Sijakataa kuwa mafanikio yanafaida ya kukuongezea mashabiki, lakini CITY inapoteza hadi mashabiki wake pamoja na mafanikio yote. Kikubwa nlichoona ni kuwa city inapoteza fans, na all these big spendings na izo deals ni to gain attention. Pale uwanjani wanaoenda kukaa jukwaa la city home fans wanaenda manutd fans na wengine kutizama mpira tu. Ata kuna siku city alicheza mtangazaji akauliza mashabiki watatu waliova jez za citeh kila mmoja kumbe ni shabiki wa timu tofauti. Pamoja na mafanikio yao, hata kwenye academy ya citeh kuna players wanataka kuchezea Man utd wakimaliza hapo.
City haijui kujibrand kibusiness, city is used to clean the image of the oil nations pamoja na psg yake. Miaka saba sasa inakwenda bila kuwa na mafanikio uwanjana kwa Man utd, still Utd inapata more deals than City. Hujiulizi why?
Narudia, City wapo desperate na Puma wapo ivo ivo wamekutana, Na usishangae kuwa mwarabu ameongeza hela kwenye hilo deal ili tu ahalalishe big spendings zake.
Kuhusu deal la Man utd na Adidas, wameambiwa washiriki tu UEFA champions league, so that means ata akitoka group stage deal iko pale pale hata kwa miaka minne. Hii should be enough to tell you that jamaa wanataka visibility na sio mafanikio yako tu.
Just because you are winning titles it gives you chance to negotiate. Ofcourse sponsoring the title winner has to be different from runners up.
Mpaka leo woodward anasecure better deals than Man city na tunashindana kwa nafasi ya nne tangu aondoke fergie.
Mafanikio yanakuletea fans lakini city haijapata bahati hio bado
Sorry for jumping in your arguments, kuna kitu nikieleze pia kuhusu fanbase.
Man Utd amekuwa kwenye kilele cha mafanikio for almost 2.5 decades (almost 25 years), fanbase aliyoitengeneza kwa kipindi hicho huwezi kuifuta ndani ya miaka 10.
City ndo kwanza wameanza kupata washabiki, leo hii mtaani (huku Tanzania) unaweza atleast kuona watu kadhaa wamevaa jezi ya City. Ila unaweza kumaliza wiki hujaiona ya Man Utd.
Na new age wanaoanza kushabikia mpira na kuchagua timu (10 - 20 years of age) wakipewa 2 options kati ya Utd na City under no influence, 80% wataichagua City.
Na hiyo fanbase miaka kadhaa ijayo na wao watakuwa wengi na imagine some thing like other 10 years hawa watakuwa ni purchasers, City will be having a good fanbase by then.
Na kama Guardiola anaendelea kuwepo na hao scouts waliopo, City inatengeneza identity moja ya hatari sana na ya kuvutia.
Imagine, City anacheza mchezo ambao neutrals au hata fans wa timu zingine tunainjoi kuangalia, fanbase inaanza namna hiyo.
Nani anaikumbuka Arsenal ya 2003/04, 2004/05 hata ile ya 2005/06 iliyocheza final UEFA? Timu ilikuwa inavutia kiasi kwamba hata wapinzani tinainjoi kuangalia games zao.
Kuhusu endorsement: viewerships zina-determine sana ukubwa wa deal, na City kwa EPL ni one of the most watched teams, leo hii Man Utd wanakimbia kuangalia game zao.
Miaka michache nyuma ilikuwa Man Utd akicheza hata na timu gani, mabanda ya mpira yalikuwa lazima yaoneshe game ya Utd na wanajaza, leo hii kaangalie uone wanaingia wangapi.