lukesam
JF-Expert Member
- Feb 23, 2015
- 13,198
- 28,080
Bado naamini tunayo nafasi,ila asiumie mchezaji tu. |
Bado naamini tunayo nafasi,ila asiumie mchezaji tu. |
Nilijiandaa kisaikolojia kupokea matokeo yoyote ligi ikianza baada ya kuona harakati zetu za usajili zilijaa tetesi za magazetini bila uhalisia wowote.msimu uliopita marcus rashford na antony martial kwa pamoja wamefunga magoli 20 kwenye ligi kuu ya uingereza kama nitakuwa nipo sahihi.
ili tusolve tatizo la ushambuliaji mabwana hao wawili watalazimika kutufungia magoli takribani 40 kwenye mechi 38.
je uwezo huo wanao?
naomba tuzungumze mambo ya soka tukiweka mbele uhalisia na si matumaini ya uongo ya kumpa ahueni mgonjwa mahututi aliyebakisha nusu saa kabla hajakata roho.
nilisema na nitaendelea kusema timu yetu tulipaswa kwanza tuongeze mshambuliaji mwengine atakeyetufanya tuwe na safu kali ya ushambuliaji kama waliokuwanayo liverpool au man city, tulichokifanya sisi ni kumuondolea mgonjwa kifaa kilicho chakaa cha kumsaidia kupumua bila ya kuwa na mipango ya kutafuta kifaa chengine.
sielewi kwa nini timu tajiri kama manchester united wanazidiwa na klabu ya arsenal kwenye harakati za usajili wa mchezaji hodari kama pepe, jamani huyu pepe alipaswa aje manchester united ili aongeze nguvu safu ya ushambuliaji na si arsenal. nyakati za SAF nimewahi kushuhudia timu yetu ikiwa na washambuliaji wanne mahiri kwa miongo miwili tofuti, sielewi kwa nini nyakati hizi imekuwa ngumu.
andy cole + dwight yorke + sheringham + solskjaer
nistelrooy + rooney + saha
rooney + tevez + berbatov + ronaldo
rvp + rooney + hernandez
leo hii tunaianza ligi tukiwa na mshambuliaji asiyekuwa na uhakika wa kufunga magoli 20 kwa msimu halafu kuna wadau wanajipa matumani ya uongo eti tutafanya vizuri.
kuna wadau wameshukuru kuondoka kwa lukaku huku wengine wakimdhihaki kwa sababu ya mwili wake kuwa na uzito mkubwa akiwemo gary neville, lukaku huyu mzito mwenye kg 300 ana uhakika wa kukupa magoli 20 kwa msimu haijalishi timu ipo kwenye kiwango kibovu kama ilivyokuwa msimu uliopita.
kupitia kurasa hii mutakuja kumuomba radhi romelu lukaku kwa aibu na fedheha itakayowakumba.
mume wetu wa soka wolverhampton anatusalimia
kuhusu winga wa kulia bado naikumbuka comment yangu nilioiandika humu ndani baada ya kutangazwa usajili wa daniel james.mkuu cooper ameongea wish ya OLE ni kama ya mashabiki, alitaka midfielder creative na winger wa kulia kabla ya dirisha la usajili, ila woodward ndio amefeli kudeliver,
![]()
Solskjaer explains how Man Utd plan to replace Romelu Lukaku
Romelu Lukaku left Manchester United in a deadline day switch to Inter Milan and has not been replacedwww.mirror.co.uk
Pereira yupo smart sana, sijui kwa nini yupo underrated
Kuna mistake huwa anafanya akichezeshwa mahala pa herrera mfano game ya burnley pale old trafford
mkuu unataka kutuambia ya kwamba arsenal hawakuhitaji mlinzi wa kushoto?Ukiniambia mimi ni rank timu zipi zilizosajili vizuri (kwa top six) kulingana na mahitaji yao, wa kwanza nitampa Man City, wa pili Spurs na wa tatu atakuwa United kisha Arsenal na Liverpool. Chelsea wao hawakusajili kabisa
Hii ni official mkuu??Msimu huu martial ndo atasimama namba tisa na mimi naamini atafanya vizuri zaidiView attachment 1176850
Ndiyo!Hii ni official mkuu??
Hili nalo neno mkuu, kwa akili ya Woodward haangalii kiwango, potential, Wala Nini, kwenye vitabu vya mahesabu ameshatick winger.kuhusu winga wa kulia bado naikumbuka comment yangu nilioiandika humu ndani baada ya kutangazwa usajili wa daniel james.
nilisema OGS atakuwa amefanya kosa kubwa sana la kuruhusu usajili wa bwana mdogo ikiwa ana mipango ya kusajili winga mwengine kwa sababu ed woodward hatoweza kulipa tena fedha kwa usajili wa mchezaji anayecheza nafasi ya winga.
hatimaye yametimia
sipingi sera ya kuwapa nafasi ya kucheza timu kubwa wachezaji wanaotokea kwenye academy, tatizo ni kwamba hii timu kubwa tulionao ina matatizo mengi ambayo si rahisi kutatuliwa na wachezaji wachanga.ila uhalisia ninaoona mimi Ole amechangia kwa hili suala.... issue inakuja solskjaer anaamini sana katika tabia ya kutumia makinda na kuwapa nafasi na kuwa na kikosi kidogo anachoweza kukimanage..... Katika press kadhaa alizungumzia hawa madogo na ameonesha anatamani Sana kuwatumia kwenye first team swali linalokuja hapa je wataderiver?, Nikweli wanatalent ila je wataweza kuishi na pressure ya kusemwa na media pindi wanapocheza chini ya kiwango?....
kama ningelikuwa solskjaer ningelimlazimisha sheikh woodward aniletee jadon sancho au philipe coutinho.Hili nalo neno mkuu, kwa akili ya Woodward haangalii kiwango, potential, Wala Nini, kwenye vitabu vya mahesabu ameshatick winger.
Maguire ilitangazwa rasmi, vp masho au ni posts tu za mitandao?Ndiyo!
tierMaguire ilitangazwa rasmi, vp masho au ni posts tu za mitandao?
Wanavyodai Sancho anakuja UTD Kama longterm plan, huwenda dirisha lijalo Kama tutafuzu Champions league.kama ningelikuwa solskjaer ningelimlazimisha sheikh woodward aniletee jadon sancho au philipe coutinho.
kwa jinsi bwana yule anavyopenda kiki angelitumia nguvu yoyote kufanikisha usajili huo hata kwa kumhonga wakala paundi millioni 20.
lakini unaweza kukuta bwana ole ndiye aliyekataa usajili wa majina na si ed woodward kama tunavyojiaminisha