenye nafasi ya ED.

Ninapomfukuza kocha, kocha anaefuata lazima awe anatumia falsafa kama ya kocha aliyepita.

In short, unaajiri kocha anaendana na falsafa ya timu. Ndio maana si rahisi barca kumuajiri Mou kama kocha.

Van gaal aliwahi kusema ,wakati anajadiliana na uongozi wa Man u, kuhusu kupewa kibarua. Football matters hazikupewa kipaumbele.
Hili ni tatizo kubwa,
Kama huyo kocha atakuwa free.

Makocha wa maana wote wana timu. Labda ummchomoe kwenye hiyo timu.
 
Mim Nina uhakika kama siyo point sita basi ni nne tutazibeba kutoka man united..

Arsenal tutazuia point nne tu.

Spurs tutazuia point tatu.

Man city point mbili.

Liverpool point mbili.

Top six itakuwa imekamilika, uku kwengine tutakuwa tunakichafua tu hakuna wa kutuzuia mkuu.

Tukutane mwisho wa msimu
Rahisi kuongea kama konda wa kike.
 
Back
Top Bottom